Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, October 30, 2014

SHIWATA WAGAWA MASHAMBA KWA WANACHAMA WAKE


Msanii Maarufu nchini Ahmed Olotu 'Mzee Chilo' wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekita wa SHIWATA Cassim Taalib wa pili kushoto  walipokuwa wakigawa mashamba kwa ajili ya wanachama wao
Watakaohamia kijiji cha wasanii kupewa bustani bure

Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umetoa bure kwa wanachama wake wanaomiliki nyumba katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga ya eneo la kulima bustani.

Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa watakaonufanika na ofa hiyo ni wale watakaohamia katika nyumba zao kabla ya Desemba mwaka huu ambapo mtandao unaadhimisha miaka 10 kutoka uanzishwe.

Alisema wanachama hao wanatakiwa kufika SHIWATA kugaiwa maeneo hayo ambayo yatalimwa mazao ya muda mfupi (ambayo si ya kudumu) kama vile pilipili,mahindi, matango, pilipili hoho, mananasi, mbogamboga, matikiti maji ambayo hustawi kwa wingi maeneo hayo.

Katika hatua nyingine SHIWATA imeamua kusafisha shamba la ekari 200 ambazo zimekwisha gaiwa kwa wanachama ambao walijitokeza kulima katika shamba hilo la 500 zinazomilikiwa na mtandao huo kwa ajili ya maandalizi ya kilimo kwanza msimu huu katika kijiji cha Ngarambe, Mkuranga.

Mwenyekiti Taalib alisema SHIWATA imeingia mkataba na Kampuni ya Willy Enterprises Ltd ya Dar es Salaam kukodisha mtambo wa kusafisha shamba (Buldoza) kwa ajili ya wanachama zaidi ya 100 waliojitokeza kulima.

Alisema SHIWATA itatumia sh. mil. 22.2 kukodisha buldoza hilo kusafisha shamba la ekari 200 zilizogaiwa kwa wanachama ambapo kila mmoja atalipa gharama ya sh. 111,000 kwa ekari moja.

Jitihada za kusafisha shamba hilo zinafanywa na SHIWATA ikiwa ni maandalizi ya kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa mtandao huo utakaoadhimisha miaka 10 ya kuanzishwa mwaka 2004.

Mpaka sasa SHIWATA inao wanachama 8,000 kutoka fani mbalimbali za uigizaji, muziki wa dansi, muziki wa kizazi kipya, taarab, soka, netiboli, vijana na waandishi wa habari.
Mwanachama wa siku nyingi wa Shiwata Manase Zabron ambaye ni kocha wa mpira wa kikapu nchiniakienda kuoneshwa shamba lake
Baadhi ya viongozi wa Mtandao wa wasanii Tanzania 'SHIWATA' wakishudia ugawaji wa mashamba kwa wanachama wake juzi Ngarambe Mkulanga Mkoa wa Pwani

SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA FILAMU NCHINI


Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akiowaonyesha mabango ya filamu za Tanzania wageni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (hawapo pichani) walipotembelea ofisi za Bodi hiyo ili kujifunza namna ya Uendeshwaji wa Bodi ya Filamu jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Silyvester Sengerema.
 Kutoka kushoto ni Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya (CA) Bi. Jacquline Kinyanjui, Afisa Mult Media kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya Bi. Mercy Tepla na Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. George Charles wakisikiliza maelezo kutoka kwa uongozi wa Bodi ya Filamu Tanzania walipotembelea ofisi za Bodi hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Kenya wakiwa katika kikao cha pamoja na Watendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Picha na Frank Shija, WHVUM

Kimenuka;Wolper alijia juu gazeti baada ya gazeti kumwandika eti amekua akimtumia picha za utupu Ali kiba

                                          

Wolper alijia Juu gazeti  moja hapa  mjini baada ya gazeti kumuwandika eti amekua akimtumia picha za utupu Ali kiba.Wolper andika hivi kwenye account yake ya Instagram,tazama hapo chini

                         
                                 

Tuesday, October 28, 2014

BONDIA FADHILI MAJIA AONESHA MAAJABU KWA KUPIGWA KWA POINT THAILAND MCHEZO WA RAUNDI 12



Bondia Pungluang Sor Singyu wa Thailand kushoto akipambana na Fadhili Majiha wa Tanzania  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point
Bondia Fadhili Majiha wa Tanzania kushoto akipambana na Pungluang Sor Singyu wa Thailand  wakati wa mpambano wao wa kugombania ubingwa wa Dunia WBO Asia Pacific bantamweight title   uliofanyika katika uwanja wa shule ya Amphawa iliyopo Bangkok, Thailand Majiha alipigwa kwa point

 Na Mwandishi Wetu


akizungumzia matokeo hayo ya kupigwa kwa point bondia huyo amejigamba na kusema kuwa yeye alistaili ushindi hivyo wamempa kwa kuwa kacheza kwao na mcheza kwao utunzwa mana nilicheza kwa ustadi wa ali ya juu na wapenzi wote wa ngumi walikuwa upande wangu wakitafakali kwa nini nilinyimwa ushindi

bondia huyo ambaye anatamba sana hapa nchini kuwa akuna wa kumbabaisha ambapo anadai kukimbiwa mara mbili na bondia Fransic Miyeyusho pamoja na Nassibu Ramadhani ambao wote amewapa onyo ole wake mmoja wao akaingia anga zake atakiona cha moto kwa kuwa mechi zao nyingi wanapenda kupangiana wenyewe kwa wenyewe

nimerudi nyumbani nipo fit sina ata kovu la aina yoyote hile hivyo nitahakikisha nafanya mazoezi kuendeleza ufiti niliokuwa nao na napenda kutoa tahadhali kwa bondia yoyote mtanzania atakayejitokeza kwa sasa mbele yangu yeye atakuwa halali yangu 

nae  Kocha wake Waziri Chara amejigamba kwa kusema kuwa bondia wake ni wa kimataifa ambapo michezo yake karibia mitatu kacheza
Philippines na mwingine Thailand hivyo wao ni wa kimataifa zaidi mana mapambano aliyocheza nje yote yalikuwa magumu na raundi ni 12 ambapo zote alimaliza kwa kuwa nilimjenga katika mazingira mazuri mabondia wengi wakienda nje ya nchi wengiwao wanapigwa raundi ya kwanza ya pili awafiki ya nne

HERI YA KUZALIWA MWANABLOGU JESTINA GEORGE


Thank you, God, for giving me another year of life.
Thank you for all the people who remembered me today
by sending me wishes & gifts.
Thank you for all the experience of this past year;
for times of success which will always be happy memories,
for times of failure which reminded me of my own weakness and of my need for you,
for times of joy when the sun was shining,
for times of sadness which drove me to you.
Forgive me
for the hours I wasted,
for the chances I failed to take,
for the opportunities I missed this past year.
Help me in the days ahead to make this the best year yet,
and through it to bring good credit to myself,
happiness and pride to my loved ones,
and joy to you. Amen. 
Happy Birthday To Me.

CHIDI BENZ APANDISHWA KIZIMBANI, AKOSA DHAMANA NA APELEKWA SEGEREA


 Msanii wa muziki wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop, Rashid Makwiro, ‘Chidi Benzi’ akisindikizwa na askari Polisi wakati akiwasili katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kujibu mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na dawa za kulevya kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 
**************************************
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benzi’ leo amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la matumizi ya dawa za kulevya.

Chid Benzi, alipandishwa kizimbani majira ya saa nane mchana, mbele ya Hakimu Warialwande Lema, ambaye alimtaka msanii huyo atolewe nje kutokana na uvaaji mbaya wa suruali yake kwani alivaa ‘Kata kei’ ili avae vizuri nguo.

Akisomewa mashitaka yake, na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono, alidai kwamba mnamo 24 Oktoba 2014, Chidi Benzi alikutwa na dawa hizo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba, shitaka la kwanza linalomkabili ni kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya sh.38, 638. Pia shitaka la pili ni kukutwa na gramu 1.72 za dawa kulevya aina ya Bangi yenye thamani 1,720.

Mbali na hilo, shitaka la tatu ni kukutwa na vifaa vinavyotumika kuvutia dawa hizo za kulevya, ambapo alikutwa na Kifuu cha nazi kitupu na kijiko kimoja.

Hata hivyo, wakili huyo alidai kwamba upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika. Hakimu Lema alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 11, mwaka huu baada wadhamini kushindwa kujitokeza kwa haraka.

Hakimu Lema alisema, mshitakiwa huyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili wa kudumu pamoja na bonfdi ya Sh.milioni 1.

Hali hiyo ya kushindwa kupata dhamana ilizua hali ya simanzi kwa familia yake, kutokana na kuchelewa kujitokeza kwa wadhamini wake mbele ya Hakimu na hivyo kushindwa kupata dhamana.

Chidi Benzi alikamatwa na dawa za kulevya katika hatua ya ukaguzi kwaajili ya kupanda ndege ya Fastjet akielekea jijini Mbeya, juzi jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Msanii wa Hip Hop, Rshid Makwiro ‘Chidi Benzi’ akiingia Mahakamani leo.
Chidi Benzi akipanda karandinga kwa ajili ya kuelekea katika mahabusu ya Segerea.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA MWEZI WA WANAWAKE WAJASILIAMALI (MOWE) JIJINI DAR ES SALAAM.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, wakati aliwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 28, 2014 kwa ajili ya kufungua rasmi Maonesho ya mwezi wa Wanawake Wajasiliamali (MOWE).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya GS 1, Ester Budili, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.Oktoba 28, 2014. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi msaidizi wa Kampuni ya Kazymate, Mariam Mjewa, kuhusu Jarida maalum la ‘Mchakarikaji’  wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Chupa ya kinywaji cha Dodoma Wine wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Viatu (makubazi) na kusikiliza maelezo kutoka kwa Bi Hadija Rashid wa Kikundi cha Wajasiliamali cha Vumilia Corporation kutoka Pemba, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonesho ya Wajasiliamali, wakati wa ufunguzi wa Maonesho hayo ya mwezi ya Wanawakae wajasaliamali (MOWE) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.

MAMBO YAZIDI KUNOGA KUELEKEA TAMASHA LA KARIBU MUSIC FESTIVAL


Px 1
WASANII kutoka ndani na nje wanatarajiwa kupamba tamasha la Muziki la Kimataifa la ‘Karibu Music Festival’ litakalofanyika kwa siku tatu kwenye mji wa Kihistoria wa Bagamoyo, Novemba 7 hadi 9 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mapema Oktoba 27, Msemaji wa tamasha hilo Muslim Nassor ‘Jazzphaa’ alisema maandalizi yamekamilika na tayari wasanii wa awali waliopatikana wapo hadharani wanaendelea na matayarisho huku akiwaomba watanzania na wadau wa burudani kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo.
Jazzphaa aliwataka baadhi ya wasanii wa nje na ndani na nchi zao katika mabano ni Panda (Japan), Maria Kate (Ufaransa), IFE Pianki (Uganda), Masayo (Japan), Fantuzz (Marekani), Shiwe Musique (Comoro), Dwembede (Kenya) na Mbiye Ebrima (Guinea).
Kwa upande wa viingilio, alisema kitakuwa ni sh 5,000 kwa kila Mtanzania huku kwa atakayekata tiketi ya siku tatu, kwa pamoja, ni sh. 12,000.

“Tamasha hili litakuwa likifanyika usiku na mchana. Wasanii wote watakaokuwepo katika tamasha hili watalazimika kupiga muziki kwa kutumia ala za asili za muziki ‘Live’ na siyo ‘Playback’” alisisitiza Jazzphaa.
Kwa upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Richard Lupia alisema tamasha hilo mbali ya burudani, wasanii pia watapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuunadi muziki wao duniani kwa njia mbali mbali ambako kutakuwa na warsha kutoka kwa wataalamu toka pembe zote za dunia.

Pia alisema katika tamasha hilo kutakuwa na sanaa za Michoro, mavazi na kuchonga zitakuwa zikioneshwa eneo la tamasha.
“Semina na mijadala ya jinsi ya kuupeleka muziki wa Tanzania katika hatua nyingine za kimaendeleo zitatolewa kwa wasanii mbalimbali. Mbinu za kuuza kazi zao kwenye masoko ya kimataifa na kutafuta soko duniano kote hii itakuwa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa hapa hapa nchini” alisema Lupia.
 Makundi na majina ya wasanii kutoka nyumbani ni pamoja na Afrikabisa Band, Wahapahapa, Segere Original, Jahazi, The Spirit Band na Mama Africa.
Wengine ni Cocodo Band, Hokororo Band, Swanu Gogo Vibes, Swahili Vibes, Fimbo Band, Abeneko Music, Man Kifimbo, Saganda na Msafiri Zawose.
Wasanii wengine ni Msafiri Zawose ‘Chibite Zawose’, Tongwa Ensemble, Leo Manyika, Swahili Blues, Profesa Jay, Shilole, Juma Nature, Barnaba, Vitalis Maembe na Jhikoman.
Aidha, Jazzphaa aliongeza kuwa lengo la tamasha hilo ni kukuza na kurasimisha tasnia ya muziki kwa umakini zaidi na kukuza uchumi wa eneo la Bagamoyo ambalo ni la kihistoria. 

