Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, July 26, 2010

TTCL KUJIULIZA SHIMUTA SEPT ARUSHA


TTCL WAKIWA WAMEBEBA BANGO
TTCL WAKIWA UWANJANA NA CBE
wafanyakazi wa TTCL wakifulaia bonanza

TIMU ya netbol ya Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) mwishoni mwa wiki ilishindwa kufua dafu baada ya kupata kichapo cha mabao 12.6 kutoka kwa timu ya Chuo cha Biashara (CBE) katika Bonanza lililoyakutanisha mashirika na makampuni mbalimbali lililoandaliwa na (SHIMUTA)

Akizungumza katika viwanja vya Chuo Kikuu cha DAr es salaam baada ya kupata kipigo Ofisa Habari wa kampuni ya TTCL Amanda Luhanga, amesema kampuni hiyo imepata changamoto baada ya kichapo hicho ambapo hitakuwa kama chachu ya kuanzisha timu ya kudumu katika kampuni hiyo

;Unajua tangu kampuni ibinafsishwe hatukuwa na timu pamoja na kufungwa tunaona bado tuna huwezo wa kushindana katika michuano mingine itakayokuja mbele yetu tuna huwakika tukifanya mazoezi ya kutosha na kujipanga kama timu tutaludisha historia yetu ya kimichezo ; alisema Luhanga

Amesema kuwa mikakati ambayo TTCL ITAIWEKA NI PAMOJA NA KUWANOWA WAFANYAKAZI KATIKA MICHEZO MBALIMBALI PINDI AMBAPO WATAKAPOTENGA MUDA WA MAZOEZI ILI KUWEZA KUFANYA VIZURI;

'Tunataka tuwe na vikosi kazi ambavyo vitashiriki rasmi katika mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) alisema mashirika yaliyoshiliki bonanza hilo ni pamoja na TTCL,CBE,PSF,TBC,COCA COLA,ARDHI,BANDARI NA BIMA YA AFYA

TWIGA STARS YAREJEA BAADA YA KUFUNGWA NA BANYANA BANYANA


wachezaji wa twiga wakiwasili jana baaba ya kufungwa

ASHANTI UNITED YAFANYA HITMA YA KUWAKUMBUKA WADAU NAKUMWAGA MPUNGA WA NGUVU


MGENI RASMI WA HITMA HIYO SHEIKH WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALHDI MUSSA SALUM AKITOWA NENO NA KUTAKA UWANACHAMA WA ASHANT UNITED
VIONGOZI NA WADAU WALIKUWEPO
SHEIKH MAULANA ABUBAKAR AKITOA MAWAIDHA
baadhi ya watu waliokuwepo

Sunday, July 25, 2010

MAPACHA WATATU KUTOA ALBAMU NYINGINE


Mapacha watatu tukiwa katika pozz la picha.toka shoto ni Khalid Chokoraa,Jose Mara mtoto wa kimara pamoja na Kalala Junior

ASHANTI UNITED KUMKUMBUKA MAREHEMU DITOPILE LEO MCHANA


KATIBU Mkuu wa klabu ya AShanti United ya jijini Dar es salaam Haji Bechina (kulia)kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea dua marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam akiwemo marehemu DITOPILE

ZANTEL YAFUNGUA DUKA JIPYA LA BIDHAA ZAO


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Leonard Gama akifunguwa rasmi duka jipya la Zantel lililopo maeneo ya Masaki mkabala na hoteli ya Sea Cliff. Kulia kwake ni Afisa Mkuu wa Biashara Zantel Nitish Malik.

WACHUHUZI WA SAMAKI WAKIENDELEA NA KAZI


Wachuuzi wa samaki wakipala samaki bila kuoshwa kutokana na kukuosekanakwa maji baada ya maji ya baharini kujaa mafuta ya Disel kutokana na bomba la kupitishia

ZAIN WAPATA WASHINDI WA JIVUNIE SMS


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya simu ZAIN Muganyizi Mutta akizungumza na waandishi wa habari WAKATI WA KUCHEZESHA DROO YA JIVUNIE SMA KULIA NI BAKARI MAGGID KUTOKA BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA

Friday, July 23, 2010

MASHINDANO YA POOL NGAZI YA MKOA YANAYODHAMINIWA NA SAFARI LAGER YAMEANZA RASMI JANA


Mchezaji wa mchezo wa pool wa timu ya topland, Omari Akida akijataarisha kupiga mpira wakati wa mashindano ya mchezo uho ngazi ya mkoa iliyoanza Dar es salaam jANA

ZANTEL HYUNDAI WAONESHA GARI YA MSHINDI WA PROMOSHENI YA DONDOKA SAUZ



Meneja mauzo wa Hyundai Antony Nyeupe (kulia) akimwonesha gari itakayoshindaniwa na wateja wa kampuni simu ya Zantel Meneja Masoko wa Zantel wiliam Mpinga Dar es salaam jana zawadi hiyo himetolewa na kampuni

HYUNDAI/ZANTEL WAZINDUWA ZAWADI KUBWA YA PROMOSHENI YA DONDOKA SAUZ
Dar es Salaam, Julai 23, 2010: Kampuni ya magari ya Hyundai wakishirikiana na kampuni ya Zantel leo wamezinduwa Zawadi kubwa itakayotolewa kwenye droo ya mwisho ya promosheni yao inayoendelea ya Dondoka Sauz. Zawadi hiyo ni gari jipya aina ya Hyundai Tucson ix35 muundo wa mwaka 2010 yenye thamani ya milioni 50 fedha za kitanzania.
Gari lipo makao makuu ya Zantel jijini Dar es Salaam na linaonyeshwa bure kwa umma. Gari hili lina vikorombwezo vya hali ya juu vilivyowekwa kuhakikishia usalama. Meneja Mauzo wa Hyundai Anthothy Nyeupe akielezea vikorombwezo hivi alisema “Gari hili limetengenezwa kutoa ufahari na vikorombwezo ilivyonavyo ni kama kadi ya kuwashia gari, uwezo wa kushika breki yenyewe kwenye mteremko au mlima, breki za dharura pamoja na vioo vya pemeni kwa ajili ya usalama.”
Akielezea jinsi ya kushriki promosheni hii, Mkurugenzi Masoko wa Zantel Ikechukwu Kalu alisema “Ili kushiriki promosheni hii, mteja wa Zantel anahitaji kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno FIFA2010 kwenda namba 15726 na moja kwa moja watakuwa wameingizwa kwenye promosheni hii. Promosheni hii ni kwa ajili ya wateja wa zamani na wapya wa Zantel na kwa wale wasio wateja wa Zantel wanachotakiwa kufanya ni kununua sim kadi ya Zantel na kuanza kutuma message nyingi kujiwekea nafasi nzuri za kushinda. Zawadi kuu ya promosheni hii ni gari mpya aina ya Hyundai Tuscon ix35 muundo wa mwaka 2010.”
Droo ya mwisho ya mwisho itafanyika LIVE makao makuu ya Zantel Jumatatu tarehe 9 Agosti, 2010 na mshindi mmoja atabahatika kujishindia gari jipya aina ya Hyundai Tucson ix35 muundo wa 2010 lenye thamani ya milioni 50.

Thursday, July 22, 2010

VODACOM FOUNDATION KUDHAMINI GALA NIGHT ZANZIBAR


Meneja wa Mfuko wa Vodacom fondition, Yessaya Mwakifulefule 8kushoto na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali wakizungumza na waandishi wa habari

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na mbunifu wa mavazi Mstapha Hassanali imejitokeza kudhamini maonesho ya mavazi ya hisani yanayolenga kuboresha hali ya mazingira ya Hospital ya wenye matatizo ya akili ZANZIBAR.

