Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 9, 2015

MADA MAUGO NA KALAMA NYILAWILA WASAIDI KUZIPIGA MARCH 8 P.T.A SABASABA




Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS
Katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Antoni Rutta katikati akiwainua mikono juu mabondia Mada Maugo na Kalama Nyilawila wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika march 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS


Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS
mabondia wakiwa katika picha ya pamoja kushoton ni Emilio Norfat,Nassibu Ramaradhani,Mohamed Matumla na Amosi Mwamakula
MADA MAUGO NA KALAMA NYILAWILA WASAIDI KUZIPIGA MARCH 8 P.T.A SABASABA Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS Katibu mkuu wa chama cha ngumi za kulipwa nchini Antoni Rutta katikati akiwainua mikono juu mabondia Mada Maugo na Kalama Nyilawila wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika march 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakitunishiana misuli wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika March 8 katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba Picha na SUPER D BOXING NEWS mabondia wakiwa katika picha ya pamoja kushoton ni Emilio Norfat,Nassibu Ramaradhani,Moham Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

RIDHIWANI KIKWETE AAPA KUPAMBANA NA MATAPELI WA ARDHI JIMBO LA CHALINZE


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi  sita iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa na matapeli katika jimbo lake la Chalinze.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi
 Mkuu wa Miradi wa Mkoa wa Pwani wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi umeme utakavyosambazwa katika Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine Jimbo la Chalinze.
 Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru mbunge kwa ahadi mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika kijiji hicho.
 Ridhiwani akibadilishana mawazo na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Fukayosi Jimbo la Chalinze.
 Mwenyekiti mstaafu wa Kata ya Fukayosi,Adam Masoud  akimuomba Mbunge Ridhiwani kuhikisha anaweka miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya katika Kijiji cha Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi.
 Mkazi wa Kijiji cha Mkenge, Khamis Mwanga akielezea kero ya barabara ya Mwavi hadi Mkenge ambayo alidai inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho hivyo kumtaka Ridhiwani awasaidia kuijenge barabara hiyo ili iweze kupitika bila matatizo katika vipindi vyote. Ridhiwani aliwajibu kuwa tayari barabara hiyo imepata mkandarasi anayetarajia kuanza kazi katika siku chache zijazo.
 Katibu wa CCM Tawi la Mkenge, Omar Seleman akimuomba Mbge Ridhiwani asaidie kumalizia ujenzi wa msikiti wa Mkenge, Ombi ambalo alilikubali na kuahidi kupaua kwa gharama zake.
 Ridhiwani akijibu maswali mbalimbali ya wananchi wakati wa mkutano katika Kijiji cha Mkenge
 Ridhiwani akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Mkenge ambao ameahidi kuchangia mabati na mbao za kupaua jengo hilo la ibada.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Fukayosi, Olnjurie Marigwa akihtubia katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi
 Masoud Fundikira akimuomba Mbunge wao Ridhiwan, anzishe mashindano ya mpira wa miguu kuwania kikombe cha Ridhiwani Cup ili kuendeleza michezo katika jimbo hilo. Ridhiwani alilikubali ombi hilo kwa kuanzia kutoa misaada ya mipira na jezi katika kila timu ya kata za jimbo hilo.
 Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Mwavi ambapo aliahidi kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la alilogawiwa Mkorea ili kijiji cha mwwavi kipate haki.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Kombo Kamote, akiwafunda viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwavi waliochaguliwa hivi karibuni ili wawatendee haki wananchi.
