KATIBU Mkuu wa Shiriko la Vyama vya Wafanyakazi nchini
(Tucta), Nicolas Mgaya amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya
uenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Watu wa Muheza (MDTF), akitaka kuvaa viatu
vya mtangulizi wake, Tido Mhando.
Mgaya ameingia katika kinyang'anyiro hicho akiwa ndiyo
mgombea pekee wa nafasi hiyo baada ya Sekretarieti iliyokuwa chini ya uenyekiti
wa Tido, kumaliza muda wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya
habari jijini Dares Salaam na Katibu Mwenezi wa MDTF, Ramadhan Semtawa uchaguzi
huo wa kupata sekretarieti mpya utafanyika kesho kwenye Kanisa la Mtakatifu
Albano, lililopo karibu na kituo cha Posta mpya.
"Chama Cha Maendeleo cha Watu wa Muheza kinapenda
kiwaarifu wana Muheza wote kwamba keshokutwa siku ya Jumamosi, tarehe 12 mwezi
huu kutakuwa na uchaguzi mkuu wa kuchagua sekretarieti mpya ya chama. Hivyo,
wana Muheza wote mnaopenda maendeleo ya wilaya yenu mnaombwa kufika bila
kukosa. Uchaguzi utafanyika kuanzia saa 3:30 asubuhi," alisema
Semtawa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi jana mchana nafasi ya
mwenyekiti ilikuwa ikiwaniwa na Mgaya huku ile ya Makamu ilikuwa ikiwania na
Mwanaidi Ngoda, Katibu Twaha Msenga, Mweka Hazina na Semtawa akiwania tena
nafasi hiyo ya uenezi.
MDTF ni chama kilichosajiliwa kwa madhumuni ya kuleta
maendeleo ya Muheza ambayo huchochea pia maendeleo ya taifa kwa ujumla katika
sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, afya, maji na kilimo. Baadhi ya miradi mikubwa
ya MDTF ni visima vya maji katika sekondari za Kelenge huku pia mfuko huo ukiwa
umejenga Shule ya Kidato cha Sita ya Muheza (Muheza High School).
Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho
ni Edward Mhina akifuatiwa na Hurbet Mtangi ambaye ni mbunge wa
Muheza, Balozi Adadi Rajabu na anayemaliza muda waake ni Tido ambaye aliongoza
Sekretarieti ambayo makamu wake alikuwa ni Merry Chipungahelo, Katibu ni Albert
Semng'indu, mweka hazina Nehemia Mchechu na Katibu Mwenezi, ni Semtawa.
No comments:
Post a Comment