Marquee
tangazo
Sunday, September 25, 2011
NGUMI, KICK BOXING ZAPINGWA DAR ES SALAAM JANA
TIGO YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE YA MSINGI TOANGOMA
SIMBA WALIA NA WAAMUZI, WADAI UZEMBE WAO UNACHANGIA WACHEZAJI WAO KUUMIZWA
SIMBA WALIA NA WAAMUZI, WADAI UZEMBE WAO UNACHANGIA WACHEZAJI WAO KUUMIZWA
WATANZANIA WASHINDA SOUTH AFRICA
Johannesburg Afrika Kusini, wamefanya kufuru isiyotegemewa baada ya kuongoza katika hatua ya tano hapo juzi.
Lukuba ambaye tuliwasiliana naye moja kwamoja jana alisema ndoto ya washiriki wa Kitanzania ni kuendela kuvuta pesa ili kuubwaga umasikini na kuwatoa nishai wenzao wa Kenya
na Uganda ambao wamekuwa wakiwabeza kabla ya mashindano kuanza. Changamoto hiyo ya Guinness itaoneshwa na televisheni inayopendwa na watazamaji wengi nchini, ITV kwa wiki nane mfululizo. Washindi wa hatua zote nane watajiunga na wanasoka wannne waliostafu soka katika onyesho ambalo pia litashirikisha
iP SPORTS YAKAMILISHA UTENGENZAJI WA JEZI ZA MICHEZO
FAINALI ZA MCHEZO WA VISHALE ZAPAMBA MOTO TANGA
REMMY ONGALA FAUNDATION
About Remmy Ongala
‘Doctor’ Remmy, as his Tanzanian audience called him, suffered a stroke in 2001 and in later years was troubled with the effects of diabetes. He died in December 2010 at the age of 63 from kidney failure. Upon news of his death, the local radio stations played his music continuously.
KUNDI LA T.MOTO KUWASHA MOTO

[WANANDOA] LEO NATAKA KUSEMA KITU KIMOJA. HEBU KILA MMOJA...
ukisikia Paaa,ujue limeshabutukaa hiloo
Thursday, September 22, 2011
SUPER D , KINYOGOLI WATAMBA BONDIA WAO KUFANYA VIZURI
Pambano hilo ni la maandalizi kwa bondia huyo kutetea mkanda wake wa Oganaizesheni ya Ngumi za KUlipwa (TPBO) litakalofanyika jijini Tanga Septemba 30 mwaka huu ambapo atapambana na Alan Kamote wa jijini Tanga.
Akizungumzia maandalizi ya bondia huyo Super D alisema maandalizi ya bondia huyo ni mazuri na anafanya mazoezi chini ya kambi ya ngumi ya Kinyogoli Foundation.
"Nategemea bondia wangu kuibuka na ushindi katika pambano lake la Septemba la jumamosi, ambalo kwa kiasi kikubwa litamsaidia katika maandalizi yake katika pambano la Tanga ambalo litakuwa la raundi 10,"alisema Super D.
Alisema bondia huyo atapigania uzito wa kg. 60 light weight ambapo katika pambano lake la kesho atapigana raundi sita.
Seper D alisema mapambano hayo ni moja ya muendelezo wa kuendeleza vipaji vya mabondia mbalimbali ambapo amewaomba wadau kujitokeza ili kusaidia juhudi hizo zinazofanywa na kambi ya ngumi ya Ilala.
KLABU ZA NGUMI ZATAKIWA KUJIANDAA NA MICHUANO YA KAMANDA KOVA
Akizungumza Dar es Salaam , Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za ridhaa nchini (BFT), Makore Mashaga alisema klabu hizo zitakapojitokeza kwa wingi zitatoa changamoto kwa timu ya Taifa ambayo inajiandaa na mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
"Kwa sasa mabondia wetu wanaendelea na mazoezi kama kawaida chini ya kocha mkuu Hurtado Primentel ambapo nao watashiriki michuano ya Kova Cup kwa ajili ya kujiweka sawa,"alisema Mashaga.
Alisema michuano hiyo itatoa mabondia mbalimbali kutoka mikoa ya Pwani na Dar es Salaam ambapo watashiriki kama klabu huku kila moja ikiwania kombe hilo ambalo limeandaliwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Suleiman Kova.
Timu hiyo ya Taifa inafanya mazoezi yake katika uwanja wa ndani wa Tafa Dar es Salaam tangu iliporejea nchini kutokea Maputo Msumbiji ilipokuwa ikishiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika.