 Ridhiwani akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kidomole, ambapo aliwajia juu anaowaita matapeli wanaouza ardhi katika Jimbo la Chalinze bila kufuata sheria na utaratibu. Alisema kuwa hayuko tayari kuona hata heka moja ya jimbo hilo ikikuzwa bila utaratibu.
Ridhiwani akiagana na Meya wa  Morogoro, Amir Nondo ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo hilo la Chalinze.
RIDHIWANI KIKWETE AAPA KUPAMBANA NA MATAPELI WA ARDHI JIMBO LA CHALINZE Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete,akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Fukayosi, Kata ya Fukayosi, wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge miezi sita iliyopita.Ridhiwani kutoruhusu hata kipande cha heka moja kuporwa na matapeli katika jimbo lake la Chalinze.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG Kijana Salumu Khamis akiuliza swali mbele ya Mbunge Ridhiwani Kikwete kuhusu tatizo la maji katika Kijiji cha Fukayosi Mkuu wa Miradi wa Mkoa wa Pwani wa Tanesco, Leo Mwakatobe, akielezea jinsi umeme utakavyosambazwa katika Kijiji cha Fukayosi na vijiji vingine Jimbo la Chalinze. Mwenyekiti mpya wa Serikali ya Kijiji cha Fukayosi, Salum Mkwecha akimshukuru mbunge kwa ahadi mbalimbali alizozitoa katika miradi mbalimbali katika kijiji hicho. Ridhiwani akibadilishana mawazo na mmoja wa watawa baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Fukayosi Jimbo la Chalinze. Mwenyekiti mstaafu wa Kata ya Fukayosi,Adam Masoud akimuomba Mbunge Ridhiwani kuhikisha anaweka miundombinu ya barabara na maji na masuala ya afya katika Kijiji cha Mkenge,wakati wa ziara yake katika Kata ya Fukayosi ya kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuangalia jinsi ya kuzitafutia ufumbuzi. Mkazi wa Kijiji cha Mkenge, Khamis Mwanga akielezea kero ya barabara ya Mwavi hadi Mkenge ambayo alidai inarudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho hivyo kumtaka Ridhiwani awasaidia kuijenge barabara hiyo ili iweze kupitika bila matatizo katika vipindi vyote. Ridhiwani aliwajibu kuwa tayari barabara hiyo imepata mkandarasi anayetarajia kuanza kazi katika siku chache zijazo. Katibu wa CCM Tawi la Mkenge, Omar Seleman akimuomba Mbge Ridhiwani asaidie kumalizia ujenzi wa msikiti wa Mkenge, Ombi ambalo alilikubali na kuahidi kupaua kwa gharama zake. Ridhiwani akijibu maswali mbalimbali ya wananchi wakati wa mkutano katika Kijiji cha Mkenge Ridhiwani akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti wa Mkenge ambao ameahidi kuchangia mabati na mbao za kupaua jengo hilo la ibada. Mwenyekiti wa CCM Kata ya Fukayosi, Olnjurie Marigwa akihtubia katika mkutano uliofanyika katika kijiji cha Mwavi, Kata ya Fukayosi Masoud Fundikira akimuomba Mbunge wao Ridhiwan, anzishe mashindano ya mpira wa miguu kuwania kikombe cha Ridhiwani Cup ili kuendeleza michezo katika jimbo hilo. Ridhiwani alilikubali ombi hilo kwa kuanzia kutoa misaada ya mipira na jezi katika kila timu ya kata za jimbo hilo. Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Mwavi ambapo aliahidi kufuatilia kwa karibu kuhusu suala la alilogawiwa Mkorea ili kijiji cha mwwavi kipate haki. Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Kombo Kamote, akiwafunda viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwavi waliochaguliwa hivi karibuni ili wawatendee haki wananchi. Ridhiwani akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Kidomole, ambapo aliwajia juu anaowaita matapeli wanaouza ardhi katika Jimbo la Chalinze bila kufuata sheria na utaratibu. Alisema kuwa hayuko tayari kuona hata heka moja ya jimbo hilo ikikuzwa bila utaratibu. Ridhiwani akiagana na Meya wa Morogoro, Amir Nondo ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Kiwangwa katika jimbo hilo la Chalinze. Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Bondia mtanzania Omari Kimweri anayetesa Australia kutoa sapoti ya mafunzo ya ndondi Dar



Omari Kimweri

.Kutua Februari, apania kuzalisha akina Mayweather kibao nchini

NA Mwandishi wetu

NDONDI ni miongoni mwa michezo maarufu mno hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.

Wapo wanamichezo waliojipatia heshima kubwa duniani kutokana na kufanikiwa kupitia mchezo wa ndondi.

Miongoni mwa wanamichezo hao ni nguli Mohammed Ali, Mike ‘Iron’ Tyson, Evender Holyfield, Floyd Mayweather, Manny Pacquiao na wengineo wengi.

Kwa hapa nchini, wapo mabondia waliojitengenezea majina wakiwamo Emmanuel Mlundwa, Habibu Kinyogoli 'Masta' Michael Yombayomba, Stanley Mabesi 'Ninja' Rashid Matumla, Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  na wengineo wengi.

Lakini ikumbukwe kuwa ndondi ndio mchezo uliotoa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani kwa sasa ambaye si mwingine bali ni Mayweather, akifuatiwa na mwanasoka raia wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.

Anayeshika nafasi ya tatu ni mchezaji wa mpira wa kikapu LeBron James, wakati mwanasoka anayechezea Barcelona ya Hispania, Muargentina Lionel Messi akishika nafasi ya nne, huku wa tano akiwa ni mkali wa mpira wa kikapu, Kobe Bryant.

Pamoja na mafanikio hayo katika ndondi, Tanzania imeonekana kuzidi kulala usingizi wa pono katika suala zima la kuvumbua na kuendeleza vipaji vya mchezo huo kama sehemu ya kutatua tatizo sugu la ajira linaloitesa nchi yetu kwa sasa.

Unapopita huko mitaani, unaweza kukutana na vijana wadogo wakiwa wanafanya mazoezi ya ngumi kwa kutumia vifaa visivyo rasmi ambavyo mwisho wa siku, huishia kuwadumaza badala ya kuwajenga kama walivyotarajiwa.

Hali hiyo imetokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifunzia mchezo huo, zikiwamo kumbi na hata wataalam wa kuwapa ujuzi wa kuwawezesha kufikia mafanikioi ya akina Mayweather.

Ni kwa kufahamu hilo, wapo wadau wa ndondi ambao wamekuwa wakijitoa kusaidia vipaji vya ndondi hapa nchini, miongoni mwao akiwa ni Kocha wa Kimataifa wa Ndondi nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’.

Bondia huyo wa zamani, ameshawahi kufanya jitihada kadha wa kadha kuendeleza ndondi hapa nchini, ikiwamo kutoa mafunzo kwa vijana chini ya klabu yake ya Ashanti Boxing Club na kupitia DVD zake zenye mapambano makali yaliyowahi kufanyika hapa nchini na duniani kwa ujumla, yakiwahusisha mabondia nyota.

Katika kuonyesha jinsi anavyoguswa na ndondi, Februari mwaka huu Super D atakuwa na ugeni mkubwa wa bondia Mtanzania anayefanya kazi zake nchini Deer Park, Victoria, Australia, Omari Kimweri ambaye anatua nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wanamasumbwi wa Tanzania.

Akizungumza Dar es salaam jana, Super D anasema kuwa ujio wa Kimweri ni fursa nyingine adimu kwa mabondia wa Tanzania katika kuona ni vipi wanaweza kutimiza ndoto zao za kutoka kimaisha kupitia mchezo huo.

Anasema kuwa Kimweri atatua akiwa na vifaa mbalimbali vya masumbwi ambapo pia atatoa mafunzo na mbinu mpya zinazotumiwa na mabondia wa nje kwa mabondia pamoja na kushuhudia mapambano kadhaa yatakayofanyika kwa kipindi atakachokuwapo hapa nchini.

“Kimweri anakuja akiwa na msafara wa watu kadhaa, akiwamo mwanasoka wa kike, Melanie Gines ambaye ni raia wa Hispania. Akiwa hapa nchini, Melanie atapata fursa ya kukutana na wanasoka wa kike wa hapa , kwani amechezea timu nyingi za Ulaya,  Hispania,” anasema Super D.

Anasema kuwa ujio wa Kimweri umewezeshwa kwa kiasi kikubwa na promota wake, Brian Amatruda ambaye ni miongoni mwa mapromota maarufu nchini kwao Australia, akiwa amekubali kutoa baadhi ya vifaa vya kisasa kutoka Hispania na Marekani kwa ajili ya ziara hiyo.

