Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 6, 2012

MSHINDI WA JUMLA TUZO ZA TASWA KUIBUKA NA DOLA 8.000 ZA KIMAREKANI



Meneja Mawasiliano wa kampuni ya ya Serengeti, Imani Lwinga, akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa City Sports Lounge jijini Dar es salaam leo, wakati kampuni hiyo ilipotangaza zawadi kwa washindi wa tuzo za mwanamichezo bora wa TASWA, (kulia) ni  Katibu mkuu wa TASWA  Amir Mhando na (katikati) ni Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto. 
******************************
CHAMA cha waandishi wa habari  za michezo Tanzania (TASWA) kikishirikiana na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) leo wametangaza rasmi zawadi za washindi wa Tuzo hizo na vipengele vya vigezo vitakavyotumika katika kutoa tuzo za mwanamichezo bora wa mwaka 2012, zoezi litakalodhaminiwa na kampuni hiyo ya SBL.

Tukio hilo la kuwatambua na kuwatunukia Tuzo wanamichezo bora wa 2012, ambao wamejikita katika michezo na kuleta mabadiliko mbalimbali katika tasnia ya michezo litafanyika katika ukumbi wa Diamond jubilee jijini Dar es Salaam Juni  14, na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 1000.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Meneja wa mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw. Imani Lwinga amesema maandalizi juu ya tukio hilo yanaendelea vizuri, ambapo kwa niaba ya SBL Meneja huyo ameishukuru timu nzima ya TASWA kwa ushirikiano wa mzuri na kuigwa. 

“Tunatambua umuhimu na uwepo wa kila mmoja wenu katika maandalizi haya na tunajivunia kuwa sehemu muhimu katika maandalizi ya tukio hili muhimu” alisema Lwinga.

Aliongeza kuwa vipengele vilivyoanishwa katika tuzo hizo ni sahihi na kwamba kila kipengele kimewasilishwa kwa umakini mkubwa

mojawapo wa kuwatambua waandishi wa habari za michezo, lakini pia kupitia udhamini huu, tungepe kuwashauri waandishi hawa wa michezo kujaribu kuangalia mbele zaidi ili kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii juu ya tasnia hii na faida zake kwa jamii hasa hapa kwetu Tanzania”alisema Lwinga.

Vipengele vilivyoanishwa katika tuzo hizi ni kama ifuatavyo ambapoa  vilevipengele vyenye mshiriki zaidi ya mmoja ni zitahusisha zitazingatia jinsia, Mshiriki wa tuzo za dhahabu watakuwa watatu, Mchezaji wa kiwango cha juu,( wa kulipwa) na mchezaji wa kawaida nafasi mbili.

Mshindi wa jumla katika tuzo hizo atazawadiwa dola za kimarekani 8,000 zitakaoztolewa na wadhamini wakuu wa tuzo hizo Kampuni ya bia ya Serengeti

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...