Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 27, 2010

MCHEZA GOFU SAYORE AIBUKA NA BLACKBERR KUTOKA ZAIN



Gidion Sayore akijiandaa kupiga mpira wakati wa mashindano ya gofu yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam. Sayore aliibuka mshindi wa jumla na kuzawadiwa simu ya mkononi aina ya Blacberry.

Gofu yamzawadia Blackberry Sayore

Na Mwandishi wetu

Gidion Sayore amejinykulia simu ya kisasa ya mkononi aina ya Blackberry baada ya kuibuka katika mashindano ya gofu yaliyofanyika juzi katika viwanja vya mchezo huo vya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Sayore ambaye ni mchezaji mkongwe katika mchezo wa gofu aliibuka mshindi katika mashindano hayo baada ya kupata pointi 31 na kumzidi mpinzani wake Simon Sayore ambaye ni mdogo wale aliyepata point 29.

Sayore ambaye ni mmoja wa wachezaji wa gofu kwa upande wa wazee katika klabu ya gofu ya Lugalo aliwashukuru wadhamini wa mchezo huo na kutoa wito kwa makampuni mengine yajitokeza kuinua mchezo wa gofu Tanzania.

“Nayaomba makampuni mengine yaige mfano wa Zain kwa kuinua mchezo huu apa nchini kwetu mchezo wa gofu ni mchezo mzuri kama unavyoona michezo mingine ni vizuri kama makampuni mengine yataona umuhimu wa mchezo huu na kuufanya uwe kama michezo mingine.,” alisema Sayore.

Mashindano hayo ambayo ushirikisha wachezaji wa rika mbalimbali yamekuwa yakifanyika kila mwisho wa wiki chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya mkononi ya Zain Tanzania.

Washindi wengine ni Priscus Nyoni , Joseph Evans, Stephania Sayore. Wasindi hao wote walijipatia zawadi mbalimbali zikiwemo seti za vyombo vya ndani na miamvuli.

Saturday, June 26, 2010

MISS ILALA KUPATIKANA LEO


Meneja Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akiwakaribisha warembo katika kitengo cha masoko cha kampuni hiyo wakati warembo hao wanaoshiriki shindano la Miss Ilala walipotembelea katika makao makuu ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania jengo la PPF Tower jijini Dar es salaam jana jioni, leo ndiyo warembo hao watapanda jukwaani kuchuana wakiwania taji la Miss Ilala 2010 kwenye shindano litakalofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza katika picha wa nne ni mtaalam wa habari Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.www.fullshangwe.blogspot.com

Friday, June 25, 2010

DR. KALIMAUGANGA AGAWA MBUZI KWA WATANGAZAJI WA MICHEZO MAGIC FM



Dr Kalimauganga kulia akimkabidhi mbuzi mtangazaji wa kituo cha radio cha magic fm leo
DR ka
mwandishi wa chanal Ten SAid Kilumanga akiwa na mbuzi aliyekabidhiwa leo na DR. Kalimauganga

Thursday, June 24, 2010

MISS UTALII TANZANIA WATAMBULISHWA RASMI LEO



Ester SAngai akiangalia moja ya dawa zinazotengenezwa na Mlonge
Capt. Shadrack Kavalambi akizungumza
Rais wa miss Utalli Tanzania Gidion Chipungahelo akizungumza na waandishi wa habari

Baadhi ya warembo wanaowania taji la miss utalii Tanzania wakiwa wamepozi wakati wa utambulisho wa mashindano hayo ambapo fainal zake zitafanyika mjini Dar es salaam


jina,Pendo Ernest
umri,22
elimu,chuo
makazi,kijitonyama
kazi,mwanamitindo
chakula,ndizi nyama



jina,Sophia Dio
miaka,22
elimu,chuo
makazi,tabata
matarajio kuwa mjasiliamali
chakula,ndizi nyama


jina, Edna Andrew
miaka,21
elimu,chuo
makazi,kimara
matarajio,kuwa mrembo wa kimataifa
chakula,wali nyama

ADEN RAGE KUGOMBANIA UBUNGE TABORA MJINI


Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya klabu hiyo Dar es Salaam, kuhusu nia yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Tabora mjini.

