Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 25, 2017

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO VIJANA KINONDONI

MABONDIA WAPIMA UZITO KUPIGANA KESHO VIJANA KINONDONI

Mabondia Baina Mazola kushoto akitunishiana misuli na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya mpambano wao jumamoso Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS
Mratibu wa mpambano wa masumbwi kaizirege Dragon Kaizum katikati akiwatambulisha mabondia mbele ya wahandishi wa habari kushoto ni Baina Mazola na Fransic Miyeyusho baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa agost 26 jumamosi hii litakalofanyika katika ukumbi wa vijana kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Selemani Simba akipama uzito kwa ajili ya mpambano wake na Kallage Hassani utakaofanyika jumamosi ya agost 26 katika ukumbi wa vijana kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Kallage Hassani kushoto akituniashiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Kallage Hassani kushoto akituniashiana misuli na Selemani Simba 'Singida United' baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho agost 26  katika ukumbi wa Vijana Kinondoni Picha na SUPER D BOXING NEWS



Mabondia Cosmas Cheka Kushoto akitambiana na Haidal Mchanjo baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni 
Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Baina Mazola 'Simba Mazola' na Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe'  wamepia uzito kwa ajili ya mpambano wao  utakaofanyika jumamosi Agost 26 katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mpambano wa raundi nane uzito wa kg 57

Wakiongea kwa nyakati tofauti kambi hizo zimejigamba kila mmoja kumpiga mwenzake raundi za awali

Kwa upande wa Miyeyusho amejigamba kuwa katika mabondia wa Mabibo wanaofundishwa na kocha Cristopher Mzazi akuna anae msumbua ata mmoja hii ni pambano la kisasi ukumbuke kuwa Mzazi ana mabondia wengi na mimi ndie ninae mwalibia


Kwa upande wa Mazola nae ametamba kumsambalatisha mpinzani wake raundi za mwanzo kwani ana jipya ukumbuke mchezo wa ngumi sio sawa na michezo mingine umri ukienda biashara imekwisha sasa naenda kumstafisha ngumi rasmi yule babu hivyo wapenzi waje kwa wingi siku hiyo ili waone ninavyo mwachisha ngumi

nae mratibu wa mpambano huo kaizirege Dragon Kaizum amesema mbali na mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi wakati bondia kutoka Singida Selemani Simba 'Singida Unaited' atakumbana na Kallage Ramadhani na Sajo Bosco atapambana na Juma Rashidi Issa Nampepecha ataoneshana umwamba na Abbas Mwamba wakati Karim Ramadhani ataoneshana kazi na Yohana Dhobian na Keisii Amali atakuchiana ngumi na Hashimu Chisola na Said Wigo atazipiga na Chicho Ramadhani

Mapambano haya yote yatasimamiwa na Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBC ambayo yenye dhamana ya kuendesha mchezo wa ndondi za kulipwa nchini


Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi  kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuhamasisha mchezo wa masumbwi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...