Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, January 9, 2015

Airtel kuzindua Airtel UNI 255 J-mosi maalum kwa Wanafunzi UDSM katika Viwanja vya Mabibo Hostel





Afisa Masoko wa Airtel Henrick Bruno akionyesha moja kati ya vocha za Airtel UNI255 maalum kwa vyuo vikuu nchini tayari kwa uzinduzi jumamosi hii.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole kupamba uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel UDSM 
 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imebainisha kuwa mwishoni mwa wiki hii itazindua rasmi huduma mpya maalum kwaajili ya kutoa huduma nafuu za mawasiliano kwa wanafunzi walioko vyuoni katika chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM ambapo hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo inayojulikana kama Airtel UNI 255 kwa vyuo vikuu vilivyopo Dar es salaam itafanyika katika viwanja vya Mabibo hostel 
 Akiongea kuhusiana na uzinduzi wa huduma hiyo Meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando amesema “Airtel Uni 255 ni huduma pekee yakibunifu toka Airtel Maalum kwa wanafunzi wa vyuo yenye kuwapa unafuu wa kuwasiliana wawapo chuoni, sasa wanafunzi wote wa chuo wanapotaka kupata nyongeza ya vile wanavyosoma kwenye mtandao huduma  hiii  ndio jibu sahihi kwao kutokana na unafuu wake kwenye inteneti, kupiga simu na hata sms. Huduma hii tayari tumeshaizindua kwa vyuo vikuu vingine vya Dodoma, Mbeya, Iringa, Mwanza na imeonyesha mafanikio makubwa sana kwa watumiaji wakiwemo wanafunzi na wale wote wanaotumia huduma hii maeneo ya vyuo”
 “Airtel tumeona ni vyema tuizindua hapa katika vyuo vya Dar es salaam wiki hii siku ya Jumamosi pale mabibo hostel ambapo mbali na uzinduzi kutakuwa na tamasha kubwa litakalopambwa na watoa burudani nguli akiwemo Ney wa Mitego, Roma Mkatoliki, Shilole pmaoja na DJ maarufu jiji Dj Zero aliongeza kusema Mmbando 
 Nae meneja wa huduma hiyo ya UNI 255 Anethy Muga alisema “Airtel tumeoana hii ni huduma maalum kwa wanafunzi na ndio maana tukaona ni vyema kuizindulia katika Hostel zao pale mabibo ambapo tunaamini wanafunzi wengi wa chuo kikuu hapa jijini wanaifahamu na wanaishi mabibo hivyo wanakaribishwa katika uzinduzi huo ambapo kiingilo chake ni BURE”
 Burudani zitakuwa zakutosha kupitia Airtel UNI 255  siku hiyo.
 Kampuni ya simu za mkononi ya airtel ilianzisha huduma ya UNI255 ili kuendana sambamba na mkakati wao wa kusaidia vyuo vikuu nchini kutumia ipasavyo huduma za mtandao ili kuboresha sekta ya elimu kwa lengo la kusaidia wateja wake walioko vyuoni kufikia malengo yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...