Maonesho hayo yanayofahamika kama 'Fashion 4 Health Black and Gold Gala' yanafanyika mara ya tatu mfururizo yanaandaliwa na Exprlore ZANZIBAR yatafanyika tarehe 30 Julai mwaka huu katika Hotel ya Serena Inn Mjini humo.

"Kwa kuthamini umhimu wa jamii ambayo tunafanya nayo kazi na kwa Heshma ya Maryam Olsen wa Explore Zanzibar tumeshawishika kudhamini onesho hili kuchangia majengo ya Hospitali hiyo," alisema Mwakifulefule.

Naye mbunifu maarufu wa mavazi nchini Mstafa Hassanali alisema katika maonesho hayo atazindua mtindo wake mpya wa mavazi unaofahamika kama 'KARAFUU Collections', akiambatana na wanamitindo wengine 10 kutoka Tanzania bara wakisindikizwa na burudani kutoka katika bendi ya Tanzanite.

Alisema mbunifu mwingine wa Mavazi Farouque Abdella wa zanzibar atafungua pazia la maonesho hayo akifuatiwa na mbunifu Mago ambapo wadhamini mbalimbali wakiwemo PSI Tanzania, 361 degree Events na Mstapha Hassanali Couture wamejitokeza kudhamini maonesho hayo.

"Wagonjwa wana kila sababu ya kujifunza na kuishi katika mazingira ya kupendeza lakini tunahitaji msaada na mimi kwa kushirikiana na wenzangu tutashiriki kikamilifu katika onesho hilo kuchangisha fedha," alisema hassanali.

POLISI KANDA MAALUMU YAKAMATA SILAA TATU


Kaimu Kamanda wa polisi Kanda maalumu Dar es salaam.ACP Charles Kenyela (kushoto) akionesha silaha tatu pamoja na risasi zake zilizokamatwa kutoka kwa watuumiwa wa ujambazi 26 waliowakamata kulia ni Naibu mratibu wa jeshi la polisi, Ally Mnzava's

YANGA YAKABIDHIWA VIFAA VIPYAA


wacheyaji wa yanga wakijaribu
Editha Mushi akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Katibu Mkuu wa yanga Lawrence Mwalusako Dar es salaam jana, kwa ajiri ya kujiandaa na msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara katikati ni Mwenyekiti wa klabu hiyo, Lloyd Nchunga

ASHANTI UNITED YAANDAA DUWA YA KUMKUMBUKA MAREHEMU DITOPILE


Haji Bechina kushoto alipotembelea mayoeyi za Ashanti boxing kulia ni Iraki Hudu


Na Mwandishi wetu

KATIBU Mkuu wa klabu ya AShanti Unidet ya jijini Dar es salaam Haji Bechina kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo wamepanga kuwaombea duwa marehemu wote waliowahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa klabu hiyo itakayofanyika katika shule ya msingi Boma Ilala jijini Dar es salaam

Akizungumza na waandishi wa habari jana Bechina aliwataja watakaosomewa duwa hiyo kuwa ni pamoja aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Tabora, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri aliyekuwa Mlezi wao RAjabu Mgodo, Athumani Nobi waliokuwa makatibu katika vipindi tofauti na Mzee Mwalimu Kinyogori ambaye alikuwa mwenyekiti

Bechina alisema kuwa klabu zote za mpira wa miguu zilizopo jijini DAr es salaam pamoja na wadau wa mchezo wa soka wamepewa miariko kwa kushiliki duwa hiyo itakayofanyika jumapili hii ya julay 25

Aidha klabu hiyo imepanga kuisuka upya timu ya soka ya AShanti United baada ya kupoteza mwelekeo miaka ya hivi karibuni

Mbali na soka AShanti pia hujishughulisha na uinuaji wa vipaji vya mchezo wa ngumi kupitia kocha Rajabu Mhamila Super D

Bechina aliongeza kuwa wanajivunia timu hiyo ya ngumi ambako mchezaji wao Joseph Richard, alimpiga kwa KO ya raundi ya pili Kijepa Omari katika pambano la utangulizi kabla ya Rashidi Matumla na Mada Maugo kwenye ukumbi wa P.T.A, Ndani ya viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam

Wednesday, July 21, 2010

KAMPUNI YA ZAINI KUBADIRISHWA JINA KUWA BHARTI AIRTEL



baadhi ya wapiga picha walikuwepo kusikia ujio wa kampuni mpya ya simu
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Zain Bi. Beactice Mallya akizungumza na waandishi wa habari kuusu kubadilishwa kwa kampuni ya Zain kuwa Bharti Airtel Dar es salaam wengini ni Mkurugenzi Mtendaji wa bharti airtel Bw. Sam Elangallor,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Manoj Kohli na ofisa wa Kampuni hiyo Bw.Jayant Khosla

SIMBA WAKABIDHIWA VIFAA KWA AJIRI YA KUTETEA UBIGWA WA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya simba, Geofrey Nyange(kushoto) akipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa Meneja wa bia ya kilimanjaro, George Kavishe na Meneja Uhusiano wa kampuni ya bia ya TBL, Editha Mushi Dar es salaam jana kwa ajiri ya kujiandaa na ligi kuu itakayoanza mwezi ujao

Tuesday, July 20, 2010

SHIRIKA LISILO LA KISEREKALI LA HABESA LAWEKA TAWI TANZANIA


Baadhi ya wadau wa HABESHA wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari

Mkurugenzi wa mipango wa shirika lisilo la kiserekali la Habesha Marekani, Ras Kofi Kwayana (kushoto) akibadilishana hati za mkataba na Mwenyekiti wa shilika hilo Nchini, Sam Odera Dar es salaam jana kwa ajili ya kuinuwa vipaji vya vijana wasio na uwezo kwenda kujifunza tamaduni za wamarekani weusi.

KUNA NINI KINAKUJA HAPA SUBILI PUNDE


NINI KINAKUJA
Baadhi ya wapita njia wakishangaa mnara uliokuwa umepambwa katika barabara ya Ali hasani mwinyi Dar es salaam jana ambapo umepabwa na maneno ya kuwa kuna kitu maalumu kinakuja baada ya siku tatu

ALLY ZAWADI WA IFM KUWANIA UDIWANI KWA TIKETI YA CCM



Ndugu Ally Zawadi {kulia} ambaye ni mhadhiri(Lecturer) wa chuo cha usimamizi wa fedha {IFM} akichukua fumu ya kuwania kiti cha udiwani kata ya Magomeni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo mchana.

Ngugu Ally Zawadi akisaini kitabu maalumu mara baada ya kukabidhiwa fomu katika ofisi za CCM kata ya Magomeni mapema mchana wa leo.{Picha:Victor Makinda}

Monday, July 19, 2010

ZAIN YATOA MSAADA KWA shule ya sekondari ya st.joseph


Mkuu wa shule ya Sekondari ya St. Joseph ya jijini DSM, SR. Edwardina Frederick (kati), akipokea msaada wa kompyuta kutoka kampuni ya simu ya Zain. Wanaokabidhi msaada huo ni mameneja wa Teknohama wa Zain, Asupya Nalingigwa (Kushoto) na Godfrey Masanja (kulia). Jumla ya kompyuta 4 zenye thamani ya Shilingi Milioni sita zimetolewa mwishoni mwa wiki kwa shule hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya St. Joseph iliyopo Salasala jijini DSM wakifurahia moja ya kompyuta kati ya nne zilizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Zain kwa shule hiyo. Kulia ni meneja wa Teknohama wa Zain Asupya Nalingigwa. Jumla ya kompyuta 4 zenye thamani ya Shilingi Milioni sita zimetolewa mwishoni mwa wiki kwa shule hiyo.