Super D anasema kuwa Kimweri ambaye ni bingwa wa WBO, atatua nchini akiwa na mikanda yake yote aliyowahi kutwaa, ukiwamo wa ubingwa wa Australia, lengo likiwa ni kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujikita zaidi katika ndondi.

“Nimezungumza na Kimweri na ameonyesha kuwa na uchungu wa kuwainua mabondia wa hapa nchini ili waweze kutimiza ndoto zao na anafanya hivyo chini ya mradi wake wa ‘Kimweri Project’ na atakuwa hapa nchini kwa wiki moja,” anasema.

Anasema kuwa ujio wa bondia huyo uliochagizwa na Super D Boxing Coach and Promotion, umelenga kuwahamasiaha mabondia kucheza mara kwa mara ili kupandisha viwango vyao kwani hiyo ndio siri ya mafanikio ya wanamasumbwi wengi duniani.


Mbali ya mafunzo kutoka kwa Kimweri, pia katika ziara zake zote sehemu mbalimbali nchini, kutakuwa na uuzwaji wa DVD za Super D zenye lengo la kutoa mafunzo kupitia mapambano ya mabondia maarufu duniani, akiwamo Floyd Mayweather,Manny Paquaio, Mohamerd Alli, na wa hapa nchini kama Mbwana Matumla, Francis

Miyeyusho,Ibrahimu Class' King Class Mawe' ambaye ni bingwa wa WPBF Africa na wengineo.
OMARI KIMWERI
bondia  Omari Kimweri ambaye ni bingwa wa uzito wa flyweight nchini Deer Park, Victoria, Australia anatalajia kucheza mpambano wake mwingine march 13 mpambano utakaopigwa katika ukumbi wa
The Melbourne Pavilion, Flemington, Victoria, Australia

Airtel kuzindua Airtel UNI 255 J-mosi maalum kwa Wanafunzi UDSM katika Viwanja vya Mabibo Hostel





Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM 
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel 
 Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”
 “Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando 
 Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE”
 Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255  siku hiyo.
 Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.

Serikali yatumia Shilingi Bilioni 881 katika Mradi wa REA Awamu ya Pili


Mmoja wa wakazi kutoka katika Kata ya Nkoma iliyopo  Wilayani Meatu mkoani Simiyu  (kushoto) akitoa neno la shukrani mbele ya  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) baada ya Wizara ya Nishati na Madini  kusambaza umeme  katika kata hiyo kupitia  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili. Kijiji cha Nkoma ni moja ya vijiji  170  vilivyopo mkoani Simiyu vilivyofaidika na mradi wa umeme  vijijini  unaotekelezwa na  REA Awamu ya Pili.
Mtaalamu kutoka  Kampuni ya  LTL (PVT) LTD inayosambaza miundombinu  ya umeme vijijini katika Wilaya ya Maswa  chini ya mradi wa REA Awamu ya PIli  Michael  Marenye (kulia), akifafanua hatua iliyofikiwa ya uunganishaji wa umeme  katika  Kata ya Balyanaga mbele  ya  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara Waziri  Muhongo alipofanya mkutano  na wakazi wa Kata Balyanaga ili  kusikiliza kero zao.

