MSHAMBULIAJI Mario Balotelli atatumia majina yake yote ya kifamilia katika jezi yake ya Italia kwenye fainali za Euro 2012.
Orodha
rasmi ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), inamtambulisha kinda huyo wa
miaka 21 kwa jina la 'Barwuah Balotelli' katika jezi yake.
Balotelli
aliazaliwa mjini Sicily kwa jina la Mario Barwuah kwa wazazi wenye asili
ya Ghana. Uafrika wake sasa unajipambanua baada ya Balotelli kusema
kwenye mahojiano kwamba ataondoka uwanjani iwapo atafanyiwa ubaguzi
kwenye Euro 2012.
Alichukua jina Balotelli kutoka wazazi wake wa kufikia mjini Brescia, ambao walimnunua baada ya kuugua sana akiwa mdogo.
Amekuwa akitumia jina la Balotelli (pichani kulia) tu katika kikolsi chake cha Manchester City.
Italia inaanza mechi za kundi lake C dhidi ya Hispania Jumapili mjini Gdansk.
Orodha ya UEFA,
pia imesuluhisha tatizo la majina ya wachezaji watatu wa Denmark
wanaoitwa Poulsen kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa timu hiyo.
Christian
Poulsen sasa atavaa jezi yenye jina 'Chr. Poulsen', Jakob Poulsen atavaa
'J. Poulsen' na Simon Busk Poulsen atavaa 'Busk Poulsen.'
Winga wa England, Alex Oxlade-Chamberlain atatumia jina la 'Chamberlain' tu kwenye jezi yake.
No comments:
Post a Comment