Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 3, 2013

Onesmo ngwi awasili Jiji la Gaborone




Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi amewasili katika jiji la Gaborone, Botswana kupromoti ubingwa wa IBF wa Kimataifa katika uzito wa Bantam.  
Bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia mwenzake kutoka nchini Namibia Immanuel “Prince” Naidjala walitoka sare wakati wakishindania ubingwa huo katika pambano lililofanyika katika jiji la Windhoek, Namibia tarehe 20 Mei  mwaka huu.  
Ujio wa Rais Ngowi ulikuwa unangojewa na wadau wengi wa ngumi katika nchi hii tangu aitembelee Botswana mwaka 2002 wakati wa mpambano kati ya bondia wa Botswana Thuso Kubamang na Peter Malinga kutoka nchini Afrika ya Kusini.  
Rais Ngowi atakutana na viongozi wa serikali ya Botswana pamoja na wadau mbalimbali wa ngumi na safari yake itaanzia jiji kuu la Gaborone mpaka jiji la pili kwa ukubwa la Francistown ambako wadau wengi wa ngumi wanamsubiri kwa hamu.  
Nchi ya Botswana ni nchi yenye msingi mzuri sana wa ngumi za ridhaa lakini tatizo kubwa limekuwa ni namna ya kuwaendelza wanapofikia kikomo kwenye ridhaa. Kikao cha Ngowi na viongozi wa serikali wa Botswana kitaweka msingi mzuri wa namna ya kuwaendeleza mabondia wa Botswana. 
Botswana ni nchi inayopakana na Namibia kwa hiyo mpambano wa Sekotswe na Naidjala unategemewa kuwa na wapenzi wengi wa ngumi kutoka katika nchi hizi mbili.

Monday, April 1, 2013

BONDIA IDDY MKWERA AMGALAGAZA LUCAS NDULA MUHEZA TANGA



Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Iddy Mkwela wa Dar es salaam kushoto akimshambulia vikali mpinzani wake Lucas Ndula wakati wa mchezo wao uliofanyika katika uwanja wa jitegemee Muheza Mkoa wa Tanga Mkwera alishinda kwa point picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akiwa na mabondia wake walipotua katika wilaya ya Muheza Mkoani Tanga kwa ajili ya kwenda kuamasisha mchezo wa masumbwi katikati ni Iddy Nkwera na Martin Richard wote kutoka Dar es salaam picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa mchezo wa ngumi Kimataifa Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kushoto akiwa na mabondia Iddy Mkwera na Martn Richard baada ya kushuka katika gari kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi Wilaya ya Muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka wakiwa na wapenzi wa mchezo huo katika stend kuu ya mabasi hayo picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mabondia walio shiriki katika mpambano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Kocha wa mchezo wa Masumbwi Wilaya ya Muheza Charles Muhiru 'Spins' akiwa na mgeni rasmi ambaye amefanikisha kuandaa mpambano huo Allan Augastino akisalimiana na mabondia kutoka Dar picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' wa tatu kulia akiwa na baadhi ya mabondia waliocheza ngumi katika uwanja wa jitegemee muheza
Mabondia wakiwa na Super D



Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza

Mabondia wa Kutoka Muheza wakionesha shoo ya masumbwi wakati wa kusherekea sikukuu ya Pasaka katika viwanja vya Jitegemee Muheza
Bondia George Allen akinyooshwa mkono juu baada ya kushinda mpambano huo

Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo

Bondia Lucas Ndula wa Muheza kushoto akioneshana uwezo wa kuoneshana uwezo wa kutupiana masumbwi na Iddy Mkwera wa Dar es salaam katika uwanja wa jitegemee muheza wakati wa sikukuu ya Pasaka Mkwera picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Iddy Mkwera akinyooshwa mkono juu baada ya kumgalagaza Lucas Ndula wakati wa mpambano wa mabondia wa Dar na Muheza Mkwera alishinda kwa pointi mpambano hou wa raundi sita uliotahalishwa kwa ajili ya kuinua mchezo wa ngumi Wilaya ya Muheza  na kusherekea sikukuu ya Pasaka picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu

Bondia Iddy Mkwera wa Dar es salaam ameibuka mshindi baada ya kumgalagaza bondia Lucass Ndula wa Muheza wakati wa mpambano wa kuhamasisha masumbwi Wilayani Muheza uliochezwa wakati wa sikuku ya Pasaka katika uwanja wa Jitegemee

Mpambano ulioanza kwa ndula kuanza kwa kasi na kushangiliwa na wapenzi wengi katika raundi ya kwanza na ya pili upepo ulianza kumbadilikia raundi ya tatu baada ya kukata pumzi uku akitupa ngumi bila mpangilio wakati Mkwera akipanga mashambulizi na kupiga ngumi kali za kushitukiza zilizo mfanya Ndula kutulia

Raundi ya tano ilikuwa ni mfululizo wa makonde yaliyorushwa na Mkwera kwa ajili ya kumuhadhibu ndula ilipofika raundi ya sita na ya mwisho wa mchenzo ndula alipigwa upcat ambayo ilimchanganya na kufanya kuwa nje ya mchezo kwa kushika magoti

ambapo aliokolewa na kengele iliyoashilia kumaliza mpambano huo wa raundi sita na kufanya Iddy Mkwera kuibuka na ushindi wa point akipeperusha vema bendera ya Dar es salaam katika wilaya ya Muheza 

Mfadhili wa mpambano huo ambaye aliwezesha kila kitu ikiwemo kupereka mabondia kutoka Dar pamoja na ulingo maarumu kwa ajili ya masumbwi  Allan Augastino ame haidi kurudia kufanya onesho hilo la wazi katika viwanja hivyo hivyo vya Jitegemee Muheza mkoa wa tanga wakati wa sikukuu ya Iddi na kuwataka wapenzi kujitokeza kwa wiki

Mpambano huo uliofanyika katika katika viwanja vya wazi vya Jitegemee iliwavuta wapenzi wengi wakiwemo watoto ,wanawake na vijana mbalimbali waliojitokeza kwa wingi

WATU 18 WAOFIWA KUFA TIKA AJALI YA KUFUNIKWA NA KIFUSI JIJI ARUSHA



ajali (66)Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa  ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram  asubuhi ya leo
ajali (55)Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi.
ajali (44)Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo  halikupata nafasi.
ajali (65)Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
ajali (49)Hali ilivyo machimboni hapo
ajali (64)Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofia kuondokewa na wapendwa wao
ajali (21)Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
ajali (35)Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa.
---
Inakadiliwa watu zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia  kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye  malori eneo la Moshono jijini Arusha.

Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao  wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi. 
 
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni  mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso  hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo. 
 
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio. 
 
Meya wa  Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless  Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kufanya uokozi. 
 
Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho. Picha/habari Kwa Hisani ya ARUSHA255 BLOG

TASWA FC, TASWA QUEENS ZANG'ARA BONANZA LA PASAKA DAR





Mwandishi wetu
TIMU ya soka na Netiboli za Waandishi wa Habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens zimemaliza maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka kwa kishindo baada ya kuwatambia wageni wao, timu ya Kiliflora ya Arusha.
Katika mchezo wa soka, uliochezwa kwenye uwanja wa TCC Chan'ombe Taswa FC iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 wakati katika mchezo wa netiboli uliochezwa pia kwenye uwanja huo huo, Taswa Queens iliyokuwa inacheza kwa mara ya kwanza baada ya miaka 18 iliibuka na ushindi wa mabao 28-8.
Taswa FC ilianza mechi hiyo kwa kasi na kufana mashambulizi ya mengi hata hivyo, washambuliaji wake, Julius Kihampa na Shafii Dauda walikosa mabao mengi ya wazi.
Katika mechi hiyo, kipa wa Taswa FC, Said Seif alikuwa ‘likizo’ kufuatia safu ya ulinzi chini ya Muhidin Sufiani, Fred Mweta, Sweetbert Lukonge, Fred “Chuji” Mbembela kuwa imara muda wote huku safu ya kiungo ilichezwa na Ali Mkongwe, Wilbert Molandi, Majuto Omary na Evarist Hagila kutotoa mwanya kwa Kiliflora kupenya na kupeleka mashambulizi.
Baada ya kosa kosa hizo, Taswa FC iliandika bao lake la kwanza katika dakika ya 24 kufuatia gonga safi za Majuto “Ronaldo De Lima” Omary na Ali Mkongwe kabla ya mpira kumfikia Hagila na kuuweka kimiani.
Bao hilo lilionekana kuwachanganya Kiliflora na kujikuta wakipachikwa bao la pili kupitia kwa Dauda baada ya pasi nzuri ya Wilbert Molandi  aliyecheza vyema na Sweetbert Lukonge na kufanya timu hiyo kuongoza kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko.
Taswa Fc ilifunga bao la tatu kupitia kwa Hagila baada ya pasi kupata pasi safi ya Fred Mbembela ‘Chuji’ na baadaye Dauda kufunga la bao la nne kufuatia ngazi nzuri ya Majuto.
Katika netiboli, ikiongozwa na Imani Makongoro aliyecheza nafasi ya (GS), Taswa Queens iliifunika kabisa Kiliflora Queens baada ya kuongoza kwa 16-3 hadi Mapumziko.
Wachezaji wengine wa Taswa Queens waliocheza mechi hiyo mbali ya Imani ni Oliver (mwananchi), Sada Ayoub,  Johari William, Elizabeth Mbassa, Shaarifa Mustapha wote wakitokea Business Times. Timu hiyo ilikuwa chini ya makocha, Amina Mussa (BTL) na Zainab Ramadhan (TBC).
 Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto akikagua timu ya Netiboli ya Kiliflora ya Arusha, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, akikagua timu ya Netiboli ya TASWA Queens, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana.
Picha ya juu ni TASWA Fc katika picha ya pamoja na ya chini ya 
Kiliflora ya Arusha, kabla ya kuanza kwa mchezo huo jana. Picha Zote na Nasma Mafoto 
www.sufianimafoto.com

NATURE NDIYE MFALME AIBUKA MSHINDI NDANI YA DAR LIVE


Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mashabiki wa TMK Halisi, wakati wote vidole juu...TATU BILA, hata walipopagawishwa na nyimbo kali za TMK Family.
Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
JB wa TMK Halisi akicheza na mashabiki wake pia
Sir Nature (kulia) na Doro..kazini
Mhe. Temba na Chege,,,kazini


..Inspector Haroun akiwa jukwaani akiwakilisha Gangwe Mob kivyake
..Inspector anapoamua kuvua viatu na kupiga shoo peku...
..Chezea Dar Live wewe!
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akionesha manjonjo yake mbele ya mpiga gitaa wake!
...dogo Lila kutoka kundi la Nature, akiwa ni member mpya wa kundi, akichana mistari vibaya mno....
...dogo Aslay wa TMK Family akiwaimbisha mashabiki


...Profesa jay nae alikuwepo kuwakilisha vilivyo game ya Hip Hop
DJ Jd alikuwepo kwenye mashine kucheza nyimbo za Prof jay na pia kuwaonesha Ma DJ chipukizi jinsi ngoma inavyochezwa!
........shooo wa Wanaume Family ikipamba moto
DJ JD alikuwa kama jaji pia, hapa akimtangaza Nature ndiye Mfalame kama mashabiki walivyoitikia.
...Nature akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mfalme.
PICHA: Richard Bukos na Issa Mnally - GPL
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...