Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, January 25, 2020

SUPER D AMUANDAA SUNDAY KIWALE KWA USHINDI WA K,O JANUARY 31 TANGA ATAKAPOZIPIGA NA YOHANA MCHANJA


Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye kwa sasa anamnowa bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' kwa ajili ya mpambano wake wa kugombania ubingwa wa Dunia na Yohana Mchanja mpambano utakaofanyika January 31 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga


Akizungumza wakati wa mazoezi ya kumuandaa Kiwale amesema kuwa kiwale yupo fiti sana hivyo mashabiki waje kwa wingi wangalie mchezo wa masumbwi yaliyokwenda shule kwa kuwa Kiwale yupo vizuri kwa asilimia mia moja sina shaka nae

aliongeza kwa kusema kuwa ushindi wa Kiwale ni K,O tu kwani sisi tunaenda Tanga kama wageni hivyo tunamtaka Mchanja ajiandae kweli kweli kwani sisi tunakuja na moto wenye kazi kubwa sana  hivyo atutofanya ajizi katika mpambano huo wa ubingwa wa dania wa U.B.O lazima tutarudi n mkanda Dar es salaam kwa mazoezi tuliyofanya 

aliongeza  kuwa katika mpambano huo pia ataenda na bondia wake mwingine Hassani Mgaya atakaezipiga na Saidi Mundi mpambano wa raundi sita hivyo mashabiki wa tanga waje kuona timu ya Super D inafanya nini siku hiyo ya january 31 katika uwanja wa Mkwakwani

na bondia Sunday Kiwale amesema yeye kama bondia amejiandaa na yupo tayali kwa mchezo ata sasaivi kwani yupo fiti sana ata hivyo tuataanza safari ya kutoka dar siku ya alhamisi na tukifika siku hiyo tutamima uzito kwa ajili ya mpambano siku ya pili yake naomba wakazi wa tanga na vitongoja vyake waje kuangalia ngumi mawe masumbwi
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimfundisha bondia Sunday Kiwale 'Moro Best' jinsi ya kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'UPCAT' kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wa bondia huyo utakaofanyika january 31 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga ambapo atazipiga na Yohana Mchanja 

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimwelekeza jinsi ya kupiga ngumi zilizo nyooka bondia Sundasy Kiwale 'Moro Best' ambaye anajiandaa na mpambano wake na Yohana Mchanja utakaofanyika January 31 katika uwanja wa mkwakwani Tanga
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...