Na Mwandishi Wetu
MSANII
nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ferouz Mrisho ‘Ferooz’ ameahidi
kuwachezesha mtindo wake wa ‘Kibodaboda’ mashabiki watakaohudhuria onyesho la
kumtambulisha Aslahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ litakalofanyika kwenye uwanja wa
Jamhuri mjini Dodoma, Jumamosi ya Juni 9, mwaka huu.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam
jana Ferooz ambaye hivi sasa anatikisa kwa sana
na nyimbo zilizo kwenye albamu yake mpya ‘Rizevu’ zilizo kwenye mahadhi ya mchiriku
alisema kuwa mashabiki wa mjino Dodoma
watapata bahati ya kuwa wa kwanza kuzisikia nyimbo zote mpya ambazo baadhi bado
hazijasikika hata kwenye redio.
Alisema
kwamba amepania vilivyo kuwaonyesha wakazi wapenzi na mashabiki wake namna ya
kucheza ‘Kibodaboda’ mtindo uliotokea kukubalika na kuifanya albamu yake mpya aliyoitoa
hivi karibuni kuwa gumzo.
“Ninawaambia
wapenzi wa wangu na wapenzi wa bongo fleva kwa ujumla wa Mkoani Dodoma wasilikose
onyesho la Dogo Aslay Live kwani nimewaandalia vitu ambavyo hawatavisahau,
nitaimba nyimbo zangu zote mpya na nitawaonyesha jinsi ya kucheza ‘Kibodaboda’,”
alisema Ferooz.
Msanii
huyo aliyepata kutamba na wimbo wa ‘Starehe’ kwa sasa anatamba na wimbo wa
’Ndege Mtini’, ulio kwenye albamu ya ‘Rizevu’ aliomnshiriki Shoz Dia wa Nyumba
ya Vipaji Tanzania (THT), pia nyimbo nyingine ni kama:
‘Tusitafutane’ aliomshirikisha Abbas
Hamisi ‘20 Pacent’, ‘Sio Ize’ na ‘Rizevu’ uliobeba jina la albamu.
Naye
Mratibu wa onyesho hilo Jackline Masano, alisema
mbali ya Ferooz, wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na wasanii kutoka
kituo cha kuibua vipaji cha Mkubwa na Wanawe cha Temeke Sandali, jijini Dar es Salaam
kilichomuibua Dogo Aslay.
“Pia
kutakuwa kundi zima la TMK Wanaume Family la Temeke jijini Dar es Salaam, Mfalme
wa Rhymes nchini Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na 20 Pacent kutoka Morogoro,
kiingilio kitakuwa sh 3,000 kwa kila mmoja atakayeingia kwenye uwanja wa
Jamhuri na onyesho hilo litaanza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 jioni, lakini saa
2:00 usiku hadi 6:00 usiku, wasanii hao wote watahamishia burudani kwenye
ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment