Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Allan Kijazi
(kulia) akimuongoza Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja
Jenerali Gaudence Milanzi kuelkea katika uwanja wa Mafunzo katika kambi
ya Mlele kwa ajili ya kufunga Mafunzo ya Wahifadhi na Askari wapya
waajiriwa wa shirika hilo .
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akipiga saluti wakati akipokea salamu za heshima wakati wa gwaride
maalumu la ufungaji wa mafunzo ya awamu ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa mfumo
wa jeshi usu.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akikagua gwaride la heshima la askari wapya na Wahifadhi waliohitimu
mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko ya mfumo wa utendaji kazi wa
kiraia kuwa mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo
Mlele mkoani Katavi.
Askari
waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya
mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa pole na kutoa heshima wakati
ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa jeshi usu kwa Wahifadhi
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akipiga saluti wakati gwarde likipita mbele ya jukwaa na kutoa
heshima,wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Wanyamapori ,Martin Loibooki,Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali
Mstaafu,Raphael Muhuga,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa,Allan Kijazi,Kaimu Mkurugenzi idara ya Wanyama pori,Ndugu
Karamaga.
Askari
waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakipita mbele ya
mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa mwendo wa haraka wakati ufungaji wa
mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi
Askari
wapya waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakionesha
umahiri katika kutumia silaha wakati wa kukabiliana na majangili mara
baada ya kupata mafunzo hayo katika kambi ya Mlele iliyopo mkoani
Katavi.
Baaadhi
ya Wahifadhi Waandamizi na Wafawidhi wakiwa wameshika silaha mara baada
ya kupatiwa Mafunzo katika Kambi ya Mlele ikiwa ni sehemu ya mabadiliko
ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kwenda Jeshi Usu.
Askari wa Hifadhi
akionesha umahiri katika matumizi ya silaha kwa kulenga shabaha wakati wa kuhitimu
mafunzo ya awamu ya kwanza ya mabadiliko
ya mfumo wa utendaji kazi wa kiraia kuwa
mfumo wa jeshi usu yaliyofanyika katika kituo cha mafunzo Mlele mkoani Katavi
Baadhi
ya Viongozi na Wageni katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa
Jeshi Usu kwa Wahifadhi na askari waajiriwa wakifuatilia maonesho
yaliyokuwa yakifanywa na wahitimu hao.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
(kulia) akiratibu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika
hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na
Asakari Waajiriwa .kushoto ni Mkuu wa Mafunzo ,Genes Shayo .
Mhifadhi Sekela
Mwangota akisoma risala ya Wahitimu wa
Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa mgeni rasmi ,Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili
na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha
mafunzo hayo kwa wahifadhi na askari wapya waaajiriwa wa shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) yaliyofanyika kwenye kambi ya Mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Wanyamapori,Martin Loibooki akizungumza wakati
wa hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi
na Asakari Waajiriwa .
Baadhi ya Wahitimu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza
wakati waa hafla ya ya ufungaji wa mafunzo ya mfumo wa Jeshi Usu kwa
Wahifadhi na Askari Waajiriwa .
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi,Meja Jenerali Mstaafu ,Raphael Muhuga akizungumza
hafla ya ya ufungaji wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi na
Askari Waajiriwa ambapo amegusia juu ya changamoto iliyopo kwa Wafugaji
kuingiza Mifugo yao katika Hifadhi pamoja na mapori ya Akiba.
Katibu
Mkuu ,Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi
akitoa hotuba yake ya kuhitimisha Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa
Wahifadhi na Askari waajiriwa wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini
(TANAPA),Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Baadhi ya Askari Waliohitimu.
Katibu Mkuu Wizara
ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa
Wahitimu wa Mafunzo ya Mfumo wa Jeshi Usu kwa Wahifadhi za Taifa(TANAPA)
yaliyofanyika kambi ya mafunzo Mlele mkoani Katavi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliyeko Katavi.