Na Mwandishi wetu
KATIKA vita ya kuondoa
rushwa nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imezindua
huduma ya njia ya simu ya mkononi kwa waombaji wa zabuni mbali mbali
zinazotolewa na mamlaka hiyo.
Uzinduzi huo uliofanyika
juzi makao makuu ya PPRA chini ya Jaji Thomas Mihayo ambaye aliwaomba
watanzania kujitokeza kwa wingi kuomba zabuni hizo na siyo kulalamika
zabuni hizo zinatolewa kwa upendeleo na zaidi makampuni ya nje ya nchi.
Jaji Mihayo ambaye pia ni
kaimu mwenyekiti wa bodi ya PPRA alitolea mfano zabuni za kufua umeme
hapa nchini na ile ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambazo zilileta
usumbufu mkubwa na kuwa gumzo katika vyomo vya habari na jamii kwa
ujumla.
“Kumekuwa na malalamiko
mengi kutoka kwa wadau wetu na vile vile kutokana na watanzania wengi
kushindwa kushiriki kutokana na kukosa taarifa kwa wakati muafaka,
tumeingia makubaliano na kampuni ya Push Media Mobile na sasa kila
Mtanzania anayetaka kupata taarifa za zabuni zetu anatakiwa kujiunga kwa
kutuma neno PPRA kwenda namba 15332 na kuanza kupokea taarifa za zabuni
popote Tanzania na njie ya nchi,” alisema Jaji Mihayo.
Jaji Mihayo
alisema kuwa ili kuondoa tatizo hilo na kupanua wigo wa kutangaza zabuni
hizo, wameamua kuweka utaratibu wa kutangaza zabuni hizo kwa njia ya
ujumbe wa simu ya mkononi
Alisema kuwa kwa kutumia
utaalam huo, kila mtu anaweza kupata taarifa kuhusiana na zabuni zetu na
kuomba ili kushinda. Alisema kuwa hata kwa hata matokeo ya tenda hizo
zitatangazwa kwa njia ya uumbe huo huo.
“Kila kitu hapa
kitafanyika kwa njia ya mtandao bila ya upendeeleo wowote, tunaishukuru
kampuni ya Push Media Mobile kwa kutuwezesha taalam huu ambao utaondoa
mianya ya rushwa katika kupoke zabauni na kuchagua washindi,” alisema.
“Hii ni fursa pekee kwa watanzania kuomba zabuni zetu, lengo ni kumfikia kila Mtanzania hata aliyekuwa vijijini kwa wakati muafaka,” alisema.
Kaimu Mwenyekiti body ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Jaji Thomas Mihayo (kulia) akielekezwa jinsi ya kujiunga katika utaratibu mpya wa zabuni kwa
njia ya ujumbe wa simu ya mkononi na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Push
Media Mobile, Fredd Manento na kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk
Ramadhani Mlinga. (Picha na mpiga picha wetu).
|
No comments:
Post a Comment