Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, October 5, 2011

Prof. Tibaijuka alia na wajenzi holela


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akizungumzahii leo jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya Makazi Duniani. Miongoni mwa mambo aliyo yakemea ni watu kujenga katika maeneo ya wazi, hifadhi ya barabara pamoja na walewanao ziba barabara na kuzuia wakazi wengine kufika makwao. Prof. Tibaijuka ametoa wito kwa watanzania wote kuchukua tahadhari hizo mapema kabla ya watendaje wake wa Wizara kufika katika maeneo hayo.
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakimsikiliza Prof Tibaijuka akifungua maadhimisho hayo yaliyoambatana na semina.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Godluck Ole Medeye akiangalia maonesho ya siku ya makazi Duniani.
OfisaMipango Miji wa Wizara, Bwana Mogella akielezea ramani ya Mji mpya wa Kigamboni.

TAIFA STARS YAJIFUA KUWAKABILI MOROCCO JUMAPILI IJAYO


Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars) Athuman Machupa (kushoto) akimtoka kiungo mshamuliaji wa timu hiyo Henry Joseph, wakati wa mazoezi yai timu hiyo, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mandalizi ya mchezo wao na Morocco utakaopigwa jumapili ijayo. Picha na Michuzi blog

HILI NDILO BARAZA JIPYA LA MICHEZO TANZANIA


Waziri Nchimbi akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Mihezo Tanzania walioteuliwa hivi karibuni, ambapo Baraza hili limezinduliwa rasmi na waziri huyo jana jijini Dar es Salaaam. Picha na Micuzi Blog

BALOZI WA INDIA NCHINI AKUTANA NA WANAFUNZI WA IFM


Balozi wa India nchini Kocheril Bhagirath akibadilishana mawazo na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM cha Jijini Dar es salaam Profesa Godwin Mjema na viongozi wengine wa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uzamili katika Biashara za Kimataifa – MBA-IB jana jijini Dar es salaam. Balozi Bharagath amesifu ushirikiano wa IFM na chuo kikuu cha Biashara cha India – IIFT katika utoaji wa kozi hiyo na hivyo kupunguza umuhimu wa watanzania kusafiri India kwa ajili ya masomo hayo.
Balozi wa India nchini Kocheril Bhagirath (katikati mstari wa mbele mwenye suti ya kijivu) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM cha jijini Dra es salaam Mkuu wa Chuo cha IFM akiwemo Profesa Godwin Mjema(kulia kwa Balozi) na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa shahada ya uzamili ya Biashara za Kimataifa – MBA-IB inayotolewa kwa ushirikiano wa IFM na Chuo Kikuu cha Biashara cha India – IIFT. Balozi Bharagath amesifu ushirikiano wa IFM na IIFT katika utoaji wa kozi hiyo hatua inayoimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili hizo na pia kupunguza umuhimu wa watanzania kusafiri India kwa ajili ya masomo hayo.

Martinez amtwanga Barker kwa KO


Martinez amtwanga Barker kwa KO


Atlantic City, Marekani

DHAMIRA ya Darren Barker kuishutua dunia imeingia dosari baada ya kutwangwa kwa KO katika raundi ya 11 na Sergio Martinez.


Barker mwenye miaka 29, aliahidi kurejea

Atlantic City akiwa na mkanda wa dunia wa wa WBC uzani wa middle uliokuwa ukishukiliwa na Martinez.


Lakini upiganaji wake mzuri katika ukumbi wa Boardwalk uliishwa baada ya kutwangwa ngumi ya nyuma ya sikio.


Bingwa huyo wa Ulaya alishindwa kuamka na kuendelea na pambano wakati refa

Eddie Cotton akimhesabia hadi 10 wakati zimbakia sekunde 91 katika raundi hiyo.


Akiwa na maumivu Barker alisema: "Sikumbuki ngumi (iliyompiga), miguu yangu ilianguka chini yangu.


"Nilikuwa nikijaribu kusimama lakini sikuweza.Nimesikitishwa kwa kuwa ilikuwa imebaki raundi moja na nusu tu iliyokuwa imebaki.


"Nilikuwa nikijisikia vizuri pale na sikuhisi kuwa kulikuwa na ngumu nzito kabl ya ile.


