Mshambuliaji wa timu ya Mbeya chini ya umri chini wa
miaka 17 wa Mbeya Seleman Victor (kushoto) akimpiga chenga mlinzi wa
Arusha Mathew Jackson wakati wa mechi ya ufunguzi wa michuano ya Airtel
Rising Stars ngazi ya Taifa katika uwanja wa Kumbu Kumbu ya Karume
jijini Dar es Salaam Jumatatu (Juni 11, 2012). Mbeya walishinda 2-1.
Timu ya soka ya wanawake wenye umri chini ya miaka 17, imeifunga
wenzao wa Lindi 4-0 kwenye muendelezo wa michuano ya Airtel Rising
Stars uliochezwa jana asubuhi, Jumanne Juni 12.
Magoli ya Temeke yaliwekwa kimiani na mshambuliaji hatari wa timu hiyo
Fatuma Iddi kwenye dakika ya 13 na 19. Arafa Abdul waliwafungia Temeke
goli la tatu huku Niewel Halafan akimalizia kazi kwenye dakika ya 58.
Wakati huo huo, timu ya Mpira wa Miguu ya Mbeya iliifunga timu ya
Arusha mabao 2-1 katika pazia la kufungua mchezo wa fainali Ngazi ya
Taifa ya Vijana chini ya umri wa 17 yanayojulikana kama Airtel Raising
Stars uliofanyika Jumatatu, Juni 11 ya wiki hii kwenye Uwanja wa
Karume ,Dar es Salaam.Huku michuano hiyo ikiwa imetanguliwa na mechi
ya wasichana baina ya Mikoa hiyo miwili huku Mbeya wakisinda 3-2.
Timu ya Arusha ya wavulana walifungua mechi hiyo kwa kasi lakini nguvu
zao hazikuweza kuzaa matunda kabla ya vijana wa Mbeya kufunga goli
dakika ya tisa kupitia mchezaji wake Mussa Msape.Goli hilo la timu ya
Arusha liliwafanya wachezaji hao kufikiria kutimiza ndoto zao kuwa
za kweli ambapo dakika ya 24 mchezaji Shabaaan Jabir wa Arusha
aliwatoka walinda mlango wa Mbeya na kupachika goli hilo.
No comments:
Post a Comment