MISS HIGHER LEARNING 2010 KUPATIKANA 22 JULY


Baadhi ya washiriki wakiwa katika picha ya pamoja
Agatha Killala
miaka,20
elimu,diploma
anaishi,dar
anapenda,kuwa mwamasiasa
chakula ndizi nyama

Pendo Sam
miaka,21
elimu,shhada ya kodi
anaishi,posta
anapenda,kuogelea
chakula,samaki

Judith Osima
miaka,22
elimu,shahada ya bank finance
anaishi,posta
anapens,kusafiri

agath killala
miaka,21
elimu,cheti cha utawala
anaishi,dar
chakula,pilau
home/majira/Desktop/miss/agath killala.JPG
Baadhi ya warembo wanaowania taji la miss higher learning 2010 wakiwa katika picha ya pamoja

Lloyd Nchunga HAWA MWENYEKITI MPYA WA YANGA


wanachama wa yanga wakiwa katika uchaguzi jana

Mwenyekiti mpya wa Yanga Lloyd Nchunga akimwaga sera kabla ya kuchaguliwa na mkutano mkuu uliofanyika jana

RASHIDI MATUMLA ASTAFU NGUMI BAADA YA KUPIGWA NA MADA MAUGO JANA


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, jana aliibuka mshindi baada ya kumchapa mpinzani wake Rashid Matumla katika pambano lisilo la ubingwa la raundi kumi lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA, jijini Dar es salaam.

Katika pambano hilo la uzito wa Middle, lilikuwa na upinzani mkali ambapo Maugo alitumia nafasi alizokuwa akizipata kwa kumchapa makonde mpinzani wake katika raundi 10 walizocheza.

Baada ya pambano hilo kumalizika mwamuzi wa mchezo Ally Bakari 'Champion' alimtangaza Maugo kuwa mshindi baada ya kushinda kwa pointi 100-95, 98-98 na 96-98.

Akizungumza baada ya pambano hilo, Maugo amesema kuwa ametimiza ahadi yake aliyowaahidi mashabiki wake ambapo kwa sasa anajifua kwa ajili ya kuzichapa na Fransis Cheka.

“Nimetimiza ahadi yangu niliyowaahidi mashabiki wangu hivyo kwa sasa najipanga upya kwa ajili ya kupigana na Cheka” alisema maugo.

Naye Matumla amesema kuwa amekubali matokeo katika pambano hilo hivyo kwa sasa anastaafu ngumi na kuamua kuwa kocha wa vijana ili aweze kuibua vipaji na kukuza mchezo huo.

“Nimekubali matokeo ya pambano langu na Maugo hivyo kwa sasa naachana na ngumi na ninatarajia kuwa kocha kwa ajili ya kuibua vipaji kwa vijana” alisema Matumla.

Katika mapambano ya utangulizi ya raundi nne nne, bondia Joseph Richard wa Ashanti boxingi ya Ilala Dar es salaam alimchapa Kijepa Omary kwa KO katika raundi ya pili katika pambano la uzito wa Super Fly, Mwalimu Mussa alimchapa kwa pointi mpinzani wake Masoud Mohamed katika pambano la uzito wa Super Bantam.

Mapambano mengime yalikuwa sare ambapo bondia Abdalah Mohamed alizichapa na Said Zungu katika pambano la uzito wa Light, Juma Seleman alizichapa na Iddy Mgodomi katika pambano la uzito wa Fly na Fadhil Majia alizipiga na Sadiq Abdulazizi katika pambano la uzito wa Fly.



Mabondia Rashidi Matumla (kuliaa) na Mada Maugo wakichuana katika mpambano wao uliofanyika katika katika ukumbi wa PTA Dar es salaam jana Maugo alishinda kwa pointi na kumfanya matumla kutangaza kustafu ngumi matumla atangaza kuwa kocha
mashabiki wa ngumi walikuwepo kushughudia

Mabondia Josephe Richard wa AShanti (kushoto) na Kijepa OMari wakichuna katika pambano la utangulizi Richard arishinda kwa KO, ya raundi ya pili
Mabondia mada Maugo na RAshidi Matumla wakichuana
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...