Na Mwandishi Wetu
BARAZA
la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya siku moja kwa majaji
wa shindano la Epic Bongo Star Search 2012 kwa kuwataka kuzingatia
maadili ya kazi zao.
Akitoa somo kwa majaji hao mratibu wa matukio wa Basata Malimi Mashili aliwataka majaji hao kutambua kuwa asilimia kubwa ya washiriki wanategemea zaidi msaada wao katika kukuza vipaji.
Mashili
aliwataka majaji hao kutambua kuwa mazingira waliyotoka washiriki na
kuangalia namna ya kuwasaidia kulingana na mikoa yao kwa kuwa wapo ambao
wana vipaji lakini wanatatizwa na suala la kuyazoea mazingira.
Alisema
kuwa kwa kuwa mwaka huu EBSS itaruhusu washiriki wa miaka 16 hivyo ni
vema zaidi wakazingatia suala la sauti kulingana na umri wa mshiriki
sababu watakuwepo wenye sauti za kitoto pia.
Pia
aliwataka majaji hao kuhakikisha kuwa hawatoi aina yoyote ya upendeleo
na wala kuwa karibu zaidi na baadhi ya washiriki wa shindano hilo.
Pia alisisitiza kuwa majaji wanalo jukumu kubwa la kuwaelekeza namna ya kuimba, kuvaa, kujiheshimu na usafi wa mwili pia.
“Hiii
ni semina ya kuwekana sawa tu kwa kuwa hili shindano lipo kwa muda
mrefu na majaji mmekuwa mkifanya vema, kwa niaba ya BASATA napenda
kuchukua muda huu kuwataka muwe makini katika kuzingatia maadili haya
niliyoyasema na hata mengine pia”alisema Mashili.Naye
Mkurugenzi wa Berchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha
Paulsen alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa majaji kwa kuwa muda mzuri wa kukumbushana mambo muhimu yahusuyo muziki.
Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 16 katika ukumbi wa Royal Village.
Majaji wa shindano hilo waliohudhuria ni pamoja na Jaji Mkuu Ritha Paulsen, Master Jay, Salama pamoja na mratibu wa EBSS kutoka Basata Vicky Temu.
habari zaidi ingia www.elimuboratanzania. blogspot.com
No comments:
Post a Comment