MABOMU
ya machozi yametumika kuwatawanya wakulima wa eneo la Melela, Mvomero
mkoani Morogoro waliokuwa wamefunga barabara ya Iringa - Morogoro
wakimtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera aende kusuluhisha
mgogoro uliopo baina yao na wafugaji.
Wakulima
hao wanadai kuwa wenzao watano jana wamevamiwa na wafugaji wa kabila la
Wamasai na kuwajeruhi vibaya kwa vitu vyenye ncha kali sehemu za siri
na kupelekea kulazwa katika Hospitali ya Mkoa Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka alifika eneo hilo ambapo
wananchi hao walikuwa wamechoma matairi na kusababisha msongamano mkubwa
wa magari yaendayo Iringa na yale yaelekeayo Moro lakini wakulima hao
walikataa kumsikiliza wakimtaka mkuu wa mkoa.
Baada ya vurugu kuwa kubwa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine
Shilogile aliwaaamuru vijana wake wawatawanye wakulima hao ambao
waligoma na kuanza kuwapiga kwa mawe kitendo kilichopelekea polisi
kupiga mabomu ya machozi na kufanikiwa kuwatawanya.
Wananchi takribani 20 wamekamatwa na polisi katika vurugu hizo.
Kwa sasa hali kidogo imetulia na magari yameanza kupita eneo hilo.Chanzo DJ Sek Blog
No comments:
Post a Comment