"Nilikamatwa na kitu na miguu yangu ilikosa nguvu. Kweli nimesikitishwa kamba sikuweza kuuleta ubingwa nyumbani."



Barker alikwenda katika mechi hiyo huku akiwa hajapoteza pambano katika mechi 23 ambapo alitwaa ubingwa wa Uingereza, Jumuiya ya Madola na Ulaya.


Alikwua hapewi nafasi ya kushinda mbe ya macho ya watu wengi, lakini alikuwa kwenye tabu katika raundi ya 10 dhidi ya mtu ambaye yuko katika namba tatu kwenye viwango vya Dunia.


Lakini mpiganaji huyo wa London ameondoka Marekani akwia kichwa juu kutokana na upiganaji wake mzuri.


Amemwacha Martinez akiwa anatiokw ana damu puani na mpiganaji huyo wa Argentina alimsifu mpinzani waka kwa kumpa kazi ya kufanya kabla ya kuibuka na ushindi.



Bonsi huyo mwenye miaka 36 anayepigana kwa mkono wa kushoto alisema: "Sikuchanganyikiwa hata kidogo, ilikuwa ni kazi nzuri ya Barker.


"Nilitakwia kuyapooza mashambulizi yake, nilitakiwa kumwangusha chini."


Martinez, ambaye hakutaka kukanusua uwezekanow akupigana na Floyd Mayweather, aliongeza : "Nilijua kuwa pambano hili lingekuwa kama hivi.


"Nilipanga hili na kiwa wakati kupata upepo wa pili. Tulifanya mzoezi kwa hili, ni sehemu ya mpango wetu unavyokwenda.


"Tulijua kuwa tutapata uimara kadiri pambano linavyokwenda. Nilikuwa nikiendelea kurusha ngumi ya kulia kwa sababu nilikuwa nikijua haraka au baadaye nitaanda kumpata."

UBO WORLD TOUTH TITLE BETWEEN BORIS MDINAZARDE (GEORGIA ) AND SELEMANI SAIDI ( TANZANIA ) @ GORI - GEORGIA.









Kamati ya mashindano TFF kujadili Daraja la Kwanza Oktoba 10


Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), litakuwa na kikao na viongozi wa klabu 18 za Ligi Daraja la Kwanza Oktoba 10, mwaka huu.

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura, amesema ligi hiyo itakayoanza Oktoba 15, mwaka huu, itashirikisha timu za AFC ya Arusha, Burkina Faso ya Morogoro, Majimaji ya Ruvuma, Mbeya City Council ya Mbeya, Mgambo Shooting ya Tanga, Mlale JKT ya Ruvuma na Morani ya Manyara.

timu nyingine ni Polisi ya Dar es Salaam, Polisi ya Iringa, Polisi ya Morogoro, Polisi ya Tabora, Rhino Rangers ya Tabora, Samaria ya Singida, Small Kids ya Rukwa, Tanzania Prisons ya Mbeya, Temeke United ya Dar es Salaam na Transit Camp ya Dar es Salaam, ambazo zitawekwa katika makundi matatu.

Wambura amesema timu za Majimaji na Small Kids, mpaka sasa hazijalipa ada ya ushiriki ya sh. 200,000 na kwamba, zimetakiwa kulipa ada hiyo kabla ya Oktoba 10, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya kupanga ratiba.

Tuesday, October 4, 2011

MATUKIO YA MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO.


Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, akiteta na mkazi wa wami dakawa , ambaye ni mlemavu wa viungo akihutaji kusidiwa fedha za kununua mipira ya baiskeli yao.
ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA MVOMERO, AMOS MAKALLA, AKIWA JIMBONI KWA AJILI YA KUTEKELEZA AHADI ALIZOTOA WAKATI WA KIPINDI CHA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU ALIPOKUWA AKIPITA KUOMBA KURA ILI ACHAGULIWE KUWA MBUNGE WAJIMBO HILO , LENGO LA ZIARA HIYO NI KUZITEMBELEA SHULE ZOTE 21 ZA SEKONDARI ZILIZOPO KATIKA WILAYA YA MVOMERO KWA AJILI YA KUTOA MASAADA WA VITABU VYA MASOMO YA SAYANSI, HISABATI NA JEOGRAFIA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA HADI NNE PAMOJA NA VIFAA VYA MICHEZO HUSANI MIPIRA.
Mafundi wakiwa kazini kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu sekondari ya Ungulu, Kata ya Kibati, Wilaya ya Mvomero.
Diwani wa Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro kupitia CHADEMA , Tusekile Mwakyoma, akiwahutubia wananchi wa mtibwa kabla ya kumkaribisha Mbunge wa Jimbo hilo, Amos Makalla ( hayupo pichani)
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ,kutoa vitabu vya masomo ya sayansi na hisabati, Sekondari ya Lusanga