WAREMBO WA MISS ILALA WATEMBELEA MAGAZETI YA DAR LEO/ SPORTS STAREHE NA MAJIRA LEO


warembo wakipata maelekezo toka kwa mpigapicha mkuu wa gazeti la majira Emanuel Kwitema

warembo wanaowania taji la miss ilala wakipata maelekezo

NMB YAKABIDHI GAWIO KWA WANAHISA WAKE, WAANDISHI WATIMULIWA UKUMBINI


Katibu Mkuu wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijo (kushoto) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. milioni 721, 443, 385, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Exim, Sabetha Mwambenja, wakati wa hafla ya Benki ya NMB, kukabidhi malipo ya Gawio kwa wnahisa wake, iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi NMB, Misheck Ngatunga na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ben Christaanse.www.sufianimafoto.blogspot.com

SIMBA YAPATA KATIBU WA KUAJIRIWA MPYA


Simba SC yapata mrithi wa kaduguda

Na Shaban Mbegu

UONGOZI wa Simba, umetangaza jana ilimtangaza Katibu Mkuu mpya wa kuajiriwa, Evadus Mtawala ambaye atakuwa akifanya kazi zote za utawala za Klabu hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Aden Rage alisema Mtawala amepewa kazi hiyo baada ya Kamati ya Utendaji ya Simba kuridhika naye.

Alisema licha ya Mtawala kupewa jukumu hilo Kamati ya Utendaji pia ilimtangaza Deoniz Malinzi kuwa mlezi wa Klabu baada ya kuridhika na sifa alizonazo.

Rage alisema Kamati hiyo pia iliwatangaza wadhamini wa Klabu hiyo kuwa Ramesh Patel, Hamisi Kilomoni, Mzee Abdulahib na Abbas Sykes ambaye amekuwa mdhamini tangu Klabu hiyo ilipoanzishwa.


Akizungumzia wasifu wa Mtawala, Rage alisema kitaaluma ni mwanasheria na pia ni mtaalamu wa mambo ya komputa, lugha za Kifaransa, Kiswahili na Kiingereza.

"Huyu ndiye tunatarajia atakuwa ni Katibu wetu wa kuajiriwa, lakini kwa sasa tumempa muda wa miezi mitatu kuangalia utendaji wake, kama tutaridhika nao tutampa jukumu hilo moja kwa moja", alisema.

Katika hatua nyingine Rage ameliomba Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), kutoa ufafanuzi juu ya sheria mpya ambayo waitangaza kuhusiana na kusajili wachezaji watano wa kigeni, badala ya kumi kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Alisema kutokana Simba kukabiliwa na mashindano ya kimataifa pamoja na Ligi Kuu ndiyo maana wanahitaji kuwa na wachezaji wengi wa kigeni kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.

Wakati huo huo Rage jana alitangaza rasmi kuwania Ubunge wa jimbo la Tabora mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Uchaguzi Mkuu ujao unatarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.

KOMBE LA DUNIA MIAMBA YAZIDI KUCHUANA



Mchezaji Clint Dempsey wa USA na Karim Zian wa Algeria wakigombea mpira

England NA Ghana ZAINGIA 16 BORA



Wachezaji England wakishangilia baada ya kufunga goli
England, Marekani zapeta 16 Bora

Maumivu yaendelea kwa timu za Afrika

PORT ELIZABETH, South Africa

HATIMAYE timu za England na Marekani, jana zilikata tiketi ya kucheza hatua ya mtoano katika mashindano ya Kombe la Dunia, yanayofanyika nchini Afrika Kusini kwa kila moja kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya wapinzani wao.

