Na Mwandishi Wetu
YAKIWA wamebakia masaa machache sana kabla ya ule mtanange wa masumbwi utakao wakutanisha mabondia Haidary Mchanjo na Fredy Sayuni utakaofanyika Septemba 15 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jumamosi hii
Mabondia hao wamendelea na mazoezi na sasa wapo tayali kwa mpambano uho akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika kwa sasa wanacho subili ni siku tu ya mpambano kwani mabondia wote wapo na molali ya hali ya juu ya kutaka kupigana
na akuna bondia yoyote alieleta malalamiko kuwa awezi kupanda ulingoni siku hiyo mabondia wote tulio ingia nao mkataba wa kuzipiga watapigana siku hiyo
mbali na mpambao uho unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki lukuki kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia
Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atazipiga na Georger Dimoso na Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Kidedea Hassani Mijugu na Martn Shekivuli Mohamedi Kashinde atakumbana na Sadiki Momba na Imani Mapambano na Paul Kamata wakati Frank John atazipiga na Bakari Mbede
Mpambano uhu umepewa Baraka zote na kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa chini inayo ongozwa na Emanuel Saleh
mabondia wote watapima uzito na Afya katika soko la Vetenali lililopo Tazara siku ya Ijumaa na watacheza jumamosi katika uwanja wa ndani ya Taifa 'Indoor Stadium'