Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International ambao ni waandaaji wa mashindano ya
urembo hapa nchini,Hashim Lundenga (katikati) akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya shindano la Redds Miss World
Tanzania 2012 litakalofanyika jijini Dar Es Saam katika ukumbi wa 324
Club uliopo Mikocheni,siku ya jumamosi Juni 16,2012.Kushoto ni Meneja wa
Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa
Redds Miss Tanzania na Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss
Tanzania,Albert Makoye.
Meneja
wa Kinywaji cha Redds Original,Victoria Kimaro (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo juu ya shindano la Redds
Miss World Tanzania 2012 litakalofanyika jijini Dar Es Saam katika
ukumbi wa 324 Club uliopo Mikocheni,siku ya jumamosi Juni
16,2012.Katikati ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International,Hashim
Lundenga na Kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert
Makoye.
Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo
imetangaza rasmi kudhamini shindano la kumpata mrembo atakewakilisha
taifa katika mashindano ya urembo ya Dunia mwaka huu, yanayojulikana
kama “Miss World 2012.
Akizungumzia
Udhamini wa shindano hilo linalojulikana kama “Redd’s Miss World 2012”
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International ambao ndio waandaaji wa
mashindano ya urembo hapa nchini Bw. Hashim Lundenga alisema; Ninajua
wadau wengi wa tasnia ya urembo watastuka kuona mabadiliko haya, hii
inatokana na kubadilika kwa ratiba ya mashindano ya Miss World toka
mwezi wa December ilivyokuwa ikifanyika awali na sasa yatakuwa
yakifanyika mwezi Julai hivyo kuwa na tofauti kubwa na ratiba ya
mashindano yetu ya Redds Miss Tanzania ambayo huanza mwezi Mei na
kumalizika Septemba.
Ili
tusipoteze nafasi yetu ya kushiriki mwaka huu, kamati ya Miss Tanzania
kwa ridhaa ya Serikali, iliamua kufanya shindano dogo “Mini competition”
ambalo litatupatia mshindi atakae wakilisha Taifa katika mshindano hayo
makubwa Duniani.
Warembo
10 wataingia kambini tarehe 13 hadi tarehe 17 June, na shindano
litafanyika siku ya Juma Mosi tarehe 16 June katika ukumbi mpya wenye
hadhi ya kimataifa wa 327 Club, uliopo Mikocheni. Mshindi atazawadiwa
pesa taslim shilingi Milioni mbili, na kupatiwa maandalizi yote kwa
ajili ya matayarisho ya safari yake kwenda kwenye mashindano ya Miss
World 2012 yatakayofanyika Inner Mongolia – China.
Kutokana
na umuhimu wa kufanya shindano hili tuliwaomba wadhamini wakuu wa Miss
Tanzania, kinywaji cha Redds ili watuwezeshe kufanikisha mchakato huu,
nao bila kusita wakakubali. Hivyo tunawapongeza sana Redds kwa mchango
wao mkubwa katika tasnia ya Urembo hapa nchini.
Akizungumzia
maandalizi ya shindano hilo, meneja wa kinywaji cha Redds, Bi. Victoria
Kimaro alisema; kwa upande wetu Redds, maandalizi yote yapo tayari,
tunatarajia kuwa na shindano lenye mvuto wa aina yake, na litakuwa ndani
ya ukumbi mpya wa kimataifa wa 327 kama mlivyosikia.
Shindano
hili litaanza saa Mbili usiku hadi saa Nne na litakuwa kwa waalikwa tu.
Tumeandaa burudani za kutosha na tuna uhakika waalikwa watakaokuja
kushuhudia mchakato huu wataridhika na maandalizi haya.
Mabadiliko
haya ya ratiba za Miss World yataathiri ratiba zetu kwa mwaka huu tu,
lakini yatakuwa na matunda mazuri kwetu kwa siku za usoni, kwani Redds
Miss Tanzania atakaeshinda mwaka huu atapata muda mwingi na wa kutosha
kujiandaa kwa ajili ya mchakato wa mashindano yajayo ya Miss World.
Tuna
imani kubwa kuwa wadau wa tasnia ya Urembo wataonesha ushirikiano wao
katika kufanikisha shindano hili na yote yajayo, ili kuinua tasnia ya
Urembo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment