Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde
muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa
maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya
Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya
Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.
|
Mjane
wa Marehemu Willy Edward akiwa kwenye majonzi mazito katika msiba wa
mumewe aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy
Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro
kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na
viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach
ni mazishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya
Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye. |
|
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha
gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto
(kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto)
wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu
Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati,
Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini
Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa.
Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na
Julius Rabach.Picha na Full Shangwe Blog |
|
No comments:
Post a Comment