Marquee
tangazo
Monday, December 31, 2012
"NAFSI NI NYONGE" TUSAMEHEANE NA MAISHA YAENDELEE. KARIBU 2013 KWA UFANISI ZAIDI
Wapendwa ndugu, jamaa na marafiki
popote pale mlipo,yamebaki masaa kadhaa kuuaga mwaka 2012, ambao kwa
hakika ulikuwa na changamoto nyingi za kimaisha, dhoruba za hapa na pale
wengi zilitukumba, lakini kwa kudra za Mwenyezi Mungu akatushika mkono
akatuinua na maisha yakaendelea.
Binafsi mpaka dakika hii namshukuru
Mungu nikiwa mwenye afya njema kabisa. Maisha ya sasa Wanadamu wengi
wamekuwa dhaifu kwa mambo mengi, lakini Mungu ndiyo njia sahihi wa
kumtumia katika sala zako kuyashinda majaribu na madhaifu ya Dunia. Yako
mengi ambayo naweza nikayaandika hapa lakini bado yasitoshe pia. Nasema
asanteni kwa ushirikiano wenu mkubwa kwa namna moja ama nyingine, kama
kuna mahali nilikosea, tukakwaruzana kidogo basi "NAFSI NI NYONGE"
Tusameheane na maisha yaendelee.
Tunahamia mwaka mwingine mpya kabisa
2013, basi na tuendelee na ushirikiano huu tuliokuwa nao kwa mambo
mbalimbali yenye kujenga na kuleta tija katika maisha yetu, Mwaka 2013
uwe wa kuhakikisha kweli sote pia tumehamia kwenye mfumo wa kidijitali,
tushauriane, tuelemishane tunyooshane njia iliyo sahihi ili kila mmoja
kila wakati abaki nafsini mwake mwenye furaha daima, Pia tumtangulize
Mungu kila wakati kwa kila jambo ili pia azidi kuzibariki kazi za mikono
yetu daima.
Kwa Blogaz wenzangu, changamoto
nyingi tumekumbana nazo 2012, ikiwemo tatizo kuu la KUKOPY NA KUPASTE.!
Na nyinginezo nyingi tuzijuazo zinatusumbua kwa namna moja ama nyingine,
basi ni nyema 2013 iwe ya kuzitafutia ufumbuzi, kama si kuzimaliza
kabisa basi angalau tuendelee kuzipunguza ili kuzimaliza kabisa, huku
suala la kujituma na ubunifu vikiwa ndio ngao kuu ya mabadiliko miongoni
mwetu. Ushirikiano tuliokuwa nao umeonesha tuna uwezo mkubwa wa
kuisadia jamii inayotuzunguka na hata serikali pia kwa namna moja ama
nyingi, basi tusimame kidete kuhakikisha ushirikiano huu hauteteleki ama
haupotei kirahisi, badala yake tuiimarishe zaidi kila kona.
Natoa shukurani za dhati kabisa kwa
makampuni na wadau mbalimbali ambayo/ambao kiukweli yametoa mchango
mkubwa kuhakikisha tunasonga mbele na libeneke hili , si vibaya
nikiyataja makampuni hayo kuwa ni Serengeti Breweries Ltd, Airtel,
Bayport, Msama Promotions Ltd, kampuni ya R&R, Dada Teddy Mapunda,
Hoyce Temu, Blogaz wote (bila kinyongo) na wengine waliotupa hatua ya
kusogea kwa namna moja ama nyingine, Mungu awabariki sana.
Asanteni
Nawatakia heri ya sikukuu ya Mwaka mpya.
JK KUTOA SALAMU ZA MWAKA MPYA
Rais Jakaya Kikwete
THE
UNITED REPUBLIC
OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
![]() |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE
STATE HOUSE,
P.O. BOX
9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jioni ya leo, Jumatatu, Desemba 31, 2012,
atatoa salamu maalum za Mwaka Mpya kwa wananchi.
Rais
Kikwete atatoa salamu hizo kupitia hotuba yake kwa Taifa ambayo ataitoa kwa
njia ya redio na televisheni.
Katika
salamu hizo, Rais Kikwete anatarajia kuzungumzia masuala mbali mbali kuhusu
matukio makubwa ya mwaka huu na mengine muhimu yaliyojitokeza katika jamii ya
Tanzania katika miezi 12 iliyopita.
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
31
Desemba, 2012
MASHAHIDI WAKWAMISHA KESI YA PONDA LEO
Katibu Mkuu wa
Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiingia katika
chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo
pamoja na washtakiwa wenzake 49, hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa
kutokana na mashahidi upande wa mashtaka kutofika mahakamani hapo.
(Picha na Habari Mseto Blog)
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa na mshtakiwa mwenzake, Mukadam Abdal Swalehe (kushoto)
Baadhi ya wafuasi wa Sheikh Ponda wakiwa katika viunga vya mahakama ya Kisutu
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda na mshtakiwa mwenzake Mukadam Abdal Swalehe wakitoka mahakamani chini ya ulinzi wa askari magereza.
Ulinzi uliimarishwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu leo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia) akiwa na washtakiwa wenzake.
MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI ZAWADI ZA MWAKA MPYA KWA KITUO CHA TUSHIKAMANE CHILDREN CARE TRUST FUND.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane
Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na
Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa
watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho
atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni
Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi
ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima
na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa
mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya
shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.
Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa
akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya
kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika
kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.
Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka
mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa
wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.
Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa
chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio
Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund
ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.
Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s
Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka
huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.
YANGA YAANZA MAZOEZI RASMI UTURUKI.
![]() |
| Tumeanaza mafunzo! |
![]() |
| Tunadaka kwa utaratibu. |
YOUNG Africans Sports Club imeanza mazoezi leo asubuhi katika viwanja vya
Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara &
Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki
mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi
Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo
yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu
ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku
asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya
Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym)
ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya
soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu
kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti
duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameandaa
sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji
wa mji huo watasherehekea pamoja.
TRA Tatizo nini Sheria au Mfumo?
MTU MMOJA AJERUHIWA MADARASA SITA YAEZULIWA NA UPEPO.
| Bati zilizoezuliwa na upope huo mkali ulioacha athari kubwa. |
| Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo. |
ONYESHO LA BENDI YA AKUDO IMPACT MSASANI BEACH
Wanenguaji
wa bendi ya Akudo Impact, wakishambulia jukwaa wakati wa onyesho lao,
lililofanyika jana jumapili kwenye Ukumbi wa Msasani Beach Club, ambapo
bendi hiyo hufanya onyesho la Bonanza katika ukumbi huo kila siku ya
Jumapili.
Mashambulizi yanaendelea jukwaani,,,
Rapa wa bendi hiyo (kulia) akiwachezesha wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa onyesha hilo.
RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI MATOKEO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI
Rais
Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba,
wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi
matokeo ya Sensa ya watu na makazi.
Bango
linaloonyesha Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika
zoezi la kuhesabu Sensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia
tamati hii leo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo ya Senza ya watu na makazi na
kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya
kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo
katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya,
alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa
asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza
nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12,
313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani
Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama
hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012,
ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44,
929,002.
Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
Kikundi
cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa
kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais
Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba,
wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi
matokeo ya Sensa ya watu na makazi.
KLABU ZA JOGGING JIJINI DAR ZAAGA MWAKA KWA BONANZA , MBUNGE WA KINONDONI ASHIRIKI AWAAMBIA HAKUNA SABABU YAKWENDA LOLIONDO MAZOEZI YANATOSHA.
| Vijana wa Klabu ya Jogging ya Barafu Magomeni wakifanya mazoezi kwenye bonanza hilo. |
|
Timu ya kuvuta kamba ya wanawake ya Klabu
ya Jogging ya Barafu Magomeni jijini Dar es Salaam ikivutwa na Timu ya Klabu ya
Jogging ya Kawe na kuondolewa.
|
| Mbunge wa Kinondoni Iddi Azzani akishiriki mazoezi ya kukimbia ya umbali wa Kilometa nane yaliyofanywa na Klabu za Jogging jijini Dar es Salaam leo. |
| Pamoja na kuwepo kwa mvua vijana hao hawakuacha kufanya mazoezi. |
| Mvua si sababu ya kuacha mazoezi. |
|
Iddi Azzani akiongoza timuyake ya Klabu ya
Jogging ya Barafu ya Magomeni na kuibuka kidedea.
|
| Vijana wakichangamsha damu asubuhi yaleo! |
|
Katibu wa Kawe Jogging Klabu (Mdau) Razalo
Ngimba (katikati) akiwa na Refaree maarufu nchini Othmani kazi (kulia) wakati
wa mazoezi kabla ya bonanza kuanza.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)





















