Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, May 1, 2012

BINGWA WA IBF AFRIKA

Jumamosi ya tarehe 28 mwezi huu, Mtanzania Francis Cheka alinyakua ubingwa wa "IBF Continental Africa" (ubingwa wa Africa wa IBF) katika uzito wa Super Middleweight. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa PTA hapa Dar-Es-Salaam. Bingwa Francis Cheka anatakiwa kutetea ubingwa huu katika kipindi kisichozidi miezi sita (6)!

Mpambano huu ulikuwa wa raundi 12 na kila raundi ilikuwa ni dakika tatu (3). Promota wa Mpambano huu alikuwa Lucas Rutainurwa wa Kitwe General Traders Limited ya Dar-Es-Salaam, Tanzania. Refarii alikuwa ni Bw.John Shipanuka toka Zambia. Majaji; Bw. William Sekelete (Zambia), Bw. Simon Katogole (Uganda) and Bw. Ismail Sekisambu (Uganda).

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) litapenda kuchukua fursa hii kumpongeza bingwa Francis Cheka kwa kunyakua ubingwa wa Afrika.

Aidha tunamtakia bondia Francis Cheka maisha mazuri kama bingwa na tunamuasa aishi kama bingwa kwa kuonyesha nidhamu na uaminifu kama ubingwa wenyewe unavyotakiwa kwani bingwa ni kioo cha jamii.

Tupenda kuchukua fursa hii pia kushukuru sana vyombo vya habari pamoja na waandishi mmoja mmoja kwa kazi nzuri sana waliyofanya wakati wote wa maandalizi na siku ya pambano hili lilipofanyika. Kwa kweli vyombo vya habari vimejenga hamasa kwa wapenzi wa mchazo wa ngumi hapa Tanzania na Afrika nzima kwa jinsi walivyokuwa wana ripoti kwa hamasa kubwa.

Wakati tukiwa kwenye somo hili la uandishi, viko vyombo vya habari na waandishi ambao waliripoti kuwa huu ulikuwa ubingwa wa "IBF Intercontinental", "IBF East Africa", "ubingwa wa IBF" n.k!
Tunapenda kutoa taarifa sahihi kwa wapenzi wa ngumi kuwa hili lilikuwa pambano la ubingwa wa Afrika (IBF Continental Africa Title) na sio mabara (IBF Intercontinental Title) au sio ubingwa wa IBF wa Afrika Mashariki (IBF East Africa)" au "ubingwa wa IBF wa dunia" (IBF Title).

Ni vizuri tuwe tunatafuta taarifa au tafsiri sahihi kutoka kwenye vyombo husika ili tusiikanganye jamii. Kwa hili pambano chombo husika ni IBF.
Tutapenda tena kurudia kwa kutoa shukrani zetu kwa vyombo vya habari pamoja na waandishi mmoja mmoja kwa kazi nzuri mlivofanya.

Mwisho, tunapenda kurudia tena kumpongeza bingwa mpya wa "IBF Continental Africa" Francis Ckeka kwa kunyakua ubingwa wa Afrika na tunamtakia maisha mema na maandalizi mazuri ya kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...