Na Greyson Mwase, Maswa.
Meneja Utaalamu Elekezi  kutoka  Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) Gissima Nyamohanga amesema kuwa serikali imetumia shilingi bilioni 881 katika mradi wa kusambaza umeme  vijijini  unaotekelezwa na  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili.
Nyamohanga aliyasema hayo kwenye  sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini unaofadhiliwa na REA uliofanyika katika kata ya Shishiyu wilayani Maswa mkoani  Simiyu.
Alisema kuwa Mradi wa  REA  Awamu ya Pili  utaiwezesha  idadi ya  vijiji  vilivyounganishwa   na umeme 3734  kati ya vijiji 15,180 ambayo ni asilimia 24.6 kufikia vijiji 5,234 ambayo ni asilimia 34.5 ifikapo  mwezi Juni mwaka huu.
Aliongeza kuwa mradi wa REA Awamu ya Pili wa miaka miwili  ulioanza mwaka 2013, lengo lake lilikuwa  ni kuhakikisha kuwa vijiji vyote Tanzania vinapatiwa umeme hivyo kuboresha maisha  ya wananchi na kukuza uchumi wa nchi.
Akielezea mchango wa mradi wa usambazaji wa umeme  vijijini  unaotekelezwa na  REA katika kuboresha maisha  ya wananchi Nyamohanga alisema kuwa awali wananchi  wote walikuwa wakilipa  shilingi  467,000 kama  gharama ya kuunganishiwa umeme ambayo ilikuwa ni kubwa na kupelekea  wananchi wachache wenye uwezo kuwa na  nishati ya  umeme huku  ikiacha kundi kubwa la wasio na uwezo kuishi  gizani.
Alisema kuwa katika Awamu ya Kwanza ya REA gharama za uunganishaji wa umeme  zilishuka kutoka  shilingi 467,000 hadi shilingi 177,000 na kuongeza kuwa katika kuhakikisha  kila mwananchi anakuwa na uwezo wa kuunganishiwa umeme  Serikali iliamua  kubeba  gharama zote kupitia REA Awamu ya Pili na wananchi kutakiwa kuchangia shilingi 27,000 tu kama kodi ya ongezeko (VAT)
Alieleza kuwa mara baada ya kumalizika  kwa Awamu ya Pili ya REA, viongozi wataainisha  vijiji ambavyo havijapata  umeme REA Awamu ya Pili, ambapo vitajumuishwa katika mradi wa REA Awamu ya Tatu.
Nyamohanga alieleza michango mingine kuwa ni  kufungua  fursa za ajira na uwekezaji kwa vijana wa kitanzania, ufaulu  kuongozeka kwa shule za sekondari na kuboreshwa kwa huduma za afya.
“Kwa mfano kwa shughuli za kiuchumi bei ya kusaga  debe la mahindi ilikuwa ni shilingi 1,000 itashuka  hadi shilingi  500 kutokana na kwamba mashine za kusaga zitakuwa zinatumia  umeme badala ya  dizeli kama zamani,” alisema Nyamohanga
Wakati huohuo Meneja wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya  Ziwa Mhandisi  Joyce Ngahyoma akielezea jinsi ya kuunganishwa na huduma ya umeme kwa wananchi wa vijiji  vilivyopitiwa na mradi wa REA  Awamu ya Pili alisema kuwa wananchi wanaoishi  mita 30 karibu na miundombinu ya umeme wataunganishiwa kwa shilingi  27,000 na kuwataka kuchangamkia fursa hiyo kwa kuboresha makazi yao.
Alisema kwa wananchi wenye  nyumba zenye  vyumba viwili na vioski hawahitaji kufunga mfumo wa umeme kwenye nyumba zao (wiring) badala yake watashauriwa kununua kifaa maalumu kijulikanacho kama “UMETA” (Umeme Tayari) kinachoweza kutumika kama mfumo kwa kuwa na uwezo wa kuunganisha taa mbili na vifaa vingine  kama  vile jiko, friji na pasi.
Aliendelea kusema kuwa kifaa hicho kinachouzwa kwa gharama ya shilingi 37,000 kitakuwa ni mali ya mteja na endapo atahama makazi basi atakuwa huru kuhama pamoja na kifaa chake.
Airtel kuzindua Airtel UNI 255 J-mosi maalum kwa Wanafunzi UDSM katika Viwanja vya Mabibo Hostel Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX · Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma hiii ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo” “Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE” Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255 siku hiyo. Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao. Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Saturday, January 3, 2015

NGUMI ZILIVYOPIGWA MANZESE KATIKA KIPINDI CHA XMASI NA MWAKA MPYA

Bondia Jacobo Maganga kushoto akipambana na Shabani Kaoneka wakati wa mpambano wao uliomalizika kwa sare Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia wa uzito wa juu Iddi Bonge kushoto na Mussa Mbabe wakipambana wakati wa mpambano wao Bonge alioshinda kwa K,O ya raundi ya kwanza na kumsambalatisha Mussa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Shomari nMirundi kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akiwa na mabondia Shomari Mirundi katikati na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anayejiandaa kugombani amkata wa UBO Africa na bondia Cosmas Cheka Feb 28
Bondia Ramadhani Kumbele kushoto akipambana na moro best wakati wa mbambano wao kumbele alishinda kwa pointi mpambani huo wa raundi sita Picha na SUPER D BOXING NEWS

