Mchezaji
bora wa michuano ya Airtel Rising Stars, Abdul Seleman wa timu ya mkoa
wa Temeke, akipokea kombe kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF,
Sunday Kayuni. Michuano hiyo ilimalizika juzi kwenye Uwanja wa Karume
kwa Temeke kuibuka bingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Mbeya
magoli 3-1.
Nahodha
wa timu ya wasichana ya mkoa wa Mbeya Mariam Ndauka, akinyanyua juu
kombe baada ya kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars kwa
wanawake baada ya kuifunga Arusha 1-0 kwenye fainali za Airtel Rising
Stars zilizofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam.
Nahodha
wa timu ya wavulana ya Temeke Khalid Salum, akipokea kikombe kutoka kwa
Naibu Mkurugenzi wa Michezo kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni
na Michez,o Juliana Matagi Yasoda. Temeke iliibuka mshindi wa michuano
hiyo kwa wanaume baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali iliyochezwa
kwenye uwanja wa Karume Jumapili 17 jijini Dar es Salaam.
Time
ya Temeke ikifurahia ushindi mara baada ya kuibuka kuwa washindi wa
michuano ya Airtel Rising Stars kwa kutwaa ushindi wa mabao 3-1 thidi ya
timu ya Mbeya
Wachezaji
nyota 6 wa michuano ya Airtel Rising stars wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kuchaguliwa jana katika michuano ya Finali
iliyofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Salaam.
Fainali
za taifa michuano ya Airtel Rising Stars iliyokuwa ikihusisha timu za
mpira wa miguu kwa timu za wavulana na wasichana, zilifikia tamati
Jumapili 17 kwenye Uwanja wa Karume huku timu za wavulana Temeke na
Mbeya wasichana zikiibuka mabingwa wa michuano hiyo.
Michuano
hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 pia imetoa wachezaji sita
bora ambao watahudhuria kliniki ya soka ya Kimataifa itakayokuwa chini
ya walimu kutoka Klabu ya Manchester United ambayo itafanyika Nairobi.
Wachezaji hao ni – Jackline Gibson na Irene Bahisi kutoka Arusha,
Madeline Sylvester (Ilala), Abdul Seleman, Denis Richard na Paul Balama
(Temeke).
Jumla
ya timu za shule za sekondari 24 kutoka mikoa sita zilishiriki michuano
ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu huku wachezaji bora wakichanguliwa
kuunda timu kombaini za mikoa kwa ajili ya fainali za taifa. Mikoa
iliyoshiriki ni Lindi, Mbeya, Arusha, Ilala, Kinondoni na Temeke.
Shule
hizo zilichanguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya taifa
ya shule za sekondari (UMISSETA) mwaka jana. Uzinduzi rasmi wa ARS 2012
ulifanyika Mei, kwenye Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam na
mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United ya Uingereza, Quinton
Fortune.
Fainali
za ARS za wiki moja pia zimetumika kuchangua timu ambayo itawakilisha
Tanzania kwenye michuano ya ‘inter-continental’ ambayo itashirikisha
nchi 17 ambao Airtel inafanya biashara. Michuano hii itafanyika Nairobi
mwezi wa Agosti.
Timu
ya wavulana ya Temeke imepata nafasi ya kuwa bingwa wa Airtel Rising
Stars 2012 baada ya kuifunga Mbeya 3-1 kwenye fainali kali y a kusisimua
huku wasichana wa Mbeya wakiibuka bingwa baada ya kuwafunga wenzao
Arusha 3-1. Timu hizo mbili bingwa zilijinyakulia vitabu vya thamani ya
Tshs1m, medali ya dhahabu na vyeti vya kushiriki.
Michuano
wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa
kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na
wasichana wenye miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda wa
kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao
watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel
Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza ya
Manchester United ya kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Huu ni mwaka
wa pili kwa Airtel kudhamini michuano hii. Mwaka jana, Klabu ya
Manchester United ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki
ya soka ya Kimataifa ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania, Afrika
Kusini na Gabon.
No comments:
Post a Comment