Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 25, 2016

WAKAZI WA KATA YA NAMAYUNI WAPONGEZA MTANDAO WA SIMU ZA MKONONI WA HALOTEL.


Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Halotel ndio mtandao pekee unaotoa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu za mkononi katika kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi.

Mtandao huu ndio unawasaidia wakazi wa kata ya Namayuni kuweza kuwasiliana na ndugu na jamaa  wa maeneo hayo na sehemu nyingine kwa njia ya simu ya mkononi kwa kuwa wamejengewa mnara unao wawezesha kuwasiliana kwa njia simu za mkononi.

 Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura amepongeza mtandao wa simu za mkononi wa Halotel na kusema kuwa umeisaidia sana jamii ya wakazi wa kata ya Namayuni mkoani humo kutokana na hapo awali kutokuwepo na mtandao wowote wa simu.

" Tunawashukuru sana Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kukumbuka kama kunaviumbe huku na kutuwekea mnara katika kata yetu kwakua kabla ya mtandao huu tulisafiri na kupanda juu ya vilima ili kutafuta mtandao(network) ili tuweze kuwasiliana na watu wengine kwa njia ya simu."

Nao wakazi wa Kijiji cha Namayuni wamesema kuwa Mtandao huu wa Halotel "umetusaidi sana katika huduma mbalimbali hasa kutufichia siri katika mawasiliano kwani tulikuwa tunaenda umbali mrefu kwenda kutafuta mtandao, kwa sasa tunakaa ndani tuu na tunawasiliana na ndugu na jamaa  bila mtu yoyote kujua kama tumewasilana na nani".

Wafanyakazi wa mtandao wa Halotel wametembelea kata  ya Namayuni kwaajili ya Kampeni ya HALO MAISHA inayoendelea katika maeneo mbalimbali  yaliyofikiwa na mtandao huo nchi zima ili kila jamii ifaidike na spidi kubwa ya intaneti na upatikanaji wa huduma nzuri za mtandao huo.
 Wanafunzi wakisoma kupitia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti ya spidi kubwa walizopewa  na kampuni ya Simu za mkononi ya Halotel katika shule ya sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani.
Mtaalamu wa masuala ya mtandao  wa kampuni ya Halotel, Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Sebastian Inocent akifafanua changamoto mbalimbali zinazo wapata wakazi wa kijiji cha Namayuni.

Afisa habari wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Halotel, Frank Mwakyoma akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namayuni kilichopo kata ya Namayuni Kilwa Masoko Mkoani lindi mara baada ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kuwatembelea katika kijijini hapo.
 Wakazi wa Kijiji cha Namayuni wakipata maelekezo walipo tembelea kibanda cha kusajili laini jijini  hapo.

 Vijana wakipiga simu kwa ndugu na jamaa wakiwa kijijini hapo.

Baadhi ya waandishi wa habari.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata mkoani Pwani, Abdala Sakasa akizungumza wakati wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel walipotembea katika shule hiyo kujionea jinsi wanafunzi wanavyotumia Kompyuta zilizounganishwa na intaneti yenye spidi ya kazi ili kusaidia wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba hasa wa kidato cha tano na cha sita kwa kusoma na kuongeza uwezo wao katika masoma kutokana na  wanafunzi hao kukosa baadhi ya vitabu. Wanafunzi wa shule hiyo wamefurahia uwepo wa mtandao wa Halotel kwani ndio mtandao pekee uliochelewa kufika hapa nchini na kuweza kutoa kompyuta 19 zilizounganishwa na intaneti katika shule hiyo.
Mwalimu wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi akifafanua jambo mbele ya wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Halotel walipotembelea shuleni hapo mkoani Pwani. Mwalimu wa  Kulia ni Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya  Lugoba, Benjamini Nyamatwema.

Mhizi amesema kuwa wanachangamoto kubwa katika kupanga zamu za wanafunzi wa shule hiyo kwani shule hiyo inawanafunzi 1391 na kompyuta zenye intaneti ni  19 tuu, kwa mujibu wa ratiba ya wanafunzi kuingia kwenye chumba hicho wanaingia wanafunzi 30 kwa kila kipindi ili kila mwanafunzi aweze kuingia katika chumba cha kompyuta.
Wanafunzi wakiwa katika Darasa la kompyuta ambalo Kampuni ya Halotel walijitolea kwa kuwapa kompyuta hizo pamoja na kuwaunganishia Intaneti  spidi kubwa ya bure kwa miaka mitatu mfurulizo iki kuweza kuwasaidia wanafunzi hao katika kujisomea machapisho mbalimbali yaliyopo kwenye mitandao mbalimbali.
Mwalimu wa somo la Kompyuta na maswala ya mawasiliano(ICT), Emmanuel Mhizi akiwakagua wanafunzi kwa uangalifu katika darasa hilo. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lugoba akiendelea kujisomea somo alilolifungua  walipotembelewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel mkoani humo.
 Walimu wa Shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata- Bagamoyo Mkoani Pwani wakijadiliana jambo wakati wanatembea.
 Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wakazi wa kijiji cha Namayuni mkoani humo walipotembelewa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Halotel ambayo ndio mtandao pekee uliowafikia wananchi na wakazi wa kata hiyo. 
Wakazi wa kata ya Namayuni na wanakijiji cha Namanyuni wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Namayuni iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi, Hussein Sungura mara baada ya kutemelewa na wafanyakazi wa kampuni ya Simu za Mkononi yz Halotel mkoani humo.

Mkazi wa Kijiji cha Namayuni akizungumza na simu wakati amekaa akitumia mtandao wa simu wa Halotel akiwasiliana na mtu aliyepo Zanzibar bila kwenda kupanda kwenye kilima kama zamani.
Aidha mzee huyo alielezea furaha yake kwa ujio wa mtandao wa Halotel unavyowasaidia na kuwafichia siri zao, kwani mwanzoni kila mtu alijua kuwa ndio anaenda kuongea na simu na mpaka kusababisha kuaga na kwenda umbali furani kwaajili ya kutafuta netiweki ili aweze kuzungumza na mtu ambaye anamtafuta.
 Mwenyekiti wa Kijini cha Namayuni, Ally Mtumbwe akizungumza na waandishi wa habari Kilwa Masoko Mkoani Lindi kata ya ya Namayuni kijijini cha namayuni mara baada ya wafanyakazi wa mtandao wa Halotel kutembelea kijijini hapo. 
 Mkazi wa Kijiji cha Namayuni akielezea jinsi mtandao huo ulivyorahisisha biashara kutokana na kujengewa mtandao wa Halotel amesema kuwa mtandao huo umewasaidia kwa kuagiza bidhaa anazozihitaji ukitofautisha na zamani ambapo ilibidi kuzifuata hata kama hajui kama bidhaa anayoitaka ipo au haipo, hata hivyo amesema kuwa Halotel imewasaidia kuokoa muda sana.
 Mkazi wa kijiji cha Namayuni akiuliza swali kuhusiana na mtandao huo kuhusiana na kama unaweza kutuma pesa  au kupokea pesa.
Watoto wa Kijijini cha Namayuni wakipata picha na mwandishi wa gazeti la The Citizen kijijini hapo.
 Afisa masoko wa kampuni ya Halotel , Charle anayepiga picha kwa simu akiwa na baadhi ya waandishi wa habari katika kijini cha Namayuni, Klwa Masoko mkoani Lindi.


Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...