Dula mbabe akivalishwa glove na Shomari Kimbau
Mabondia Abdallah Pazi Kushoto na Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mbambao wao wa kufungua mwaka uliomalizika kwa droo baada ya kugongana vichwa katika raundi ya tatu  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Mabondia Abdallah Pazi Kushoto na Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mbambao wao wa kufungua mwaka uliomalizika kwa droo baada ya kugongana vichwa katika raundi ya tatu  Picha na SUPER D BOXING NEWS

Polisi Dar wakamata Panya Road wawili, wakiwaondoa hofu wananchi

   


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiJDwfvhEw0RWQuBy_ecE7t6K9zCBeYlfzItpU1RWO2JIO2wyCSsAPHV4J4NL8MFsB8OLSfjrViAbxXM_fo1mdZTEd3vRasqWtVkQ1NcNvO5X2Uv8RgECMtmTua78zQVjheSWUWNp652RIV/s1600/Kova1(30).jpg
Kamanda Kova
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewaondoa hofu wakazi wa jiji hilo juu ya kuzagaa kwa habari za uvamizi wa kundi la vijana wahuni la Panya Road, ingawa Kamanda wa Polisi Suleima Kova amekiri kutokea tukio hilo na vijana wawili wameshatiwa mbaroni mpaka sasa.
Akihojiwa muda mfupi na kituo cha TBC1, Kamanda Kova alisema kuwa usambazaji wa taarifa juu ya kundi hilo zimekuzwa sana na kuleta hofu kutokana na uvumi uliosambazwa na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.
Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi limedhibitiwa tangu walipoanzisha fujo zao na wawili walishatiwa mbaroni na sasa wanaendelea kuwataja wenzao ili kuwasaka walioibua taharuki hiyo.
"Uvumi huu wa kutumiana meseji na kutumia mitandao ya kijamii imeleta taharuki na kukuza jambo kinyume na uhalisia, lakini nataka kuwamabia wakazi wa Dar wasiwe na hofu jeshi la Polisi limewadhibiti na vijana wapo kazini kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa shwari,'" alisema Kamanda Kova.
Tangu jioni kulikuwa na taarifa za kuwepo kwa matukio ya uporaji na uvamizi uliokuwa ukidaiwa kufanywa na Panya Road, ingawa DC wa KIinondoni, Jordan Rugimbana alifafanua mapema kabla ya Kamnada Kova kumaliza utata hivi punde. akisisitiza kuwa Dar ni shwari na watu walale kwa amani na utulivu kwa kuwa yeye Kamanda na vijana wake wapo kazini na Panya Road au wahalifu wengine hawawezi kuwazidi ujanja.

MWAKA MPYA WA WATANZANIA DMV

 Aliyekuwa mwakilishi wa Diaspora bunge la katiba Mhe. Kadari Singo akielezea shughuli za bunge hilo na jinsi gani alivyopigana kutetea swala la uraia pacha huku akiwasihi wanaDiaspora kubadili mtizamo wao kwa nchi yao.
Mwakilishi wa maswala ya uhamiaji Bi. Fatmata Barrier akifafanua sera ya uhamiaji ya Obama kuhusiana na kutoa vibali vya kazi kwa wasiokua na makaratasi kwenye sherehe ya mkesha ya Jumuiya ya Watanzania DMV iliyofanyika Lanham, Maryland Jumamosi Desemba 31, 2014

