Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, October 2, 2011

WAZIRI DK. NCHIMBI AZINDUA MFUMO WA DIGITAL WA KAMPUNI YA VING'AMUZI YA STARTIME MEDIA KWA KUSHIRIKIANA NA TBC


Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda katikati, akizindua mfumo wa Kidigital utakaotumiwa na kampuni ya Televisheni kupitia Ving'amuzi Startime Media usiku huu, katika hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Godfrey Nyachia Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TBC, Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng na kutoka kushoto ni Clement Mshana Mkurugenzi wa TBC na Mwenyekiti wa Bodi ya Startime Bw. Pang Xingxing wakishiriki pamoja na Waziri kuzindua mfumo huo.
Hapa tayari wameshazinduza kama linavyoonekana neno Startime katika tufe hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi katikati akigonganisha glasi kama ishara rasmi ya uzinduzi wa mfumo wa Kidigital utakaotumiwa na kampuni ya Televisheni kupitia Ving'amuzi Startime usiku huu kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es salaam kutoka kulia ni Godfrey Nyachia Mwenyekitiwa Bodi ya wakurugenzi TBC, Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng na kutoka kulia ni Clement Mshana Mkurugenzi wa TBC na Mwenyekiti wa Bodi ya Startime Bw. Pang Xingxing wakishiriki wakishiriki kwa pamoja katika kugonganisha glasi
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa hotuba yake kwa niaba ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi huo.
Kutoka kulia ni Davis Mwijage Meneja Masoko Msaidizi, Pamela, Kidali na Freddy Mlay wakipozi kwa picha.
Makamanda wa Startime Media wakiwa katika picha ya pamoja.
Kutoka kulia ni Freddy Mlay afisa masoko, Zuhura Meneja Masoko na Davis Mwijage Meneja masoko Msaidizi.
Eeh Pozi lingine tena kutoka warembo wa Startime Media.
Mwigizaji Steven Kanumba akiingia katika hafla ya uzinduzi huo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na balozi wa China nchini Tanzania Balozi Liu Xinsheng, kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Star Time Media Bw. Pang Xingxing.
Vimwana wa kampuni ya Startime wakipozi kwa picha.
Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana kulia na Mwenyekiti wa bodi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Godfrey Nyachia wakijadilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Digital wa kampuni hiyo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh Dk. Emmanuel Nchimbi akiingia ukumbini, tayari kwa kuzindua kampuni ya Televisheni kwa njia ya Ving'amuzi, kulia ni Mkurugenzi wa TBC Clement Mshana.
Bw Davis Mwijage meneja msaidizi wa Masoko akieleza jambo mbele ya mitambo ya kurushia matangazo ya kampuni hiyo kwa waandishi wa habari kulia ni Zuhura Meneja Masoko wa Startime , wengine kutoka kushoto ni Salum Shomari fundi na Terry Du Meneja mkuu wa ufundi.
Meneja mkuu wa ufundi Terry Du kushoto na moja wa mafundi wa kampuni hiyo Salum Shomari , Davis meneja msaidizi wa masoko na Zuhuru Meneja Masoko wa Star Time wakiwaongoza waandishi wa habari, wakati walipotembelea eneo la mitambo ya kupokelea matangazo na kurusha iliyopo mikocheni jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa ufundi wa kampuni ya Startime Media Bw Terry Du akiwaelezea waandishi wa habari, jinsi mitambo ya kampuni hiyo inavyorusha matangazo yake katika ziara waliyoifanya kabla ya kampuni hiyo kuzinduliwa rasmi leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...