Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult,
Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya
siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha
hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika
warsha hiyo.
Miriam Mnada (kulia), akichangia mada
Vijana wasomi wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Vijana wakisikiliza mada kwa makini
Na Dotto Mwaibale
VIJANA wasomi wametakiwa
kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe wabunifu katika
masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa kiuchumi.
Mwito huo umetoewa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna Kamaleki Dar es
Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo vijana
iliyoandaliwa na taasisi hiyo.
"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.
Kamaleki aliwataka
vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza kufanya kitu
chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.
Akizungumzia taasisi
yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii na
ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto.
"Tuna amani kwamba haki
za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa watoto, pia watoto
wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu na sheria
zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema Kamaleki.
Alisema taasisi hiyo
inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo watoto, watu
binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria
na mikataba ya kisheria.
Aliongeza kuwa shughuli
zingine zinazofanywa na taasisi hiyo ni kushauri namna ya kufungua kesi
katika masuala ya jinai, madai, ndoa, ardhi na usimamizi wa mirathi
pamoja na kuwawakilisha wateja wao mahakamani katika shauri lolote la
kisheria.
Alitaja kazi nyingine ya
taasisi hiyo kuwa ni kuwasaidia watu binafsi kuunda na kusajili kampuni
au taasisi na kujenga uwezo wa taasisi au watu binafsi kuhusu sheria
mbalimbali za nchi na kimataifa na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu
masuala ya kisheria.
Kwa mawasiliano na
taasisi hiyo wasiliana nao kwa facebook lecriconsult, twitter
lecriconsult na instrag ni lecriconsult1601 na simu namba 0767855174 na
0657023585.
No comments:
Post a Comment