Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BONDIA Mtanzania, Ibrahim ‘King Class’ Mgender usiku wa jana ametwaa taji la GBC uzito wa Light, baada ya kumpiga Jose Luis Forero Atencio wa Panama kwa pointi ukumbi wa Muggelspreehalle, Hangelsberg, Brandenburg Jijini Berlin, Ujerumani.
Hilo linakuwa pambano la sita kwa Forero anayekwenda kwa jina la utani El Tigre kupoteza katika historia yake ya ngumi, akiwa amepigana jumla ya mapambano 20 hadi sasa, akishinda 13, mawili kwa Knockout (KO) na kutoa sare moja.
Kwa Ibrahim Class mwenye umri wa miaka 26, jana ameshinda pambano la 18 kati ya 22 aliyocheza, moja tu ameshinda kwa KO, huku akiwa amepoteza mara nne.
“Lilikuwa pambano la kukata na shoka, hakika haikuwa kazi rahisi kwangu kuibuka mshindi kwenye pambano hilo, kwani mpinzani wangu Jose Ferero kutoka nchini Panama, alionyesha upinzani mkubwa kwa raundi zote 12 kabla ya mimi kuibuka mshindi kwa pointi na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Light,”amesema Ibrahim Class.
Ushindi wa Ibrahim Class unakuja wiki moja, baada ya bondia mwingine Mtanzania, Francis Cheka kupoteza pambano kwa pointi mbele ya Enes Zecirevic ukumbi wa Salle de Fetes, Le Lignon, nchini Uswisi.
BONDIA Mtanzania, Ibrahim ‘King Class’ Mgender usiku wa jana ametwaa taji la GBC uzito wa Light, baada ya kumpiga Jose Luis Forero Atencio wa Panama kwa pointi ukumbi wa Muggelspreehalle, Hangelsberg, Brandenburg Jijini Berlin, Ujerumani.
Hilo linakuwa pambano la sita kwa Forero anayekwenda kwa jina la utani El Tigre kupoteza katika historia yake ya ngumi, akiwa amepigana jumla ya mapambano 20 hadi sasa, akishinda 13, mawili kwa Knockout (KO) na kutoa sare moja.
Ibrahim Class (kulia) akiinuliwa mkono baada ya kushinda pambano lake hilo na kutwaa mkanda wa GBC uzito wa Light nchini Ujerumani |
Ibrahim King Class (kulia) ametwaa mkabda wa GBO usiku wa jana nchini Ujerumani baada ya ushindi wa pointi dhidi ya Jose Ferero kutoka nchini Panama |
“Lilikuwa pambano la kukata na shoka, hakika haikuwa kazi rahisi kwangu kuibuka mshindi kwenye pambano hilo, kwani mpinzani wangu Jose Ferero kutoka nchini Panama, alionyesha upinzani mkubwa kwa raundi zote 12 kabla ya mimi kuibuka mshindi kwa pointi na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Light,”amesema Ibrahim Class.
Ushindi wa Ibrahim Class unakuja wiki moja, baada ya bondia mwingine Mtanzania, Francis Cheka kupoteza pambano kwa pointi mbele ya Enes Zecirevic ukumbi wa Salle de Fetes, Le Lignon, nchini Uswisi.
No comments:
Post a Comment