OMARI KIMWERI ACHOCHEA MOTO MPAMBANO WA MCHANJO NA SAYUNI WA SEPTEMBA 15 TAIFA
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Mtanzania anaefanya shughuli zake nchini austalia Omari Kimweri amechochea Moto mpambano kati ta Fred Sayuni na Haidari Mchanjo kwa kutoa vifaa vya kupigania siku hiyo mabondia hawo watakaozipiga Septemba 15 katika uwanja wa ndani wa Taifa
yeye ndie atakaekuja na vifaa vitakavyo piganiwa ulingni siku hiyo akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa Kimweri ndie atakae kuja na vifaa vya kupigania vipya kabisa siku hiyo kwa ajili ya mabondia hawo watakaozichapa kwa raundi nane ulingoni
mbali na pambano hilo rinalosubiliwa na mshabiki lukuki siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atakumbana na George Dimoso na bondia machachali Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Kidedea wakati Mohamedi Kashinde ata vaana na Sadiki Momba na Issa Nampepeche atakabiliana na Faraji Sayuni naBakari Mbede atakutana uso kwa uso na Frenk John
mapambano hayo yote na mengine yataanza saa 12 jioni yani itakuwa mapema ili ngumi hizo ziisha kwa wakati uliopangwa
siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua
mpaka kujua kitu kamili katika
mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd
Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchin