Mbunge wa Jimbo la Segerea, Dk. Makongoro Mahanga (kulia), Meya wa
Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto) na Mwenyeji wa harambee ya
kuchangia mpango wa elimu wa Kata ya Kipawa, Diwani wa Kata hiyo Bonah
Kaluwa, wakimuongoza Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye alikuwa
mgeni rasmi kuingia ukumbini Katika hafla iliyofanyika jana usiku ndani
ya hoteli ya Kilimanjaro (Kempiski hotel) jijini Dar es Salaam .
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye harambee hiyo
Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akitoa neno la shukurani kabla ya kuanza kwa harambee hiyo.
Mgeni rasmi wa Hharambee hiyo akimpa mkono wa asante mwakilishi wa
kampuni ya Home Shopping Centre Bi Madiha Al Harthy (kushoto),Salma
baada ya kuchangia sh. milioni 22.
Mkurugenzi wa SONGAS Limited Bw;Christopher Ford(katikati),akimkabidhi
mfano wa hundi yenye thamani ya dolla za kimarekani 10,000, mgeni rasmi
wa harambee hiyo.kushoto meneja
rasilimali Songas Bi Agatha Keenja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja
(katikati) akipongezwa na Mgeni rasmi wa harambe hiyo baada ya
kuchangia sh. 500,000.
eya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kushoto), akimkabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh.milioni 10, Waziri Mkuu wa zamani, Edward
Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia mpango wa
elimu Kata ya Kipawa, iliyofanyika Dar es Salaam juzi. Fedha hizo
zilitolewa na Manispaa hiyo ambapo zaidi ya sh. milioni 400
zilipatikana.
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI Mkuu wa zamani , Edward Lowassa, ameendeleza kuwa mstari wa mbele
katika harakati zake za kuchangisha mamilioni ya fedha baada ya
kuchangisha Sh.421,850,000 kwa ajili ya kuboresha Mfuko wa Elimu Kata ya
Kipawa katika Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Lowassa ambaye ni mbunge wa Monduli (CCM), aliendesha harambee hiyo juzi
katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Kempiski Jijini Dar es Salaam
ambapo yeye mwenyewe alichangia Sh.milioni 10.
Katika harambee hiyo miongoni mwa makampuni yaliyochangia kiasi kikubwa
ni Lion Club Sh.milioni 70, Home Shipping Center Sh.milioni 22, African
Barrick Gold Dola 10,000, Songas Dola 10,000, Maersk Sea Line
ilichangia Sh.Miliono 90, na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
alichangia milioni Sh.10.
Wengine waliochangia ni madiwani, viongozi wa Chama Cha Mapinduzi,
Chadema, taasisi za watu binafsi na mtu mmoja mmoja ambapo Radio Clauds
walitoa muda wa hewani wa kutangaza mpango huo wenye thamani ya sh.
milioni 12.
Akizungumza kabla ya kuendesha harambee ya kuchangisha, aliwataka
Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuendelea kuwahamasisha
wananchi kuwekeza katika kuchangia sekta ya elimu.
Lowassa alimpongea Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwa jitihada
zake alizozionyesha za kuchangia elimu na kuwataka madiwani wengine
kuiga mfano huo.
Diwani wa Kata ya Kipawa, Bonnah Kaluwa, kwaupande wake alisema shule
saba za Msingi na Sekondari zilizopo kata hiyo zinakabiliwa na matatizo
lukuki ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa hali inayosababisha
wanafunzi kati ya 140 hadi 160 kusomea katika darasa moja.
“Shule za kata yangu kwa kweli zinakabiliwa na changamoto nyingi,
kwa mfano Shule ya Msingi ya Majani ya Chai ina vyumba vya madarasa nane
wakati wanafunzi waliopo ni 2,200, Shule ya Msingi ya Minazi Mirefu
madarasa yake yaliyopo ni machakavu pia hayatoshelezi,”alisema Kaluwa.
Kaluwa alisema jitihada nyingine zilizofanywa katika kutafuta pesa kwa
ajili ya kuziboresha shule hizo ambapo Machi 17 mwaka huu kuliitishwa
matembezi ya hisani yaliyoongozwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Aliongeza kuwa katika hafla hiyo kiasi cha shilingi milioni 15 kilichangwa na wadau
mbalimbali ambapo kati ya hizo Sh.Milioni 3 zilitolewa na Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete na Clouds Media Group ambao walitoa shilingi milioni
moja na wanafunzi kadhaa wa shule za msingi na sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Segerea Dk.Makongoro Mahanga aliwashukuru wadau
waliojitokeza kuchangia kata hiyo ambayo ipo katika jimbo lake na
kuwataka wadau wengeni kuchangia kata zingine ili kukabiliana na
matatizo hayo katika shule mbalimbali.
No comments:
Post a Comment