Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, September 2, 2012

HIVI NDIVYO MWANAHABARI DAUD MWANGOSI ALIVYOPOTEZA MAISHA LEO KTK VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI

 

 


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
IRINGA, Tanzania
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari 


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote.  Francis-godwin.blogspot.com

SVG YAKABIDHI GARI LA POLISI, YASAIDIA WAENDESHA BODABODA

 

 Mwenyekiti wa Salasala Vision Group (SVG), Yahaya Mbanka
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akizungumza katika hafla hiyo.
 Waendesha bodaboda wa kituo cha Mbuyuni Kunduchi nje kidogo ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vizibao 100 vilivyotolewa na SVG kwa ajili ya kuwatambua wakati wakiwa katika maeneo yao ya kazi hususani katika eneo la Salasala
 Mwanachama wa SVG, Iman Kajula akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akimvisha mwendesha bodaboda, Patson Agustino moja kati ya vizibao maalum 100 vilivyotolewa na kikundi cha Salasala Vision Group kwa ajili ya kuwatambua waendesha pikipiki wa eneo hilo.
Gari la Polisi lililofanyiwa matengenezo na SVG
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kawe, Gilles Muroto akipokea gari la doria la  Polisi lenye namba za usajili T332 ANV kutoka kwa Mwenyekiti wa Salasala Vision Group (SVG), Yahaya Mbanka baada ya kikundi hicho kujitolewa zaidi ya sh. milioni 2 kwa ajili ya kulifanyia matengenezo gari hilo.
 Baadhi ya Askari wa doria waliohudhuriua hafla ya makabidhiano ya gari la Polisi
Inspetka Modesta Msome akitoa maelekezo kwa waendesha bodaboda wa kituo cha Mbuyuni ili kujua umuhimu wa kufuata sheria za usalama barabarani wakati wa hafla ya kutoa vizibao 100 kwa waendesha pikipiki wa eneo la Salasala, mwishoni mwa wiki

JAMHURI YA PEMBA YAIFUNGA FALCON KATIKA MCHEZO WA NGAO YA HISANI

 

 Waziri wa Afya na ustawi wa jamii wa Smz, Juma duni Haji
Waziri wa Afya na ustawi wa jamii wa Smz Juma duni Haji akifanya ukaguzi kwa timu ya Jamhuri kabla ya kuanza kwa mchezo baina yao na Super Falcon, kulia ni Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttala na Kushoto ni Makamu wa pili wa ZFA pemba Ally mohamed.Timu ya Jamhuri iliifunga timu ya Super Falcon ya pemba 3:1 kwenye mchezo uliochezwa usiku uwanja wa Amani.
 Washindi mchezo wa Ngao ya hisani ya Ligi Kuu ya Grandmalt Premier Legue ya Zanzibar timu ya Jamhuri ya Pemba wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Waziri wa Afya na ustawi wa jamii wa Smz Juma duni Haji katikati,kulia ni Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt Fimbo Buttala na Kushoto ni Makamu wa pili wa ZFA pemba Ally mohamed.Timu ya Jamhuri iliifunga timu ya Super Falcon ya pemba 3:1 kwenye mchezo uliochezwa usiku uwanja wa Amani.
 
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Smz Juma Duni Haji akimkabidhi ngao ya hisani nahodha wa timu ya Jamhuri ya Pemba baada ya kuifunga Falcon 3-1. 

WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUTOKA TANZANIA WAKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI


 

 
  Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na kuviomba vyombo vyao viweze kutambulisha timu ya wabunge hao tisa kwa watanzania ili wapate kuwafahamu kama wawakilishi wao wanaosimamia masuala ya taifa. Kulia ni Mbunge Angela Kizigha ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira katika bunge hilo. Picha na Anna Nkinda – Maelezo
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Angela Kiziga (kulia) ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya biashara na uwekezaji na kamati ya mazingira akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu tofauti ya kiuchumi na maendeleo baina ya nchi tano wanachama wa jumuia hiyo . Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wabunge hao Alhaj Adam Kimbisa.
  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki ambao wataufanyia kazi katika kikao cha Bunge kinachotarajia kuanza kesho mjini Nairobi Nchini Kenya. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji (kulia) akiongea jambo na Abdullah Mwinyi (kushoto) ambaye ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge hilo wakati wa mkutano baina yao na waandishi wa habari uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) jijini Dar es Salaam. Vikao vya Bunge hilo ambavyo ni vya wiki mbili vinatajiwa kuanza kesho jijini Nairobi Nchini Kenya
 Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki Abdullah Mwinyi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa uwanja wa Ndege unaoendelea huko Taveta nchini Kenya kwamba hauna dhamira ya kuathiri uwanja wa ndege wa Kilimanjaro. Kulia ni Katibu wa Wabunge hao Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji .
Kutoka kusho ni Mjumbe wa kamati ya mahesabu ya fedha wa bunge la Afrika Mashariki Abdullah Mwinyi,Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Alhaj Adam Kimbisa na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima
 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Twaha Issa Taslima akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki (EALA) Tawi la Tanzania Shy-Rose Bhanji (kushoto) akiwaomba waandishi wa habari waweze kutangaza umuhimu wa Bunge hilo na fursa zilizopo kwa wajasiriamali hasa wanawake. Wabunge hao waliongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (Maelezo) uliopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti, Alhaj Adam Kimbisa na  Mjumbe wa Kamati ya Mahesabu ya Fedha wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi.

MSONDO NGOMA WATOA BURUDANI KWA WAKAZI WA ILALA


Shabiki maarufu wa bendi ya msondo ngoma DKT.MBonde akitunza baada ya kukunwa na burudani za msondo ngoma

mchambuzi wa miziki ya zamani Rajabu Zomboko katikati akiimba sambamba na wanamziki wa bendi ya msondo ngoma kushoto ni Eddo Sanga na Romani Mng'ande wakati wakitumbuiza leo katika ukumbi wa max bar ilala bungoni burudan zinaendelea mpaka saa sita na nusu usiku


Saturday, September 1, 2012

SACCO - Yapatiwa Mkopo Wa Matrekta Na Benki Ya Raslimali-TIB


Matrekta 11  yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akizungumza na wananchi kisha alikabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya Mkalama, yaliyotolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB), kwa gharama ya Sh.Milioni 450.5.
Mwenyekiti wa Talanta SACCOS tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum,akifurahia trekta alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB), kupitia SACCOS hiyo.


MKUU wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akikaribishwa na mmoja wa wanachama wa ‘Talanta SACCOS’ katika kijiji cha Iguguno tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama alipoenda kukabidhi matrekta 11 yaliyogharimu Sh. Milioni 450.5.


Na: Elisante John,Singida

Wananchi wametakiwa kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo inayotolewa nataasisi za vyombo vya kifedha. Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Kone,alisema hayo wakati wa kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri, wilayani Mkalama, yenye thamani ya Sh. Milioni 450.5 kutoka benki ya raslimali (TIB). Dk. Kone alisema kupitia ushirika wakulima na wananchi kwa ujumla watanufaika na mkakati wa kilimo kwanza.Kwa upande wake mwenyekiti wa Talanta SACCOS, Myasa Salum aliishukru benki hiyo ambayo imelenga kumkomboa mkulima wa kawaida kijijini.

JWTZ MORO WAADHIMISHO MIAKA 48 KWA KUFANYA USAFI WA NGUVU KATIKA SOKO KUU LA MKOA.



Sehemu ya askari wa jeshi la wananchi la kujenga taifa (JWTZ) kutoka shule ya mafunzo na huduma Pangawe Morogoro wakieka takangumu katika lori wakati wa zoezi la kufanya usafi ndani na nje ya soko kuu la mkoa huo ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuadhimisha maadhimisho ya miaka 48 tangu kuanzisha kwa jeshi hilo ambapo kilele cheke hufanyika kila septemba mosi kila mwaka hapa nchini.
Hapa askari hao wakiwa na tenga lenye uchafu wakielekea katika lori kwa ajili ya kutupa taka hizo.
Wakikusanya uchafu uliopo chini na kuweka katika vyombo.
Kazi hiyo iliendelea katika sehemu nyingine katika soko hilo kama wanavyoonekana askari hao wakiendelea na zoezi hilo.
Askari huyu akizoa takangumu kutoka chini na kuweka katika toroli baada ya kuutoa ndani ya mtaro katika mtaa wa Uhuru unaopakana na soko kuu hilo.
Kwa kweli kazi zilikuwa nyingi sana hapa afande akisukuma toroli lenye taka hizo wakati akielekea kwenye lori.

SHULE ya huduma na mafunzo ya jeshi la wananchi la kujengataifa (JWTZ) Pangawemkoa wa Morogoro inatarajia kuadhimisha miaka 48 kwa kufanya michezo mbalimbali wakati wa kilele chicho itayofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo kesho mkoani hapa.

Akizungumza na gazeti hili mjinihapa Afisa Mahusiano wa shule hiyo Meja Henry Komba alisema kuwa jeshi hilolinatarajia kuadhimisha miaka 48 tangu kuundwa kwake kwa kufanya michezo ainasita kwa wanamichezo kushiriki michezo hiyo.

