 |
| Mwanzilishi
wa Mbio za Mbuzi za Hisani Dar es Salaam, Paul Joynson-Hicks
(katikati) akizuingumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam laao
kuhusu mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Septemba 1 mwaka huu katika
Viwanja vya The Green, Barabara ya Kenyatta, jijini humo. Kushoto kwake
ni Mwenyekiti wa mbio hizo, Karen Stanley na baadhi ya wadhamini wa mbio
hizo. |
Dar es Salaam
MASHINDANO ya 12 ya Mbio za Mbuzi za Hisani yapo mbioni na yanatarajiwa kufanyika Septemba 1 Mwaka huu waandaaji wameeleza.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mbio hizo, Karen Stanley anasema “Mashindano yam bio za
Mbuzi za mwaka huu yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko ilivyowahi
kutokea”. Tuna mbio za mbuzi kama kawaida. Tuna aina mbalimbali za
vyakula kutoka kwa watayarishaji bora wa hapa jijini wakati wa mbio
hizo, michezo na burudani za watoto na michezo ya kupima uwezo wao kwa
umri wowote. Hii sio ya kukosa.
Watu zaidi ya 3000 huudhuria
mashindano haya kila mwaka na wengi hushiriki katika mashindano ya
mavazi ya aina yake ya kuvutia yenye zawadi za kuvutia.
Bi
Stanley anaongeza; “ Mwaka huu kukiwa na kauli mbiu ya ‘Zama hizo katika
nchi za Magharibi’ itawafanya watu wengi wakija huku wamevaa kama
wachunga ng’ombe wa kimarekani wa zamani ‘cowboys’ wakiwa na mabuti na
makofia makubwa, japo si lazima uje na muonekano huo.
Mbio za
mbuzi za mwaka huu zinatarajiwa kuanza saa 6.00 mchana hadi saa 12.00
jioni katika Viwanja vya The Green kwenye Barabara ya Kenyatta jijini
Dar es Salaam..
Ukiacha mbio hizo kuwa ni kitu cha kuburudisha, lakini pia zina makusudi mengine muhimu.
Tukio
hilo la kifamilia linalofanyika kila mwaka tayari limeshafanikiwa
kukusanya kiasi cha Shilingi milioni 544 (zaidi ya dola 345,000 kwa
kiwango cha sasa) kutoka kwa karibu makundi 50 ya wahisani wa ndani
tangu lilipoanza mwaka 2001. (Tazama maelezo chini kwa mbio za mwaka
huu.)
Asasi mbili zitakazopewa msaada mwaka huu ni, Kidzcare Tanzania na Kigamboni. Community Centre.
Asasi
ya Kidzcare huendesha kitujo cha watoto wenye mahitaji na kituo cha
watoto wadogo mjini Bagamoyo, Pwani na vituo vingine viwili Mkoani
Mbeya. Kwa pamoja vikiwa na watoto wanaokaribia 300.
Asasi ya
Kigamboni Community Centre hutoa elimu kwa watoto wadogo na shughuli
nyingine za ubunifu wa sanaa na michezo kwa ajili ya vijana ikisaidia
vijana takriban 300. Wacheza sarakasi wa asasi ya KCC watakuwa kivutio
kikubwa kwa watoto watakofika katika mbio za mbuzi za mwaka huu.
Mwanzilishi
wa Kidzcare,Rob Notman anasema, “Ukiangalia maisha ya mtoto mmoja
utaona ni jinsi gani yamebadilika, shukrani kwa ufadhili unaotokana na
fedha za Mbio za Mbuzi. Sio mabadiliko ya kimwili lakini pia maisha yote
kwa ujumla, ni ajabu”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kigamboni
Community, Nassoro Mkwesso anasema, “Watoto hapa hawana fursa nyingi,
lakini wale wanaokuja hapa kituoni wanaanza kuamini kuwa wanaweza kuwa
watu fulani. Baadhi wana ndoto fulani na KCC inawasaidia katika kufanya
ndoto zao kuwa kweli”.
Mwanzilishi wa Mbio za Mbuzi za Dar es
Salaam Paul Joynson-Hicks anasema, “Siri ya mafanikio za mbio hizi za
hisani ipo katika mchanganyiko wa burudani na nia ya kutaka kuleta
mabadiliko katika maisha ya watanzania. Tunachukua mitazamo yote kwa
makini mno.
“Na tusingeweza kufanya hayo kwa namna yoyote bila ya
wafadhili wetu, wale wanaolipa ili kumiliki mbio. Wamiliki wa mbio za
mwaka huu ni Hoteli ya Southern Sun, Shirika la Ndege la British
Airways, Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Coca-Cola, Kampuni ya Bia ya
Tanzania Breweries Limited, British Gas, aetna and Mantra Tanzania.”
Tiketi
moja ni Shilingi 5,000 na zitauzwa getini. Kwa maelezo zaidi tembelea
tovuti www.goatraces.com, au tuma barua pepe: goatraces@goatraces.com au
piga simu 0755 555 900.