Msemaji wa tamasha la Karibu Music Festival, MAuslim Nassor ‘Jazzphaa’ (katikati) akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
px2
Mwanamuziki wa Msafiri Zawose anayepiga nyimbo za Cigogo, akionjesha vionjo vya moja ya nyimnbo zake kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho kwa wanahabari.
px 3
Mmoja wa viongozi wa kundi la muziki wa Pwani ‘taarab’ kutoka kundi la Jahazi, akiongea machache.
px 4
Msanii nguli wa reggae, Jiko Manyika ‘Jhikoman’ akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo.
crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii
Crew ya Karibu Festival na baadhi ya wasanii.

WAZIRI MKUU PINDA AWASILI OMAN KWA ZIARA YA KIKAZI


  
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua gwaride baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Muscut wa Royal  Airport kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Oman Oktoba 27, 2014. Kushoto ni Naibu Waziri Mkuu wa Oman Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiongozana na Naibu Waziri Mkuu wa Oman,  Mheshimiwa Sayyid Fahad Mahmoud Al Said  (kushoto kwake) baada  ya kuwasili kwenye  uwanja wa ndege wa  Kimataifa wa  Muscut wa Royal Airport kwa ziara ya siku mbili nchini humo Oktoba  27, 2014.  

Monday, October 27, 2014

RAIS KIKWETE AWASILI VIETNAM KWA ZIARA RASMI YA SIKU MBILI


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea shada la maua akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Mhe Truong Tan Sang wa Vietnam wakati wa mapokezi yake rasmi katika Ikulu ya Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa Mjini Hanoi katika siku ya kwanza ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini humo Jumatatu Oktoba 27, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam Ndugu Nguyen Phu Trong, katika Makao Makuu ya Kamati Kuu ya Chama hicho tawala cha nchi hiyo Jumatatu Oktoba 27, 2014.PICHA NA IKULU.

NECTA YAFANIKIWA KUDHIBITI UDANGANYIFU NA WIZI WA MITIHANI YA TAIFA NCHINI


 Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Bw. Daniel Mafie akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar s salaam kuhusu utaratibu wa kutoa nakala za vyeti kwa watahimiwa waliopoteza vyeti vyao ambapo utaratibu huo unahusisha uchunguzi wa uhalali wa mwombaji.  Kulia ni Afisa Habari wa NECTA John Nchimbi na kushoto ni Msaidizi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Bi Glee Magemba.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) na Vyombo vya habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ukilenga  kuonyesha mafanikio ya Baraza hilo nchini.
**************************************
Frank- Mvungi - MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa Mitihani ya Taifa na udanganyifu wakati wa Mitihani katika ngazi mbalimbali za elimu nchini.

Mafanikio hayo yametokana na ushirikiano uliopo kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya ili kutatua tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na udanganyifu wakati wa mitihani uliokuwa ukifanywa kinyume na taratibu za baraza la mitihani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo Bw. Daniel Mafie wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jjijini Dar es salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.

Akifafanunua Mafie amesema kuwa katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.

Aidha Mafie aliongeza kuwa katika Mtihani wa Kidato cha nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa Mafie alisema Baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.

Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 Baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.

Katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalam hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.

Baraza la Mitihani la Tanzania ni Taasisi ya Umma iliyochini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoanzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 21 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 1998 na 2002 kwa ajili  ya kuendesha mitihani ya Taifa kwa lengo la kuweka misingi ya sera ya mitihani, kuendesha mitihani na kutunuku stashahada mbalimbali na vyeti kwa watahiniwa wanaofuzu na kufaulu mitihani iliyo chini yake kisheria.

MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA IITWAYO MAPENZI YA MUNGU .FILAMU YAINGIA SOKONI



 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.
 Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba
Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.
--
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.

