Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal wa nne kutoka kushoto na mama
Tunu Pinda wanne kutoka kulia pamoja na wake wa viongozi mbalimbali
wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya Netiboli Taifa Queen
mara baada ya kukabidhiwa kombe lao la ushindi wa pili katika michuano
ya Afrika ya Netiboli, baada ya Malawi kuchukua ubingwa huo, fainali
hizo zilifanyika jana kwenye uwanja wa Taifa wa ndani na kufuatiwa na
hafla fupi nyumbani kwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
Hata hivyo fainali hizo zilichelewa kuanza kutokana na hali ya hewa
ambapo muda mwingi mvua ilikuwa ikinyesha na kufanya waandaaji kuhamisha
uwanja wa kuchezea mara kwa mara kutoka uwanja mkubwa wa Taifa na
uwanja wa ndani
Crew ya Fullshangwe inamushukuru sana mama Tunu Pinda kwani juhudi zake
zimeonyesha matunda na ni wazi kwamba hata wachezaji wa timu hiyo ya
Taifa Queen wamefurahia sana michuano hii na wanajiona kwamba kweli
walikuwa wakiwakilisha taifa, lakini pia watanzania wakiongozwa na mama
Tunu Pinda pamoja na kamati yake walikuwa nyuma yao, Hongera sana mama
kwa kutoa zawadi nono kwa wachezaji
Mashabiki na wanafunzi mbalimbali wa shule ya Filbert Bayi wakishuhudia mchezo huo.
Kutoka kulia ni Patrick Nyembea wa EATV, Nandi Mwiyombela Meneja Miradi
Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya bia ya Serengeti SBL na Jamal Bayser
wa Superdoll pamojana nwadau wengine wakishuhudia mchezo huo..
Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Kampuni ya bia ya Serengeti SBL
Teddy Mapunda akipozi kwa picha na baadhi ya wake wa viongozi.
No comments:
Post a Comment