Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 4, 2012

KWANINI WAZANZIBARI WANALALAMIKIA ZAIDI MUUNGANO KULIKO BARA?


Hiizi ni kumbukumbu ambazo wazanzibari wakiziona huwafanya watokwe na machozi na kusema wamerudishwa nyuma kwa zaidi ya asilimia miamoja, thamani ya pesa hii kwa sasa ni karibu 22,500 kwasababu rupia moja ni zaidi ya T sh4000.

Bila shaka kuna sababu nyingi zinazowafanya wazanzibari kulalamikia muungano, moja wapo ni kuwa na spidi ndogo ya maendeleo pamoja na udogo wa Visiwa vyake ikilinganishwa na kasi ya maendeleo ya bara panoja na ukubwa wake.

Kupotea kwa haiba na hali nzuri ya kimaisha iliyokuwepo hapo mwanzo kwa wakazi wake na kurudi nyuma kabisa kwa mfumo wao wa maisha waliouzoea likiwepo suala la kipato kwani kwa khadithi za wakati ulee wanazo khadithiwa vizazi vya sasa mambo yalikuwa safi yani kwa maneno ya sasa tunasema mambo yalikuwa 'MSWANO'

Yapo mambo mengi lakini tutadadavua kidogokidogo hadi tutaelewa kwanini Wazanzibari wapo kama wanavyoonekana.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...