Men's Day Out
Aching Heart
Glamour
Uchumi wa soko huria Bongo
karibuni umechangia kukua kwa sinema za
Kiswahili. Ukipita mitaani Bongo
unakutana na filamu kila kona. Si kama miaka ileeee… tukililia sinema
hatuzioni….
Imekuwa kama mchezo bila refa, mkutano bila mwenyekiti, darasa
bila mwalimu, nyumba bila mzazi…
Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi hadi
ishirini kwa sinema; watoaji wanalipua; waigizaji hawalipwi vizuri;
utengenezaji sinema unafanywa haraka haraka.
Sinema zinatolewa ndani ya mwezi mmoja. Haraka haraka….
Wasanii
wanaigiza bila mazoezi, baadhi ya watengenezaji wanakula ngono na wasichana wazuri wazuri, sinema
zinazotolewa eti zinalinganishwa na za Wanaijeria. Tangu lini
sinema za Wanaijeria zikawa kipimo cha filamu zetu?
Pia Watanzania hatupendi au
hatununui sinema zinazotolewa na Wabongo wenzetu. Kisa? Hazituvutii. Moja ya
sababu ni kwamba zinatengenezwa vibaya kwa kulipuliwa. Sinema ikitengenezwa vizuri tuinunue,
tuifurahie, tuitolee maoni na kuitangaza. Hiyo ndiyo njia kuu itakayotufanya
tuendelee kama wenzetu, tunaowaona Miungu kutuzidi.
No comments:
Post a Comment