Ngowi akiwalikisha Mradi wa Sports Tourism
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA)
limenzisha programu ya kila mwaka ya kupanda mlima Kilimanjaro ili
kuutangaza utalii wa Tanzania kote ulimwenguni.
|
Programu hiii inayofahamika kama “IBF Mount Kilimanjaro Climb Expedition” itawashirikisha manachama wote wa IBF/USBA, familia zao, marafiki na wapenzi wa IBF/USBA na ngumi kote ulimwenguni.
Akiwakilisha Mradi wa “IBF Sorts Tourism”
katika mkutano wa 29 wa shirikisho hilo uliofanyika katika jiji la
Honolulu, jimbo la Hawaii nchini Marekani, Rais wa IBF/USBA katika bara
la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi
alitaja kuwa programu hiyo itaanza rasmi mwezi wa December mwaka huu.
“IBF/USBA Mount Kilimanjaro Climb Expedition” itakuwa moja kati ya program zilizopo katika Mradi wa “IBF Sports Toirism”
ambao lengo lake ni kuitangaza Afrika kama sehemu muafaka ya kutembelea
na kuwekeza. Programu hii inaanzia katika nchi za Ghana na Tanzania
kama nchi mbili za Afrika zilizoteuliwa (Pilot Countries).Tanzania
itafaidika na mtandao mpana wa IBF/USBA ambao uko katika nchi zaidi ya
204 duniani.
Makao
makuu ya Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama cha Ngumi cha
Marekani (IBF/USBA) yako katika jimbo la New Jersey nchini Marekani.
Ofisi za Shirikisho hilo katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na
Ghuba ya Uajemi ziko Tanzania.
Kuanzishwa kwa programu hii ya “IBF/USBA Sports Tourism” pamoja na programu tanzu ya “IBF Mount Kilimanjaro Climb Expedition”
kutaifanya Tanzania kufaidika na ujio wa watalii wengi kutoka katika
mataifa makubwa kama Marekani, Canada, Brazil, Ujerumani, Uingereza,
Italia, Ufaransa, Urusi, China, Japan pamoja na chi za Scandinavia.
Watalii toka mataifa haya wanajulikana kwa matumizi yao makubwa ya
fedha.
No comments:
Post a Comment