Ni baada ya Nahodha huyo wa timu ya Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa kuumia nyonga (groin) wakati akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa daktari wa Taifa Stars, Dk. Mwanandi Mwankemwa, maumivu hayo yatamweka Nsajigwa ambaye pia ni Nahodha wa Yanga nje ya uwanja kwa kati ya wiki mbili hadi nne.
Kutokana na ushauri wa daktari, Kocha Jan Poulsen amemuondoa kwenye kikosi hicho ambacho kitasafiri Oktoba 6 mwaka huu kwenda Casablanca, Morocco kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Oktoba 9.
Badala yake Kocha Poulsen amemuita kwenye timu yake Nassoro Masoud Said ‘Cholo’ wa Simba kuziba nafasi ya beki huyo wa pembeni.
WACHEZAJI KUTOKA NJE
Wachezaji wanaocheza nje ya nchi walioitwa na Kocha Poulsen wameanza kuwasili. Idrissa Rajab anayechezea Sofapaka ya Kenya na Mbwana Samata wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili jana jioni na tayari wameripoti kambini Taifa Stars.
Henry Joseph wa Kongsvinger IL ya Norway), Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) wanatarajiwa kuwasili leo (Oktoba 3 mwaka huu) usiku kwa ndege ya KLM.
No comments:
Post a Comment