Komba alisema kuwa michezo hiyoni pamoja na soka, netiboli, wavu, kukimbiza kuku, kuvuta kamba, wavu na mashindano ya kwata.

“Tunaanzimisha miaka ya 48 tangu kuundwa kwa  JWTZ na kilele chake hufanyika kila septemba 1 na mwaka huu uongozi wa Pangawe tumefanya kazi tatu za kijamii katika maeneo matatu tofauti kwa kufanya usafi katika soko kuu la mkoa wa Morogoro, kuchangia damu katika benki ya damu hospitali ya rufaa ya mkoa na kufanya pia katika kituo cha Mgolele Bigwa” alisema Komba.

Alitaja kazi ambazo wamefanyakakuwa ni  pamoja na kufanya usafi katikakituo cha kulelea watoto yatima cha Mgolole kilichopo Bigwa, kuchangia damukatika benki ya dawa ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro na kufanya usafindani na nje ya soko kuu la mkoa huo.

Akieleza juu ya michezo hiyoKomba alisema kuwa askari wenye umri mkubwa watahusika na  michezo miwili ya kuvuta kamba na kukimbizakuku wakati vijana wa kiume wao watashindana katika mchezo wa soka hukuwasichana wakionyeshana ubabe katika mchezo wa netiboli na mchezo wa wavu.

Aliendelea kueleza kuwa katikamashindano ya kwata itajumuisha kombania aina mbalimbali na michezo hiyoinatarajia kuanza majira ya saa 2 asubuhi na kumalizika majira ya saa 7 mchana.

Komba alisema kuwa baada yakumalizika kwa michezo hiyo kutakuwa na hafla itayowakutanisha askari wotewakiwemo na maafisa wa jeshi hilo.

WAKAZI WA MUSOMA WAKUNWA VILIVYO NA UJIO WA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012


Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki, akiwajibika mbele ya mashabiki wake, kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya Viwanja vya Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Farid Kubanda a.k.a Ngosha the Swagadon, akiwaimbisha mashabiki (hawapo pichani) wake waliokuwa wamefurika kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia leo.
Msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigos 'Ray',akionesha manjonjo yake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012, muda mfupi baada ya kukaribishwa kwa ajili ya kuwasalimia baadhi ya mashabiki zao waliokuwa wamefurika ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma.
Wasanii wa Filamu Steve Nyerere (kushoto), na Aunt Ezekiel wakishindana kuonesha uwezo wa kuzungusha mauno yao katika tamasha la Sererengeti Fiesta 2012, lililofanyika kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma. 
Sehemu ya umati uliyofurika viwanjani hapo ukifuatilia kwa makini makamuzi ya wasanii hao wa Filamu, kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, mjini Musoma.
Msanii mwenye umbo kubwa katika tasnia ya filamu Bongo, Jacob Steven 'JB', akionesha uwezo wa kunengua kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 ndani ya uwanja vya Karume mjini Musoma.

CHADEMA Leo Wako Marekani-Mapokezi


mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA) Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr. II(wa pili Kushoto)akiwa na Uongozi Mzima wa Tawi la Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema DMV kwaajili ya mapokezi
mbunge wa Hai, na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa Wanawake CHADEMA Maryam Khamis wapili kulia na Katibu wa wanawake Baybe Leila, wa kwanza kushoto wakiwa katika mapokezi ya kumpokea mgeni rasm wa mkutano wa Jumamosi Mh. Freeman Mbowe.
 Mbunge wa Hai, na Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe(Wa nne Kulia) pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini(CHADEMA)Mhe. Joseph Mbilinyi(wa tatu kushoto) wakiwa na wa Chadema DMV

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh. Freeman Mbowe akiwa na baadhi ya viongozi wa Tawi la Chadema DMV aliopowasili siku ya Ijumaa Aug 31, 2012, kwenye uwanja wa kimataifa Dulles Airport, kwaajili ya mkutano utakaofanyika Siku ya Jumamosi Spet 1,2012.

Mkutana huo utaaza rasmi mida ya saa 4:PM (Kumi za Jioni) Wageni rasmi wamkutano huo ni Mhe. Freeman Mbowe na Mhe Joseph Mbilinyi ADDR. Addr: 9670 Baltimore Ave. College Park. MD 20740
Baada ya mapokezi Katibu wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Isdori Lyamuya akiongea mpango mzima wa mkutano utakaofanyika Jumamosi Sept 1, 2012 kwenye ukumbi wa Marriott Hotel Addr: 9670 Baltimore Ave. College Park. MD 20740.Picha Zote na CHADEMA
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...