Kwa matokeo hayo timu hizo, zilifanikiwa kutuliza mzuka za mashabiki wao, ambao walikuwa hawana raha kutokana na kuanza vibaya michuano hiyo, inayofanyika kwa mara ya kwanza katika bara la Afrika

Ikicheza mechi yake ya mwisho hatua ya makundi England ikiwa Kundi C, ilipata goli lake pekee kupitia kwa mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe, dhidi ya Slovenia ambayo nayo ilikuwa ikipambana ili kupata ushindi.

Defoe ambaye alicheza kuanzia mwazo, aliunganisha mpira wa krosi kutoka kwa James Milner katika dakika ya 23 na kuifanya Englad, kupata ponti tatu na kufikisha tano na kuwa kinara wa kundi hilo

katrika mechi ilichezwa mjini Pretoria.

Slovenia iliyokuwa kinara wa kundi C, ikiwa na pointi nne imejikuta kitumbua chake kikiingia mchanga kutokana na Marekani nayo kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Algeria iliyokuwa na pointi moja na kuchumpa hadi nafasi ya pili hivyo yenyewe kuachwa nje.

England ilicheza mechi hiyo kwa umakini, huku ikizuia kufungwa na huku ikishambulia toka mwanzo.

Bao la Marekani iliyokuwa ikicheza katika Uwanja wa Loftus lilifungwa na Landon Donovan, ambaye alimpiga chenga kipa wa algeria, Rais Bolhi katika dakika za majeruhi, baada ya kutema shuti la Clint Dempsey.

Hilo lilikuwa ni goli la nne kwa Donovan katika fainali hizo za Kombe la Dunia, akiwa sawa na Bert Patenaude wa Marekani pia.

England sasa katika hatua ya mtoano itacheza na mshindi wa pili kutoka kund D, lenye timu za Australia, Serbia, Ghana na Ujerumani. Wakati Marekani itacheza na mshindi wa kwanza wa Kundi D.

Leo katika mfululizo wa mashindano hayo Kundi F: Paraguay itachuana na New Zealand na Slovakia itacheza na mabingwa watetezi Italia saa 11 jioni.

Usiku saa 3:00, Cameroon itachuana na Uholanzi na Ghana itacheza na ujerumani. Ghana inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne.

MREMBO MWENYE KIPAJI KINONDONI KUPATIKANA JUMAPILI


Mrembo mwenye kipaji Kinondoni kusakwa Jumapili

Na Mwandishi Wetu

WANYANGE wanaowania taji la Redd's Miss Kinondoni 2010, Jumapili wanatarajia kupanda jukwaani kumsaka mrembo mwenye kipaji 'Miss Talent 2010'.

Akizungumza Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Kinondoni, Yusuf George alisema kila kitu kuhusu mashindano hayo yamekamilika na kinachosubiriwa ni kumpata mnyange mwenye kipaji.

Mwenyekiti huyo alisema mshindi atakayepatikana katika kinyang'anyiro hicho atatangazwa katika fainali za mashindano ya Redd's Miss Kinondoni 2010.

"Kila kitu kinakwenda vyema kuhusiana na mashindano haya ya kumsaka Miss Talent 2010, kinachosubiriwa sasa ni Jumapili ifike ili kumpata mshindi," alisema Mkurugenzi huyo.

Yusuf alisema mashindano ya kumsaka Miss Talent yatafanyika katika ukumbi wa hoteli ya Geraffe Ocean View iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam.

Akizungumzia mashindano ya Redd's Miss Kinondoni, Yusuf alisema mashindano hayo yatafanyika Julai 2, mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City.

Alisema washiriki wote wapo katika hali nzuri na kila mmoja anajitapa kunyakua taji la kanda hiyo, ambayo inaoongoza kwa kutoa Miss Tanzania na pia mwaka 2005, Miss Kinondoni alifanya vizuri Miss world kwa kuweza kutwaa taji la Miss World Afrika.

