Warembo wa Tabata wakiwa wamepozi
Na Mwandishi Wetu
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2012, litafanyika Juni 1 katika ukumbi wa Da West Park, Tabata.
Mratibu
wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho hilo pia kutakuwa
na sherehe kabambe ya kusherehekea miaka 10 ya Miss Tabata.
“Shindano
la mwaka huu litakuwa ni la aina yake kwa sasabu hii itakuwa ni mwaka
wetu wa 10 kuanda Miss Tabata. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje
na ndani ya nchi. Pia tutahakikisha tunashirikisha warembo bomba wenye
hadhi ya kushinda taji la Miss World,” Kapinga alisema mratibu huyo wa
Bob Entertainment na Keen Arts.
Kapinga alisema kuwa warembo
waliyowahi kushinda mataji tofauti tofauti la shindano hilo pia
watakuepo kusherekea miaka 10 ya Miss Tabata.
Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Dar West Park.
Warembo
hao ni Neema Saleh (18), Noella Michael (19), Queen Issa (20),
Hycalisa Joseph (18), Phillios Lemi (19), Wikllihemina Mvungi (20) na
Nightness Rajab (19). Wengine ni Suzanne Pancras (19), Caroline David
(21), Khadija Nurdin (19), Jamila Omary (18), Advent Mamkwe (21),
Nadya Marjeby (21), Axer Peter (20), Rahama Hassan (19), Mercy Mlay
(21) na Diana Simon Laizer (20).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.
"Bado
milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo
anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,”
mratibu huyo aliongeza.
Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo
wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano ya Miss Tanzania
ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda nafasi ya tatu kabla ya
kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika shindano la mwaka
juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi hiyo ya
taifa.
Juliet ndiye anayeshikilia taji la dunia la Miss Progressive International
No comments:
Post a Comment