TATHMINI YA PAPA KAIJAGE KUHUSU MATUKIO MAKUBWA YA MUZIKI WA DANSI KWA MWAKA 2014…



​​BENDI MPYA
•Vijana Ngwasuma ilizinduliwa ndani ya Letasi Lounge (zamani Business Park ,Victoria) Ijumaa ya tarehe 07-Mar-2014.
•Yamoto Band yazinduliwa rasmi tarehe 21-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala.
•Utalii Band yazinduliwa Ijumaa ya tarehe 26-Sep-2014 ndani ya ukumbi wa MRC (Mikocheni Resort Centre)
•Kundi la Chuchu Sound liliibuka tena na kupiga show kadhaa katika ukumbi wa Max Bar Ilala. Baadaye kwa sababu kadhaa bendi ikapotea.
•Pia kulikuwa na bendi ambazo sio mpya lakini ndani ya mwaka 2014 ziliundwa upya. Bendi hizi ni Victoria Sound  na Ruvu Stars.
•Bendi nyingine zilizoanzishwa ndani ya mwaka 2014 ni JJ Band, bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe. Pia kuna Ruby Band. Bendi hizi 2 zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwanzoni mwa mwaka 2015.

UZINDUZI WA ALBUM MPYA
•Extra Bongo walizindua album ya “Mtenda Akitendewa” Jumamosi ya tarehe 22-Feb-2014 ndani ya Dar Live Mbagala.
•Talent Band (ya Hussein Jumbe) wazindua album ya “Kiapo Mara Tatu” Jumatano ya 30-Apr-2014 ndani ya Kisuma Night Pub, Temeke (zamani Sugar Ray)
•Christrian Bella azindua album ya “Nani Kama Mama” ndani ya Mzalendo Pub Jumamosi ya tarehe 30-Aug-2014
•Tarsis Masela katika viunga vya Ten Lounge (Business Park) Victoria azindua album ya “Acha Hizo” Ijumaa ya tarehe 21-Nov-2014
•Mashujaa Band yazindua album ya “Ushamba Mzigo” kwenye ziara za mikoani.

KILI MUSIC AWARD
•Kili Music Award 2014 ilifanyika Jumamosi ya tarehe 03-May-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Kulikuwa na jumla ya vipengele (categories) 8  vya muziki wa dansi. Washindi walikuwa kama ifuatavyo;
1. Mwimbaji Bora wa Kiume-Jose Mara (Mapacha Watatu)
2. Mwimbaji Bora wa Kike-Luiza Mbutu (Twanga Pepeta)
3. Rapa Bora-Fergusson (Mashujaa Band)
4. Wimbo Bora-Ushamba Mzigo (Mashujaa Band)
5. Bendi Bora-Mashujaa Band 6. Mtunzi Bora-Christian Bella (Malaika Music Band) 7. Producer Bora-Amorosso 8. Hall of Fame (Individual)-Hassan Rehani Bitchuka (Mlimani Park Orchestra)

WANAMUZIKI WALIOFARIKI
•Mpiga tumba wa Twanga Pepeta Soud Mohamed “MCD” afariki dunia Jumatatu ya tarehe 27-Jan-2014
•Mpiga bass wa Vijana Jazz, Maulid Mwangia afariki Jumatano tarehe 12-Mar-2014 na kuzikwa Alhamis tarehe 13-Mar-2014
•Mwanamuziki mkongwe Muhiddin Gurumo afariki dunia Jumapili ya tarehe 13-Apr-2014 na kuzikwa kijijini kwao Masaki, Kisarawe Jumanne ya tarehe 15-Apr-2014
•Mpiga gitaa wa Skylight Band, Chili Challa wa Skylight Band afariki dunia tarehe 17-Apr-2014.
•Amina Ngaluma “Japanese” afariki tarehe 15-May-2014  akiwa mji wa Phuket, Thailand.
•Mwanamuziki DIGITAL wa FM Academia afariki Ijumaa tarehe 18-Jul-2014.
•Ally Rashid “Mwana Zanzibar” ambaye mara ya mwisho alikuwa mpuliza sax wa Msondo Ngoma afariki tarehe 10-Oct-2014.
•Suzuki Sauti ya Malaika aliyepigia Extra Bongo katika album ya “Mjini Mipango” alifariki tarehe 15-Oct-2014
•Mwanamuziki Khamis Kayumba “Amigoulaus” afariki tarehe 09-Nov-2014.
•Mwanamuziki Shem Ibrahim Kalenga afariki dunia 15-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 16-Dec-2014 katika makaburi ya Kisutu.
•Mnenguaji Aisha Madinda afariki dunia tarehe 17-Dec-2014 na kuzikwa tarehe 19-Dec-2014.