TAMASHA LA KWANZA LA BIA KUFANYIKA NCHINI
Mbunge Bi Zarina Madabida Awacharukia Wanaharakati
Mbunge wa Viti Maalum Bi.Zarina Madabida akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Mikocherni Dar es Salaam jana .Pamoja na mambo mengine pia aliwataka wana harakati kumwekea wakili Mkuu wa wilaya ya Igunga Bi.Fatuma Kimario katika kesi aliyoifungua wilayani humo kupinga udhalilishaji aliofanyiwa na wanachama wa Chadema hivi Karibuni.
"Nashindwa kuelewa TAWLA,TGNP,TAMWA na wanaharakati wengine wanaotetea haki za wanawake wamekaa kimya bila kutolea maamuzi suala tuwaeleweje. Hii inanipa mashaka makubwa,"alisema.
Bi. Madabida alisema kuwa wanaharakati hao siku zote wapo mstari wa mbele kutetea wanawake na watoto ikiwemo jamii, lakini anashangazwa na ukimya kuhusu utetezi wa Bi. Kimario.
Alisema mbona wanawake wakiwa wananyanyaswa wanakuwa mstari wa mbele kutetea lakini iweje leo hii aliyefanyiwa hivi ni mwanamke tena kiongozi lakini wamekaa kimya tuwaeleweje?.
"Hawa tuwaeleweje ni wanawaharakati au wao wanavyama vingine vya siasa, utetezi wao huko wapi inanipa mashaka,"alisisitiza
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Chama Cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania (TAMWA)Bi.Analelia Nkya alipoulizwa juu ya kimya walichonacho kuhusu kudhalilishwa na Bi. Kimario alishindwa kutoa tamko kuhusu udhalilishaji huo kwa madai kuwa wao wanashughulikia masuala ya jamii na wala siyo ya mtu mmoja.
"Sisi tumekuwa tukizungumzia masuala ya jamii na sio suala la mtu mmoja sasa wewe kama mwandishi ukiniuliza tumekaa kimya kuhusu kudhalilishwa kwa mwamamke mwenzetu nakushangaa sana,"alisema Bi. Nkya.
Hivi karibuni wafuasi wa CHADEMA walimkamata Mkuu huyo wa Wilaya na Kumdhalilisha kwa madai kuwa alikuwa anapanga njama za kuupatia ushindi CCM katika uchaguzi mdogo unaoendelea jimboni humo,wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa wilaya hiyo.
UBALOZI WA MAREKANI WADHAMINI WASANII WALIOSHIRIKI TAMASHA LA MTEMI MILAMBO TABORA.
Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.
Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.
Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru
Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.
Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.
KUNDI LA T-MOTO MODERN TAARAB LATUA DAR KUFYATUA SITA MPYA KWA MPIGO
Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland yatembela Bunge la Tanzania
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akieleza nafasi ya Bunge katika Maswala ya Mambo ya Nje kwa Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland Mhe. Ine Marie Erikson (Mb) mara baada ya kamati hiyo kutoka Finland kutembela Bunge la Tanzania kwa ziara ya kubadilishana uzoefu leo.
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao na Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland iliyofanya ziara katika Bunge la Tanzania kwa lengo la Kubadilishana uzoefu
Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama ya Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb) akimkabidhi zawadi kwa niaba ya Ujumbe wake Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya Nje kutoka Bunge la Finland Mhe. Ine Marie Erikson (Mb) mara baada ya kufanya ziara Bungeni kwa lengo la kubadilishana Uzoefu MUKAMA ATOA TATHMINI YA KAMPENI ZA CCM
KATIBU Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ya CCM wilaya ya Igunga mkoani Tabora, kutoa tathmini na mambo mbalimbali yaliyojiri katika kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga utakaofanyika Oktoba 2, mwaka huu. Kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma. Wednesday, September 21, 2011
STAR TIMES YAPATA WASHINDI WA PROMOSHENI YAO
WASANII WA TMK WANAUME CHEGE NA TEMBA WATEMBELEA OFISI ZA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA
![]() | |||
Wasanii wa kundi la wanaume TMK Chege na Temba wakiwa katika picha ya pamoja wakati walipotembelea katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza jijini London kabla ya kumaliza show zao nchini humo siku chache zilizopita. Vilevile waliweza kutembelea idara mbalimbali na kujionea jinsi gani Ubalozi wetu hapo jijini London unavyofanya kazi hususani katika idara nyeti ya Uhamiaji inayoongozwa na ofisa Ambokile na Kupiga Picha za pamoja wakiwa na Mh Naibu Balozi Mh Chabaka Kilumanga Pamoja na baadhi ya maofisa wa Ubalozi. |














