Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, leo imezindua rasmi somo la Polisi litakalojulikana kama Usalama wetu kwanza kuwa moja ya masomo yatakayofundishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi visiwani humo.
Akizungua
mpango huo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar Mh. Ali
Juma Shamhuna, amesema kuwa somo hilo litaanza kufundishwa kwa majaribio
katika shule kumi za msingi kisiwani Unguja na hivyo kulifanya somo
hilo kuwa sehemu ya masomo yaliyopo katika mitaala ya shule za msingi
Visiwani hapa.
Mh.
Shamhuna amesema kuingizwa kwa somo hilo katika mitaala ya shule za
msingi, kutasaidia kujenga uwezo na uwelewa wa kujitambua na katika
kuwabaini wahalifu mbalimbali wakiwemo maadui wa taifa letu.
Mh.
Shamhuna ambaye alikuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa mpango huo,
amekagua vitabu vitakavyotumika katika kufundishia somo hilo ambavyo
vimeandaliwa na Jeshi la Polisi hapa nchini kwa ajili hiyo.
Awali
katika Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Visiwani hapa Bi.
Mwanaidi Salehe Abdallah, alisema kuwa somo la Usalama wetu kwanza
litakuwa kama somo linguine na litatungia mitihani ya kujipima na ule wa
Taifa.
Somo
la Usalama wetu kwanzxa ni somo lililobuniwa na Jeshi la Polisi hapa
nchini ili kuwawezesha wananfunzi wa shule za msingi na sekondari
kujenga uwelewa katika matumizi salama ya usalama barabara kwa lengo la
kuepuka ajali za mara kwa mara.
Naye
Mwakilishi wa Kamishna wa Polisi zanzibar ACP Mohammed Ali Mweri,
amesema kuwa somo la Usalama wetu kwamza limeanzishwa na jeshi la Polisi
na ni moja ya Miradi ya Polisi Jamii inayomjenga mtoto katika
kuwatambua watu wabaya na jinsi ya kuwaepuka na hata kuwatolea taarifa
katika vituo vuya Polisi.
Wakati huo huo,
Mh. Shamhuna amekemea vikali baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu
kutaka kuhatarisha usalama wa Taifa letu kwa kudai kura ya maoni juu ya
Muungano kabla ya shughuli za ukusanyaji wa maoni ya Katiba mpya Jamhuri
kukamili.
Amesema
watu hao ni hatari kwa Taifa letu na kwamba Serikali haiwezi kukaa
kimya kuona amani inavurugika kutokana na kikundi cha watu wachache kwa
imani za itikadi ya kidini.
Amesema
tangu kukusanywa kwa maoni yaliyoandika Katiba mpya ya Zanzibar yenye
sura ya Umoja wa Kitaifa, hivi sasa Zanzibar vimekuwa tulivu na eneo la
mfano kwa nchi za Kiafrika zenye utulivu.
No comments:
Post a Comment