MATUKIO MENGINE MAKUBWA
•Mdahalo wa kwanza wa aina yake wa kujadili muziki wa dansi wafanyika katika ofisi za TBC Jumamosi ya tarehe 05-Apr-2014 chini ya u-moderator wa Dacota Khamis, kuhudhuriwa na wadau karibia 30 na kuonyeshwa live na TBC2 na baadaye kuonyeshwa recorded na TBC1 kwenye kipindi cha “Nyumbani ni Nyumbani”
•Bendi ya Msondo Ngoma yafanya sherehe za maadhimisho ya kutimiza miaka 50. Maadhimisho yalianza Ijumaa ya tarehe 10-Oct-2014 ndani ya Leaders Club na kuhitimishwa TCC Chang’ombe Jumamosi ya tarehe 01-Nov-2014. Pia wanamuziki wa bendi walikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete, Alhamis ya tarehe 30-Oct-2014.
•Kwa mara ya kwanza tukio la “Usiku wa Msanii” lafanyika tarehe 25-Oct-2014 katika ukumbi wa Mlimani City. Marehemu Father Kanuti alipewa tuzo ya Humanitarian Award.
•Tarehe 09-Dec-2014, siku ya maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru na miaka 52 ya Jamhuri ya Tanganyika (Tanzania Bara), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla maalum iliyofanyika katika viwanja vya ikulu atoa nishani maalum kwa kundi zima la Atomic Jazz Band ya Tanga. Tuzo hiyo ni ya miaka 50 ya Muungano ya daraja la nne. Aliyepokea kwa niaba ya kundi ni mzee Stephen Hiza (Mgosingwa). Atomic Jazz Band imepewa nishani hiyo kutokana na kazi yao kubwa katika kulihamasisha taifa kuenzi muungano hususan kwa kupitia wimbo wao wa  “Tanzania Yetu”.
•Mpambano wa Msondo na Sikinde wafanyika mara mbili kwa kuandaliwa na Fred Ogot na kampuni yake ya Bob Entertainment. Mara ya kwanza ulifanyika siku ya sikukuu ya Eid Mosi (Eid al-Fitr) tarehe 25-Jul-2014 ndani ya TCC Chang’ombe. Mara ya pili umefanyika pia TCC Chang’ombe Christmas tarehe 25-Dec-2014. Kwenye mpambano wa mara ya pili, kwa mara ya kwanza tukio limesindikizwa na bendi ya Vijana Jazz Pambamoto “Saga Rumba”.
•MAONYESHO YA PAMOJA: Bendi 3 za FM Academia, Mapacha Watatu na Ruby Band zapiga pamoja Ijumaa ya tarehe 19-Dec-2014 ndani ya Mzalendo Pub. Yamoto Band mara kadhaa imefanya maonyesho ya pamoja kwa kupiga pamoja na Mapacha Watatu, Skylight Band na Twanga Pepeta. Pia Mlimani Park Orchestra wamepiga pamoja mara kadhaa na Machozi Band ya Lady Jaydee. Ruby Band walipiga pamoja na Twanga Pepeta Jumapili ya tarehe 28-Dec-2014 ndani ya Leaders Club
•Onyesho la Miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta lililokuwa lifanyike Jumamosi ya tarehe 20-Dec-2014 limeahirishwa hadi tarehe 31-Jan-2015 kutokana na kifo cha mnenguaji Aisha Madinda.
•Mechi ya mpira wa miguu kati ya kundi la BONGO DANSI na kundi la WATANASHATI WA MUJINI lafanyika katika viwanja vya Leaders Club Jumapili ya tarehe 23-Nov-2014. Matokeo yalikuwa suluhu 0-0. Kundi la BONGO DANSI mara kadhaa limefanya ziara ya kumtembelea Nguza Vicking na Papii Kocha ambao wapo gerezani Ukonga.
•Tarehe 26-Dec-2014, umoja wa wanamuziki wa dansi katika viwanja vya Karimjee wafanya dua maalum ya kumuombea Rais Jakaya Kikwete ili hali yake ya kiafya iimarike.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...