Mayweather, akisindikizwa na Mwanasheria wake, Karen Winckler (katikati) na rafiki yake 50 Cent , wakati akiingia katika Mahakama ya Las Vegas kusomewa hukumu ya kesi yake.
Mayweather akifungwa pingu tayari kuelekea katika gereza la Clark County, Detention Center Nevada.
Sare na Yeboyebo atakazotumia Mayweather kipindi atakachokuwa gerezani.
*********************************************
KUTOKA LAS VEGAS, Marekani
NI
saa 72 zimepita sasa, kati ya saa 2160 ambazo mkali wa masumbwi duniani
Floyd Mayweather Jr baada ya kuhukumiwa kutumikia kifungo chake jela.
Mkali huyo wa masumbi amelimwa hukumu hiyo ya kutumikia kifungo kutokana na vitendo vya unyanyasaji majumbani aliofanya miaka miwili iliyopita.
Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa Mayweather, alimfuata mpenzi wake wa zamani, Josie Harris, hadi
nyumbani, na kumtandika makofi, kabla ya kushtakiwa na kukutwa na
hatia iliyomtia hatiani na kuhukumiwa kifungo hicho kwenye gereza la Clark County Detention Center Nevada.
Akisomewa mashtaka hayo, Bondia
huyo alikiri kumkunja mkono mpenzi wake, Harris, mama wa watoto wake
watatu, ambapo alikilri kosa lake na kuwa alitenda hivyo baada ya
ushauri wa kisheria, ambapo kama angeendelea
kubisha na baadaye kukutwa na hatia, angeweza hata kufungwa miaka 34
jela – jambo ambalo wanasheria wake walimuhadharisha mapema.
50 Cent azungumzia kifungo cha rafiki yake
Wakati
alipofika mahakamani na kisha kumaliza taratibu za kimahakama tayari
kwenda jela, Mayweather alikuwa mpole akilengwa na machozi, kitu
kilichomfanya ashindwe kuongea chochote, haikuwa hivyo kwa swahiba wake
50 Cent.
"Ni
hali ya simanzi kwa kila mmoja akiwamo yeye mwenyewe, lakini naamini
atakuwa sawa tu," aliongeza 50 Cent akionekana kuelemewa na sikitikoto.
"Kila mmoja ana tafsiri tofauti katika stori ile ile," aliongeza 50 Cent, ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson III.
"Yeye ukilinganisha mgogo kati ya Mayweather na Harris uliochangia kuvunjika kwa ndoa yao ambapo watoto wao watatu walihusika. Harris na watoto wake wanaishi huko Kusini mwa California.
"Hakuna
tofauti kwa kila mmoja kuelekea mchakato wa talaka kwa umpendaye,"
alisema rapa nyota huyo na kuongeza: "Na namna rafiki yako anavyoweza
kugeuka kuwa adui yako mkubwa."
Ni
siku ya nne sasa, kati ya siku 90 za kuishi maisha ya kifungo, ambapo
atakapotoka jela atalazimika kufanya shughuli za kijamii zitakazomfanya
atumie kiasi Fulani cha pesa.
Anasubiriwa kwa hamu na mashabiki hapo Agosti 30, 2012 kuona kama atakuwa amebadilika kiakili, kimwili na kiroho kama alivyoahidi.http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment