Mchakato wa kuendelea kuitambulisha
huduma ya Airtel Supa5 mikoani utaendelea mwishoni mwa wiki hii ambapo
Airtel itaweka kambi mkoani Mwanza katika viwanja vya wazi vya furahisha
vilivyopo jijini Mwanza.
Akizungumzia
tamasha hilo la kuitambulisha SUPA5 mkoani Mwanza Afisa Uhusiano wa
Airtel Bi Jane Matinde alisema lengo la kuunganisha utambulisho huu
burudani ni kuwavutia vijana na wateja wengi kuhudhuria na kujifunza
faida lukuki za SUPA5 ili waitumie zaidi
Tamasha
linafanyika kwa siku mbili mfululuzizo ambapo siku ya jumamosi tunatoa
fulsa kwa wasanii chipukizi kujitokeza kwa wingi kuonyesha vipaji vyao
sambamba na kupata huduma ya Airtel SUPA5
Jumapili
itakuwa uzinduzi kamili ambapo wasanii wakubwa watatoa burudani BURE,
akiwemo Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi, Mwasiti a.k.a SOJA,
Roma Mkatoliki a.k.a mzee wa tuzo kibao watatoa burudani kali kwa
wateja watakaohuduria tamasha hilo BURE
Bi Matinde pia amezungumzia lengo la huduma ya dili tano bomba zilizopo kwenye huduma ya SUPA5 kuwa Airtel inatimiza dhamira yake iliyojiwekea ya kufikisha na kupunguza gharama za mawasiliano nchini kote bila kuwasahau vijana na wanafunzi kunufaika kwa kupata internet bure wakati wa usiku, kutuma sms bure na faida nyingine nyingi.
Huduma
ya Airtel SUPA5 ilizinduliwa rasmi siku za karibuni jijini Dar es
salaam kisha kufuatiliwa na kufanyika kwa matamsaha ya burudani ya BURE
katika mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Arusha huku mwishoni mwa wiki
hii itakuwa zamu ya wakazi wote wa Mwanza
Wasanii
mahiri waliokwishapamba majukwaa ya Airtel SUPA5 hadi sasa kwa mkoa wa
Dar es salaam ni Fid Q, Mwasiti, Godzilla, pamoja na Kundi la Tip Top
Connection akiwemo Madii, Tundaman,Richard na Dodo Janja kwa mkoa wa
IRINGA ni Juma Nature na kundi zima la wanaume halisi,Roma mkatoliki,
pamoja na Kundi la Tip Top Connection akiwemo Madii, Tundaman na
Richard. Mkoa wa Morogoro na Dodoma ni kundi mahiri la Wanaume family
likiongozwa na Chege na Temba na kukamilisha ladha ya zaidi kwa kuwepo
kwa Bendi Maarufu jijini ya Mashujaa band ikiongozwa na kingunge
Charles Baba na wasanii wengine.
No comments:
Post a Comment