Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 11, 2011

Wakazi wa Kinyenze wakipita katika uzio







Mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Mary Nathan akipita katika njia ndogo iliyofunguliwa na mwekezaji raia wa kigeni alinayemiliki ardhi katika

eneo la kitongoji hicho kilichopo Kijiji cha Kipera Wilaya ya Mvomero

Mkoani Morogoro. Mwekezaji huyo analalamikiwa na wakazi wa kijiji hicho kufunga njia na kuvamia mashamba yao. Wakazi hao bado wanalalamika kuwanjia hiyo licha ya kufunguliwa lakini imetengenezwakama ya kupitisha mifugo kwani ni nyembamba na hairuhusiwi kupitisha gari wala pikipiki jambo ambalo bado ni kero kubwa kwa wakazi hao. (Picha na Mroki Mroki).

Mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Nuru James akipita katika njia ndogo iliyofunguliwa na mwekezaji raia wa kigeni alinayemiliki ardhi katika eneo la kitongoji hicho kilichopo Kijiji cha Kipera Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro. Mwekezaji huyo analalamikiwa na wakazi wa kijiji hicho kufunga njia na kuvamia mashamba yao. Wakazi hao bado wanalalamika kuwanjia hiyo licha ya kufunguliwa lakini imetengenezwakama ya kupitisha mifugo kwani ni nyembamba na hairuhusiwi kupitisha gari wala pikipiki jambo ambalo bado ni kero kubwa kwa wakazi hao. (Picha na Mroki Mroki).

Vodacom foundation yakabidhi madarasa mawili yenye thamani ya sh. Milioni 30 kwa Shule ya Sekondari TAI Wilaya ya Rorya Mkoani Mara







Mkuu wa Wilaya ya Rorya Bw. Benedict Kitenga (kulia) akikata utepe kufungua madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa katika shule ya Sekondari TAI wilayani humo kwa msaada wa Vodacom Foundation, (kushoto) ni Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii (Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule.

Meneja wa mfuko wa huduma za kijamii wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule (kulia) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi madarasa mawili yenye thamani ya shilingi milioni 30 yaliyojengwa kwa msaada wa mfuko huo katika Shule ya Sekondari TAI iliyoko Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, (kushoto) ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Richard Okore

MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)kufanyika Desemba 17








MKUTANO Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), utafanyika Desemba 17, 2011 eneo la Dar es Salaam Zoo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.















Kamati ya Utendaji ya TASWA iliyokutana hivi karibuni, ilifikia uamuzi wa mkutano huo ufanyike eneo hilo lililopo Kilometa 37 kutoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kuwaweka pamoja kwa siku nzima waandishi wa habari za michezo na kubadilishana mawazo kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea mwaka 2011.













Nia ya TASWA ni kumaliza Mkutano Mkuu saa nane mchana na baada ya hapo, waandishi watajumuika katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam Zoo kwa nia ya kuburudika na kutumia nafasi hiyo kupongezana kwa kazi za mwaka 2011 na kupanga mikakati ya mwaka 2012.













Kamati ya Utendaji awali ilitaka mkutano huo ufanyike Desemba 31 Bagamoyo mkoani Pwani, ili kuukaribisha kwa pamoja mwaka mpya 2012, lakini wajumbe walikubaliana ifanyike Dar es Salaam Zoo Desemba 17, kwani Desemba 31 wengi huwa wanapenda kuukaribisha mwaka na familia zao.













Kutokana na hali hiyo, TASWA inawaomba wanachama wake wote wajipange kwa ajili ya mkutano huo, ambao ajenda zake zitakuwa zile za kawaida zilizopo kwenye Katiba, ambazo ni pamoja na Ripoti ya Utendaji kwa mwaka 2010/2011, Ripoti ya Fedha 2010/2011.













Pia wanachama ambao watapenda kuwa na ajenda nyingine zijadiliwe kwenye mkutano huo wawasilishe kwa maandishi kwa Katibu Mkuu wa TASWA ama Katibu Msaidizi wa TASWA na mwisho wa kufanya hivyo itakuwa Novemba 30 mwaka huu.













Pia TASWA inawaomba wanachama wake wote kuhakikisha wanalipia ada zao za uanachama za mwaka 2011/2012 haraka iwezekanavyo na wawasiliane na Mhazini wa TASWA, Sultani Sikilo ama Mhazini Msaidizi Mohammed Mkangara na mwisho wa kufanya hivyo ni Desemba 10 mwaka huu.













Wengi wa wanachama walilipa ada kabla ya uchaguzi uliopita, ambayo ilikuwa ya mwaka 2010/2011.













Huu utakuwa Mkutano Mkuu wa Kwanza tangu uongozi wa TASWA chini ya Uenyekiti wa Juma Pinto uingie madarakani Agosti 15 mwaka jana.


http://fullshangwe.blogspot.com/

TASWA YAWASHUKURU WALIOFANIKISHA MAFUNZO YA WAANDISHI WA HABARI MOROGORO







TASWA imetoa shukurani kwa wote waliofanikisha mafunzo ya waandishi wa habari za michezo yaliyofanyika Oktoba 1 na 2 mwaka huu mkoani Morogoro na kushirikisha wadau 40.







Katibu wa TASWA Amir Mhando amewashukuru TASWA Morogoro chini ya uenyekiti wa Nickson Mkilanya kwa ushirikiano mkubwa uliowezesha kufanikisha mafunzo hayo.







Pia TASWA inawashukuru wadau wake mhariri mkongwe Said Salim, mdau Anna Kibira, mwanasheria Damas Ndumbaro, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Alfred Selengia ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya kuendeleza mpira wa wavu Tanzania kwa mada zao walizotoa kwenye mafunzo hayo.







Pia tunaishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, pamoja na Kampuni ya mabasi ya Al Saedy kwa kudhamini mafunzo hayo, tunaomba ushirikiano huo uendelee.





Juhudi zinaendelea ili kuhakikisha mafunzo yaliyopangwa kufanyika mkoani Arusha Novemba mwaka huu yanatimia kama ilivyopangwa, tunaamini hakuna lisilowezekana

Monday, October 10, 2011

CABO SNOOP WA ANGOLA NA FAMILY BONANZA DAY JANA


Mwanamuziki Cabo Snoop kutoka nchini Angola akifanya vitu vyake jukwaani huku akisasaidiwa na meneja wake kulia wakati wa tamasha la Family Day Bonanza lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leadesr Kinondoni jijini Dar es salaam na kushirikisha pia wasanii kadhaa wa nyumbani Tanzania wakiwemo Diamond, Islay na Baendi ya African Stars ya jijini Dar es salaam.
Msanii Islay akifanya vitu vyake na wimbo wake "NAENDA KUSEMA KWA MAMA" msanii huyo amekuwa akivuma kwa sasa na wimbo wake huo na kujipatia sifa kibao.
Mwanamuziki Diamond akiimba jukwaani katika tamasha hilo lililofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders.
Mambo ya Chakacha nayo yakashika kasi katika tamasha hilo kama ubavyoona katika picha hii wanenguaji hwa wakifanya mambo makubwa jukwaani.
http://fullshangwe.blogspot.com/

Taswa FC yaharibu haribu sherehe za uzinduzi wa uwanja ya uwanja wa michezo wa Boko Beach


Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa Habari za Michezo nchini, Taswa FC leo iliharibu sherehe za uzinduzi wa uwanja ya uwanja wa michezo wa Boko Beach baada ya kuichabanga timu hiyo kwa mabao 4-1.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja huo, Said Seif alifunga mabao mawili akitumia pasi safi za Majuto Omary kutoka wingi ya kulia.
Mabao hayo yaliichanganya timu ya Boko beach veterans pamoja na kumchezesha Hussein Swed wa timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Kagera Sugar.
Taswa FC ilitawala sana mchezo huo na hadi mapumziko, timu hiyo ilikuwa mbele kwa mabao 2-0. Kipindi cha pili, Boko ilifanya mabadiliko kwa asilimia 95 ya wachezaji wake na kuanza kipindi hicho kwa kasi.
Timu hiyo ilipata bao lake kupitia kwa Elly Alexander kufuatia kazi nzuri ya Swed. Bao hilo lilizua utata kutokana na waamuzi kupingana, mwamuzi wa pembeni akisema ni kona na wa kati kusema mpira huo umeingia wavuni.
Baada ya mabao hayo, Taswa FC ilikuja juu na kufunga bao la tatu kupitia kwa Hussein Omari kufuatia kazi nzuri ya Seif na bao la nne likifungwa na Ali Mkongwe kwa njia ya penati baada ya beki wa Boko Beach Veterans, Singbert Ndululu kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Katika michezo mingine, Rose Garden ililala kwa mabao 2-1 na Kunduchi na Sitakishari ilifungwa kwa mikwaju ya penati 4-2 dhidi ta TBL.
http://fullshangwe.blogspot.com/

Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amepelekwa nchini India leo


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani jijini Dar es Salaam jana(Jumamosi) mchana(picha na Freddy Maro)
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe leo amepelekwa nchini India kwa matibabu zaidi ya ugonjwa wa ajabu uliomuanza kiasi cha miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye mwili wake kunza kuvimba na ngozi kuharibika. Msemaji wa familia ambaye pia ni Mbunge wa Lupa Mh Victor Mwambalaswa amesema kwamba hali ya ngozi Dk Mwakyembe ni mbaya, japokuwa ana nguvu zake na fahamu na anaongea bila shida na anatembea mwenyewe. Viongozi kadhaa akiwemo Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli walikuwepo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar kumsindikiza Dk Mwakyembe, ambaye jana alitembelewa na Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwake Mbezi Beach. Kwa mujibu wa mke wa Dk Mwakyembe, Mama Linah Mwakyembe, daktari wa mumewe amesema mgonjwa anasumbuliwa na ugonjwa wa ngozi unaojulikana kitaalamu kama Exfoliative Dermatitis. “Alianza kuugua muda mrefu kidogo, kama miezi mitatu iliyopita, hali hiyo ilikuwa inatokea na kupotea hadi sasa ambapo hali imekuwa mbaya zaidi,” alisema. Alisema madaktari waliomfanyia uchunguzi kwa nyakati tofauti katika kipindi hicho walitoa majibu tofauti na kuongeza kuwa wapo waliosema hali hiyo ilisababishwa na kisukari na mwingine ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kulikuwa na chembechembe za sumu katika damu yake. “Baada ya ngozi yake kubadilika sana na hali kuwa mbaya, tulienda hospitali na madaktari walitupa majibu tofauti, wapo waliosema ni kisukari na kuna mwingine alisema kuna chembechembe za sumu,” alisema Linah na kufafanua kuwa daktari aliyedai hivyo hakuwapa maelezo zaidi. Kwa mujibu wa Linah, ngozi ya Dk Mwakyembe inawasha na inakuwa kama inatoa mba mwili mzima hadi kichwani.

Sunday, October 9, 2011

DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI


http://3.bp.blogspot.com/-EjllZT6LNOk/Tkj15jBW8wI/AAAAAAAAEOw/1ZDHd3LqhkQ/s1600/super+d+banner.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-EjllZT6LNOk/Tkj15jBW8wI/AAAAAAAAEOw/1ZDHd3LqhkQ/s1600/super+d+banner.jpg
DVD ZA  SUPER D BOXING COACH KUINGIA SOKONI
DVD ZA MAFUNZO YA MCHEZO WA NGUMI ZIPO MTAANI KWA AJILI YA MAFUNZO YA MCHEZO HUO HIVI SASA KWA MATAJI YA JUMLA NA REJAREJA PIGA SIMU 0787/0774/0715/0754/0733/0713-406938 AU FIKA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI 0652755838

MKENYA AMSULUBU MTANZANIA BILA HURUMA

Bondia, James Onyango kulia kutoka, Kenya akimsulubu, Abdallah Mohamed , wakati wa mpambano wa kirafiki uliofanyika, ukumbi wa DDC Keko jana, Onyango alisghinda kwa KO raundi ya nne
Bondia, James Onyango kulia kutoka, Kenya akimsulubu, Abdallah Mohamed , wakati wa mpambano wa kirafiki uliofanyika, Onyango alisghinda kwa KO raundi ya nne

TANGAZO LA DAWA YENYE NGUVU


DAWA YA NGUVU ZA KIUME NA MSIMKO KWA WANAWAKE WASIO NA HAMU YA TENDO LA NDOA AMBAYO HULETA MSISIMKO KWA WANAUME NA WAKE WAKUTANAPO.KWA SASA INAPATIKANA KWA BEI NAFUU HAPA JIJINI DAR ES SALAAM MAKUTANO YA MTAA WA KIPATA NA BARABARA YA MSIMBAZI


PIGA NO O713827689, 0755074505 , au 0719 541366

BUGURUNI LOZANA STENDI YA TAX ULIZIA ADAMU KIBANDANI 0755875884

KARIAKOO SHULE YA UHURU STENDI YA MABASI YA TANDIKA ULIZIA ZUNGU MUHUZA TIKETI 0712743870

NA UKIWA ILALA SHARIF SHAMBA FIKA DSJ BANDA NAMBA 14 SIMU 0718718671

NA UKIWA KOTA ZA BANDARI KARIAKOO FIKA MKUNGUNI KIBANDANI KWA HUSEIN 0753893295

MWANANYAMALA FIKA JABA KLABU ULIZA MACHELLAH 0713470492

ENZOY INALETA HESHIMA

Pinda akutana na Maximo Brazil


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu, Marcio Maximo kwenye hoteli ya JW MARRIOTT ya Rio deJaneiro akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil Oktoba 8,2011.

"MFALME WA BIA" PILSNER LAGER YAZINDULIWA MAISHA CLUB


Mgeni rasmi Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe wa pili kutoka kulia akigonganisha glasi na Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (wa pili Kulia) Mkurugenzi wa Masoko Bw. Ephraim Mafuru na Brand Manager Pilsner Lager Maurice Njowoka kushoto, kuashiria uzinduzi rasmi wa bia ya pilsner lager. uliofanyika jana usiku kwenye klabu ya Maisha Oysterbay jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Mauzo SBL Bw. Segun Macalauy (kushoto), Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Serengeti Breweries Bi. Teddy Mapunda (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya hiyo Ephraim Mafuru wakibadilishana wakati wakimsubiri mgeni rasmi kuwasili pamoja na wageni waalikwa
Sasa imezinduliwa rasmi.
http://fullshangwe.blogspot.com/

BALOZI MUTINDA MUTISO AFUNGUA MASHINDANO YA KENYA AIRWAYS GOLF SAFARI


Balozi wa Kenya nchini Tanzania Matiso Mutinda akipiga mpira wa Gofu wakati alipozindua Mashindano ya Kenya Airways Golf Safari kwenye viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam leo huku Meneja mkazi wa Kenya Airways Lucy Malu wa tatu kutoka kulia akishuhudia, mashindano haya yanafanyika nchi zaote za Afrika ambazo kampuni hiyo ina matawi, na mwakani washindi wote kutoka nchi 35 za Afrika watakutana pamoja mwakani na kushindana Nairobi nchini Kenya, ambapo mshindi wa kila nchi wa shindano hilo atagharamiwa kila kitu ikiwa ni pamoja na malazi kwenda kwenye mashindano hayo makubwa nchini Kenya.
Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutindo Mutiso kulia akizungumza na Lucy Malu Meneja mkazi wa kampuni ya Kenya Airways wakati wa uzinfuzi wa mashindano ya Kenya Airways Golf Safari.
Meneja mkzi wa Kampuni ya ndege ya Kenya Airways Lucy Malu akiwa katika picha ya pamoja na Mchezaji wa gofu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Aerengeti Breweriers SBL wakati wa uzinduzi wa Mashindano ya Gofu yanayoitwa Kenya Airways Safari Golf yanayozinduliwa leo katika viwanja vya Gymkana jijini Dar es salaam.
Mchezaji wa gofu Mustafa Jacks akipiga mpira wakati wa mashindano hayo yanayoendelea kwenye viwanja vya Gymkana.
Mchezaji K. Mbaya raiwa wa Kenya akipiga mpira katika mzunguko wa kwanza wa mchezo huo.
Victor Joseph akipiga mpira.

Friday, October 7, 2011

MBWANA MATUMLA AJIFUA KUMKABILI FRANSIC MIYAYUSHO

Kocha Mkongwe wa mchezo wa ngumi, Habibu Kinyogoli (kushoto) akiwaamulu mabondia, Mbwana Matumla wa pili kushoto na Mussa Sunga kupigana wakati wa mazoezi ya kambi ya Ilala kulia ni kocha wa viungo, Mohamedi Chipota Matumla anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Fransic Miyayusho litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.(PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Mabondia Mbwana Matumla (kushoto) na Mussa Sunga wakipigana wakati wa mazoezi ya kambi ya ILala Dar es salaam jana kulia ni kocha MOhamedi Chipota, Matumla anajiandaa na mpambano wake wa ubingwa na Fransic Miyayusho litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.(PICHA NA www.superdboxingcoach.blogspot.com)

NGUMI KUPIGWA DDC KEKO KESHO


Bondia, James Onyango kutoka, Kenya akipima uzito, Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wake wa kirafiki utakaofanyika na Abdallah Mohamed kushoto

ZIARA YA WAZIRI MKUU BRAZIL


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Madini na Nishati wa Brazil, Mhe. Eddison Lobao (kulia) October 5, 2011 kwenye Ofisi za wizara hiyo zilizoko Brasilia. Yuko katika ziara ya kikazi nchini humo


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikaribishwa na Waziri wa Kilimo na Mifugo (MInister for Agriculture, Livestock and Supply , Mhe. Jorge Alberto Portanova wakati alipowasili kwenye ofisi za Wizara hiyo zilizoko Brasilia kwa mazungumzo ya kiserikali akiwa katika ziara ya kikazi nchini Brazil, October 5, 2011

TBL YAKABIDHI MRADI WA MAJI WA MIL 21 SOKO LA MACHINGA MCHIKICHINI


Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akifungulia maji wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambao ulikabidhiwa kwa uongozi wa Soko la Machinga. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo ambayo imejenga mradi huo kwa sh. mil. 21.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kulia), Mkurugenzi wa Uhusiano wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) na Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu wakiwa na furaha baada ya kukabidhi mradi huo wa maji kwa uongozi wa Soko la Machinga la Mchikichini, Ilala, Dar es Salaam
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana (kushoto) akimtwisha mfanyabiashara wa Soko la Machinga la Mchikichini, Asumpta Mosha ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji uliojengwa kwa sh. mil. 21 na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Hafla hiyo ilifanyika sokoni hapo Dar es Salaam

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO WAONJA JOTO LA NHC

IKIWA ni katika muendelezo wa kukusanya madeni na kuwatoa wadeni wake Shirika la Nyumba (NHC)leo asubuhi rungu lao lilitua katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) ambapo wafanyakazi wake wamejikuta wakilazimika kutoka nje kutokana na kudaiwa kodi ya miezi saba ambayo ni kiasi cha sh.mil.47 Ilifahamika kuwa Kodi ya mwezi waliyotakiwa kulipa ni sh.mil7,149,000.Kabla ya MAELEZO kupatwa na kadhia hiyo NHC walianza katika ofisi ya Utamaduni ambako wanadaiwa sh mil87




Mwandishi kutoka Kituo cha Star TV akalazimika kufanya mahojiano na kikundi kilichokwama kufanya mkutano ndani ua Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO.
Baazi ya wapagazi wakiwa wamesimama kidogo katika zoezi linaloendelea la kutoa vitendea kazi vya MAELEZO Dar es Salaam leo zoezi ambalo linaendeshwa na NHC la kuwatoa kwa nguvu wadeni wao.
Ofisa wa Shirika la Nyumba akiomwonyesha mwandishi wa habari kutoka gazeti la Majira Mohammed Mambo karatasi iliyokuwa ikionyesha kiasi cha kodi wanachodaiwa MAELEZO na NHC.

