Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 2, 2015

WASHINDI WA TIGO KILI HALF MARATHON WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

TI1
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 2, mshindi wa kwanza wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon Ismail Juma baada ya kushinda katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mkoani Moshi, katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Riadha Mkoa wa Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI2Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kulia) akifurahia jambo na Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano wakati wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI3Washindi wa kwanza mpaka wa tatu wa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, kwa upande wa wanaume, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Leonidaz Gama (kushoto), kulia ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage pamoja na na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.
TI4Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili kushoto) akisoma risala katika mashindano ya fainali ya mashindano ya Tigo Kili Half Marathon, iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa kwanza kushoto ni Ofisa Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama pamoja na Makamu Mwenyekiti wa RT William Kalage na Mwenyekiti wa KAA Liston Metacha.
TI5Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Tigo Diego Gutierez (kushoto) akizungumza na Kaimu wake Cecile Tiano (katikati) pamoja Mkurugenzi wa Kanda ya Kaskazini David Charles kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yaliyofanyika juzi Mkoani Moshi.
TI01Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano (wa pili) kushoto, akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo kabla ya kuanza kwa mashindano ya Tigo Kili Half Marathon iliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi.
TI02Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI03Washindi wa mashindano ya Tigo Kili Marathon, kwa upande wa Wanawake, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
TI04Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 mshindi wa tatu Vicoty Chepkemei, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI05Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh. Milioni 1 mshindi wa pili wa mashindano Tigo Kili Half Marathon, Eunice Echumba, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Tanzania (RT) William Kalage.
TI06 
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidaz Gama (kushoto), akimkabidhi hundi ya sh.500,000 mshindi wa tatu Theophil Joseph, baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Tigo Kili Half Marathon kwa upande wa Wanaume, katika mashindano hayo yaliyofanyika juzi kwenye Uwanja wa Chuo Cha Ushirika Mjini Moshi, wa pili katikati ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo Cecile Tiano, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Riadha Kilimanjaro (KAA) Liston Metacha.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...