MWIGIZAJI WA KUNDI LA VITUKO SHOW AZUA TIMBWILI KANISANI



Mwigizaji wa Kundi la Vituko Show linalorusha vipindi vyake kwenye Runinga ya Channel Ten, Jasmini Emiry akiwa katika hali ya sintofahamu.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Patriki mjini hapa, mwishoni mwa wiki iliyopita, wakati wa kuaga mwili wa msanii mwenzake, Shirley Edward almaarufu Sherry Magali.
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakichukua uamuzi wa kumtoa nje ya kanisa ili ibada ya mazishi iendelee.
Awali, kabla ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu, Jasmini, akiwa benchi la mwisho nyuma sambamba na wasanii wenzake akiwemo Asha Boko na mke wa Mzee Majuto, Rehema Majuto, alionekana mwenye simanzi kupita kiasi.
Msanii Jasmini Emiry akibebwa kuelekea nje ya kanisa.
Ulipofika muda wa kuaga, Jasmini alipomaliza kulizunguka jeneza lililobeba mwili wa Sherry mbele ya madhabahu, alianguka na kuanza kurusha mateke kama punda huku akizungumza maneno yasiyoeleweka.
Jasmini Emiry akiwa amelala mbelea ya gari alilotaka limkanyage.
Baada ya kuona hivyo, baadhi ya wasanii wa Bongo Movies mjini hapa wakiongozwa na Chediel

FILAMU YA MAPENZI YA MUNGU KUINGIA SOKONI


Mwezi, Wiki na Siku zikabaki, Masaa  kwa ile Filamu Mpya na ya Kusisimua ya MAPENZI YA MUNGU Kuingia Sokoni, Sasa filamu hiyo yaingia sokoni leo ambayo imewakutanisha wasanii mahiri wa hapa hapa Tanzania ambapo Mmoja kati ya Wasanii waliocheza filamu hiyo Ni Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya anayejulikana kama Linah Sanga, kwa Kushirikiana na Elizabeth Michael bila Kumsahau Flora Mtegoha ambae ni Mama Mzazi wa Marehemu Steven Kanumba watakuwa ndani ya filamu Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU...Ni Filamu ambayo Kisa chake na Mafunzo yake yanasisimua lakini Pia ni Moja kati ya filamu ambayo kiukweli ina hadhi na vigezo vya kimataifa......

Nimefika hapa leo sio kwa Ujanja wangu Bali ni Kwa "Mapenzi ya Mungu..."
Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" ni moja ya filamu ambayo Msanii Linah pamoja na Mama Mzazi wa Marehemu Kanumba wameonyesha uwezo wa hali ya juu na kuthibitisha kuwa kweli Sanaa ni Kazi.

Filamu ya "Mapenzi ya Mungu" itakuwa Sokoni Kuanzi Wiki hii Kwa Wauzaji wa Filamu kote Nchini.

Filamu hii itasambazwa na Kampuni mahiri ya Proin Promotions Ltd.

Sunday, October 26, 2014

BONDIA SAIDI MBELWA APIGA GEORGE DIMOSO KWA POINT


Bondia Georger Dimoso kushoto akipambana na Said Mbelwa wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamoso iliyopita Mbelwa alishinda kwa point mpambano huo wa raundi nane Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Said Mbelwa kushoto akioneshana umwamba na Geore Dimoso wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi jana Mbelwa alishinda kwa point Picha na SUPER D BLOG


 Mashabiki wa mchezo wa masumbwi wakifatilia kwa makini mchezo huo
Bondia Said Mbelwa akinyooshwa mkono juu kuashilia ushindi wa mpambano huo


S
Bondia Hamza Mchanjo kushoto akipambana na Juma Fundi wakati
wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Fundi alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BLOG
Baadhi ya mashabiki kutoka Tanzani Boxing Fans Group Watssup wakijadili jambo na bondia Thomasi Mashali wa pili kushoto anae ongea nae ni Rajabu Mkamba mwenye tai
Bondia Aman Bariko 'Manny Chuga' akioneshana umwamba na Ally Bugingo wakati wa mpambano wao Bariki alishinda kwa point picha na SUPER D BLOG

Bondia Zamoyoni Mbishi kushoto akipambana na Sadiq Nuru wakati wa mpambano wao uliofanyika jana Mbishi alishinda kwa pointi picha na SUPER D BLOG


Bondia Hassan Mandula kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Mohamed Jaka Mandula alishinda kwa TKO ya raundi ya pili picha na SUPER D BLOG
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...