
Hatimaye lile tukio la utolewaji wa Tuzo za chama cha waandishi wa habari za michezoTanzania (TASWA) ambazo hutolewa kila mwaka kwa wanamichezo wanaofanya vizuri, zimekamilika usiku wa October 12 kwa wanamichezo, taasisi na viongozi waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka 10, Tuzo hizo safari hii zimekuwa tofauti na miaka yote kwani waliopewa Tuzo ni wale waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi.
Tuzo hizo ambazo zilikuwa maalumu mwaka huu, kwani zimetumika kumuaga RaisKikwete kwa kumaliza muda wake madarakani na kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo nchini katika kipindi cha utawala wake. Ikumbukwe kuwa Tuzo hizo ziligawanyika katika vipengele vinne, Taasisi iliyochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5.
Tuzo zimetolewa kwa wanamichezo waliofanya vizuri katika kipindi cha miaka kumi, viongozi waliochangia kuinua michezo katika kipindi cha miaka kumi Tuzo 5 na Tuzo ya heshima kwa Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuheshimu mchango wake katika kuinua michezo wakati wa utawala wake, baadhi ya waliopewa Tuzo usiku wa October 12 ni Francis Cheka, Mbwana Samatta, Iddi Kipingu, Abdallah Majura na Hashim Thabiti

Kanali Iddi Kipingu akipokea Tuzo yake ya heshima kwa kusaidia kuinua michezo kwa muda mrefu toka yupo shule ya Makongo

Abdallah Majura akikabidhiwa Tuzo ya heshima katika kuinua michezo sasa kafungua kituo cha Radio kinachojihusisha na michezo.

Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto akimkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya heshima akiwa pamoja na mkuu wa mkoa Dar Es Salaam Meki Sadiki, waziri wa michezo Dk Fenella Mukangara na Dioniz Malinzi.

Nahodha wa Taifa Stars Nadir Haroub akikabidhi jezi ya Taifa Stars kwa Rais Kikwete ikiwa imesainiwa na wachezaji wote.
No comments:
Post a Comment