Rais Museven wa Uganda azuru Tanzania



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo mchana kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo ikulu jijini Dare s Salaam leo mchana.Rais Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja.

Usalama wa Taifa na 'vita' dhidi ya wapigapicha Tanzania


Maofisa wa usalama wa Taifa wakiwa wamemnyang'anya kamera na kumtoa eneo lake la kazi Mpigapicha wa magazeti ya The Guardian na Nipashe, Khalfan Said wakati wa ujio wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo.
Maofisa hao wamekuwa ni kikwazo kikubwa kwa wapigapicha za habari kufaya kazi zao kwa uhuru jambo linalosababisha kero kwa wapigapicha nchini na hata wakati mwingine kufikia kuwanyang'anya vitendea kazi vyao, kupigwa. Vitendo kama hivi pia vimekuwa vikifanywa na Polisi jambo ambalo linaleta taswira kuwa Wapigapicha nchini ndio watu hatari zaidi kwa vyombo hivi viwili vya usalama.

NSAJIGWA NJE TAIFA STARS

Ni baada ya Nahodha huyo wa timu ya Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa kuumia nyonga (groin) wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa ambaye pia ni Nahodha wa Yanga nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne.

Kutokana na ushauri wa daktari, Kocha Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho ambacho kitasafiri Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9.

Badala yake Kocha Poulsen amemuita kwenye timu yake Nassoro Masoud Said ‘Cholo’ wa Simba kuziba nafasi ya beki huyo wa pembeni.

WACHEZAJI KUTOKA NJE
Wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa na Kocha Poulsen wameanza kuwasili. Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya na Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili jana jioni na tayari wameripoti kambini Taifa Stars.

Henry Joseph wa Kongsvinger IL ya Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) wanatarajiwa kuwasili leo (Oktoba 3 mwaka huu) usiku kwa ndege ya KLM.

Washambuliaji Abdi Kassim na Dan Mrwanda wanaochezea timu ya DT Long An ya Vietnam ndiyo watakaokuwa wa mwisho kujiunga na kambi ya Stars ambapo watawasili nchini kesho (Oktoba 4 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Qatar Airways.

Sunday, October 2, 2011

MABONDIA WA TANGA WANYAKUA MIKANDA YOTE YA TPBO KATIKA VIWANJA VYA TANGAMANO





Bondia Saidi Mundi wa Tanga akinoshwa mkono juu baada ya kumtwanga Mohamedi Bakari wakati wa
mchezo wa kugombania mkanda wa ubingwa wa taifa wa chama cha ngumi za kulipwa TPBO viwanja
vya tangamano TANGA.(http://www.superdboxingcoach,blogspot.com/)













furaha ya ubingwa





ngumi sio uadui hapa mabondia wakisalimiana





Alani kamote wa tanga akitupa makonde





mashabiki kibaoooo







Nakwambia umuwezi bondia yoyote wa tanga karibu tena ndio anavyosema mmoja wa wadau wa ngumi baada ya bondia wake kushinda



Bondia Haji Juma wa Tanga kushoto akipambana na Juma Sel;emani wa Dar wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa KG.48 uliofanyika katika viwanja vya tangamano jijini tanga















KASEBA ALIVYOCHUKUA UBINGWA WA PST UZITO WA KG. 72



Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Iddy Azani akimvisha mkanda wa ubingwa unaotambuliwa na chama cha mchezo wa ngumi za kulipwa PST bondia Japhet Kaseba baada ya kumtwanga Maneno Oswald kwa Point jijini Dar es salaam jana.(picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)



Baadhi ya mashabiki wakiangalia mpambano

Ernest Bujiku alitoka sale na Ambokile Chusa











Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...