Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 28, 2011

MAMA SALMA KIKWETE ACHANGISHA FEDHA KWAAJILI YA TAMASHA LA (MOWE)


Mwenyekiti wa Taasisi wa WAMA pia Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Wajasiriamali Aug 26,2011 jinini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) 2011 litalofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mwaka huu Taasisi ya WAMA ndio mratibu wa Tamasha hilo.Jumla ya zaidi milioni 55 zimechangwa katika hafla hiyo na kauli mbiu ya mwka huu ya MOWE ( MIAKA 50 WANAWAKE WAJASIRIAMALI TUNAWEZA-TUTUMIE FURSA),(kulia ni Mwenyekiti wa MOWE Tanzania Elihaika Mrema,na (kushoto) ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Consolata I. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea vitabu kutoka kwa muwakililishi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania Gloria Kavishe(kulia) katika hafla ya Uzinduzi wa uchangiaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la Wajasiriamali (MOWE) August 26,2011, Vitabu hivyo vimekabidhiwa kwaajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule ya mfano ya watoto yatima WAMANAKAYAMA iliopo Rufiji mkoa wa Pwani, (Picha na Mwankombo Jmaa-MAELEZO)
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akipokea hundi ya shilingi milioni tano (5m/-) kutoka kwa Mwakilishi wa Bank ya CRDB (kulia)kwaajili ya kuchangia tamasha la wajasiriamali wanawake (MOWE) 2011 , (aug 26,2011)) jijini Dar es Salaam, Zaidi ya shiligi 55 milioni zimechangwa.(55,368,500/)
Picha na Mwankombo Juma-MAELEZO).
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya MOWE na vbaadhi ya viongozi wa meza kuu akiwepo Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete.(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Baadhi ya Wanawake wajasiriamali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Slama Kikwete (Aug 26,2011) katika hafla ya uzinduzi wa uchangishaji wa fedha kwaajili ya Tamasha la wajasiriamali (MOWE) jijini Dar es Salaam (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...