Marehemu Willy Edward Ogunde enzi za uhai wake.
*Yasema ni pigo kubwa kwa wadau wa habari
· *Yawataka wanahabari kumuenzi
Kampuni
ya simu ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa mshtuko na
huzuni kubwa taarifa ya kifo cha ghafla cha mwanahabari mahiri Bw. Willy
Ogunde Edward kilichotokea usiku wa kuamkia Jumatatu wiki hii.
“Tunatoa
mkono wa pole kwa familia ya marehemu, waajiri wake na kipekee familia
ya wanahabari nchini kwa kuondokewa na mpiganaji na kamanda wetu
aliyekuwa sehemu muhimu ya ujenzi wa tasnia ya habari nchini.”Alisema
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza
Marehemu
Willy Edward alikuwa ni mdau wa habari mwenye msaada na ushauri pale
anapohitajika na aliiwakilisha vyema tasnia hii ya habari tangu
alipokuwa Majira mpaka kabla umauti haujamkuta akiwa Mhariri wa habari
wa Jambo Leo.
Marehemuatakumbukwa
kwa jinsi ambavyo alikua mahiri katika kazi yake, ndani na nje ya
mipaka ya Tanzania na kwamba mchango wake utaendelea kuwa chachu hasa
kwa vizazi vijavyo vya wanahabari chipukizi nchini.
“Tutamkumbuka
sana Marehemu Willy ambae alikuwa ni mpole na mcheshi na mwenye utashi
wa mafanikio katika kazi zake. Hakusita kutoa ushauri kuboresha uandishi
wa habari ili kutoa ujumbe uliokamilika na sahihi pale alipoona
mapungufu kutika habari husika”. Alisema Meza.
Mkurugenzi
huyo Mkuu wa Vodacom amesema kampuni yake daima ina thamini na
kuheshimu mchango wa wanahabari katika maendeleo ya taifa na uimarishaji
ustawi wa jamii na kuamini kuwa wanahabari waliobaki wataendeleza
urithi (Legacy) aliouacha marehemu Willy.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Bw. Willy Ogunde Edward, mahali pema peponi –Amen.
No comments:
Post a Comment