Wednesday, June 23, 2010

MACHESTA SOUND YATAMBULISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI LEO


wanenguaji wa manchesta


WAnenguaji wa bendi ya Manchesta wakiwajibika wakati wa utambulisho wa bendi hiyo kutoka kushoto ni Kulwa Adamu Amina Remmy na Mariam Hassani


Waimbaji wa bendi ya Manchesta wakiwajibika wakati wa utambulisho wa bendi hiyo mbele ya waandishi wa habari Dar es salaam kushoto ni Yahana Zungufya na Amina Remmy

shindano la Kombe la Dunia Trivia SMS, la voda com yapata mshindi


Ully Mwaipopo mkazi wa kimara akipokea zawadi ya Luninga aina ya LCD nchi 32 iliyounganishwa na king’amuzi cha DSTV kutoka kwa mtaalamu wa bidhaa wa Vodacom Tanzania Joe Bendera (kulia) kwa niaba ya mshindi wa shindano la Kombe la Dunia Trivia SMS, Ganga Mlipano. Katikati ni Afisa Huduma wa DSTV, Carlos Amri,Vyote vikiwa na thamani ya Milioni 1.6 picha na www.fullshangwe.blogspot.com

CHUO KIKUU MUHIMBILI CHAZINDUA BAABARA YA TIBA ASILIA




wadau wa tiba
Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Muhimbili Dkt. Modest Kapingu (kulia) akizungumza na Balozi waSwitzerland nchini Bw. Adrian Schlapfer katikati ni Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Muhimbili.Prof. Kisali Palangyo baada ya uzinduzi wa maabara ya chuo hiko Dar es salaam
Balozi waSwitzerland nchini Bw. Adrian Schlapfer (kulia) akikata utepe kuashiria kuzindua maabara ya Tiba za ASili Dar es salaam jana kushoto ni Makamu Mkuu wa chuo Kikuu Muhimbili.Prof. Kisali Palangyo

KLABU MAISHA KUANZA KAZI KESHO





Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa klabu ya Maisha ambayo ilikuwa imeteketea kwa moto miezi michache iliyopita na leo itaanza maonesho yake rasmi baada ya kusimama kwa mda

KLABU ya Usiku ya Maisha inatarajiwa kufunguliwa tena hii Kesho kuendelea na shughuli zake za burudan baada ya kufanyiwa marekebisho upya tangu kuungua kwake.

Maisha Club iliyokuwa ikiendesha burudan nyakati za usiku uliungua kufuatia ajali ya moto na kufanyiwa marekebisho tena kuanzia Januari 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Dj Majay) alisema ukumbi huo kwa sasa umeboreshwa zaidi tofauti na awali kutokana na kuweka mbele tahadhari kwa ajili ya usalama wa wateja wao.

Alisema maboresho hayo yametokana na kuangalia hasara kubwa ambazo zinaweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kudhuru afya za wateja wao na matatizo mengi na kuamua kuingia gharama zaidi katika ujenzi na maboresho.

"Baada ya kuangali juu ya ajali ile ya moto, tukaona kuwa kuna mambo mengi ambayo yalikosewa kitu kilichofanya kuanza upya ujenzi wa kisasa wa jengo maalum la shughuli za buruda nyakati za usiku (Night Club) ambayo itakuwa na hadhi ya kimataifa.

"Hilo likatufanya kuingia gharama zote ambazo kwa sasa zinafanya ukumbi huu kuwa wa kisasa zaidi na kama unavyoweza kuwa wa kisasa ukilinganisha na nyingine kubwa ndani na nje ya Tanzania," alisema mkurugenzi huyo.

Jengo hilo la sasa lenye vitu mbalimbali vilivyoongezwa kama luninga zilizounganishwa na channel za kimataifa za burudani, sehermu maalum za kuvuti sigara, vyumba saba vya kuuzia vinywaji, imegharimu kiasi cha zaidi ya bilioni 2.2 mpaka sasa inapokamilika.


Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Entertainment Masters inayomiliki klabu hiyo, Francis Anthony Ciza (Majey),akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi rasmi wa Club Maisha,shoto ni Meneja wa Club hiyo Allan Ngugi
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...