|
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi,
(kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum
cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya
michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete. |
|
|
Afisa
Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa
hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es
Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO wa
Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi
la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.
Akikabidhi vifaa
hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili
kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.
“Nyinyi mkiwa
kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,
tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza
majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya
lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,
“Nichukue
fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata
kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama
ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe
hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.
Akipokea vifaa
hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum
cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange
Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani
vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya
kiuanamichezo.
Baada ya
makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo
ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.