SHIRIKA LA NDEGE LA KENYA WADHAMINI MICHUANO YA SIKU MOJA YA GOFU


Kapteni wa Klabu ya Gofu (Gymkhana Club Dra es Salaam) Joseph Tango Kulia akiwa na Meneja wa Shirika la Ndege la Kenya Ms.Lucie Malu , wakizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mchana katika ukumbi wa mikutano Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.
SHIRIKA la Ndege la Kenya jana limetangaza kutoa udhamini mnono katika michuano ya siku moja ya Gofu itakayofahamika kama KQ Golf Safari itakayochezwa katika uwanja wa Gymkhana Dar es Salaam.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana Meneja wa Shirika la Ndege la Kenya Lucie Malu alisema wao kama wadhamini wanajisikia furaha kubwa kutoa udhamini kwa wachezaji wa Gofu nchini Tanzania pia ameahidi washindi wawili watapata nafasi ya kwenda Nairobi Kenya ambako watashiriki katika fainali ya michuano hiyo iliyopangwa kufanyika Februari 2012 watakakochuana na washindi waliopatikana katika nchi zingine.

Lucie alisema shindano hilo litakalofanyika Jumamosi (Kesho) ni la siku moja ambapo litachezwa na wachezaji 100 katika mtindo wa Stable Ford yaani watacheza wanne wanne.

Lucie anasema udhamini huo ni wa kipindi cha mwaka 2011/2012 ambapo pia utajumuisha mashindano 35 ambayo yatachezwa katika nchi17 barani Afrika .

Anazitaja baadhi ya nchi hizo kuwa ni pamoja na pamoja Egypt, Cameroon , Afrika ya Kati, Accra Ghana, Cot d’Ivore na Senegal (Afrika Magharibi).

Aidha anazitaja nchi zilizopo katika ukanda wa Afrika Kusini ambapo mashindano ya KQ yatafanyika kuwa ni pamoja na Botswana, Zambia, Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini pia michuano kama hiyo itafanyika katika visiwa vya Shelisheli.

Huku akimalizia katika ukanda wa Afrika Mashariki michuano ya KQ itafanyika Kenya,Uganda na Tanzania.
Wakati huohuo Lucie alisema kwamba kutakuwa na michuano mingine ya KQ itafanyika nje ya bara la Afrika katika miji ya Bangkok , Thailand na Guangzou China.

Nishioka atetea taji lake WBC


Nishioka atetea taji lake WBC

LAS VEGAS,Marekani

MJAPAN Japan, Toshiaki Nishioka,amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa Shirikisho la Masumbwi Duniani (WBC),katika uzani wa super bantam, baada ya kumshinda mpinzani wake kwa pointi, Rafael Marquez, katika pambano lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa MGM Grand,uliopo jijini Las Vegas nchini Marekani.

Shirika la Habaria la Marekani AP,lilieleza kuwa kwa ushindi huo, Nishioka ambaye atakuwa amefikisha ushindi mara 39-4-3 yakiwemo mapambano sita aliyokuwa akitetea ubingwa wake alipata pointi 117-111, 116-112 na 115-113 kutoka kwa majaji watatu na wakati Marquez atakuwa ameporomoka kwa ushindi wa 40-7.
“Mafanikio yangu ni kutokana na kutojiweka mbali na Marquez,”alisema bondia huyo mwenye umri wa miaka 35 kupitia kwa mkalimani.

. “Ana ngumi nzito za mbali.Marquez ni mzuri kwa kukwepa makonde na ni vigumu kukwepa makonde yake yenye nguvu.Hakuna dakika ambayo niliweza kupumzika,"aliongeza bondia huyo.

Wednesday, October 5, 2011

NGUMI KULINDIMA ILALA Oktoba16




ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya Ilala, Rajabu Mhamila, 'Super D' alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala.

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.

Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka katika klabu hizo hizo

Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zai unaweza kuwa siliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298 au unaweza kuwasiliana na Super D Boxing Coach O713,0787-406938 Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...