Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, March 30, 2014

Ni Mwadui na Stand kupanda Ligi Kuu msimu ujao

Kocha wa Mwadui Shinyanga, Jamhuri Kihwelu 'Julio' akikaribia kuipandisha daraja timu hiyo


TIMU ya Mwadui Shinyanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu baada ya kuinyuka Toto Africans nyumbani kwao Mwanza kwa bao 1-0.
Mwadui inayofundishwa na Jamhuri Kihwelu 'Julio' kwa ushindi huo wa ugenini imefikisha jumla ya pointi 28 na imesaliwa na mechi moja, huku Toto Africans ikipoteza matumaini ya kurejea katika ligi hiyo.
Hii inatokana na Stand Utd pia ya Shinyanga iliyopo nafasi ya pili kuibutua JKT Kanembwa nyumbani kwao mjini Kigoma kwa mabao 3-2 na kufikisha jumla ya pointi 26 na kuendelea kuibana Mwadui ambao wamekuwa na upinzani mkubwa baina yao.
Toto iliyopo nafasi ya tatu imebakia na pointi 21 ambapo hata kama itashinda mechi yao ya mwisho haitaweza kuwafikisha popote na kuziacha timu pinzani za Shinyanga, Mwadui na Stand zikisubiri kujua hatma ya mmoja wao kupanda Ligi Kuu msimu wa 2014-2015 siku ya Aprili 5 mwaka huu.
Tayari timu mbili za Polisi Moro na Ndanda Fc zimeshafuzu ligi ya msimu ujao baada ya kuongoza kwenye makundi yao ya A na B.

Hivi ndivyo Shule ya Joyland ilivyowapa faraja yatima wa Chamazi


Wanafunzi wa Joyland Pre& Primary wakiwa wamejichangana na yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund huku walimu wao wakiwa wamesimama

Walimu wa Shule ya Joyland wakijitambulisha mbele ya hadhara mchana wa leo kabla ya kukabidhi msaada wao kwa yatima
Mkurugenzi wa Shule ya Joyland, Fred Otieno akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwa yatima wa kituo cha Yatima Trust Funds
Wanafunzi wa Joyland wakiwa wamekaa kando ya yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund
Baadhi ya yatima wanaolelewa na kituo cha Yatima Trust Funds wakiwa makmini kufuatilia matukio yaliyokuwa wakiendelea kwenye hafla ya kukabidhiwa misaada na Shule ya Joyland
Watoto wakiwa bize kufuatilia matukio kwenye hafla iliyofanyika leo Chamazi
Yatima wanaolelewa kituo cha Yatima Trust wakionyesha ujuzi wao wa kunengua
Wnachuana kucheza muziki uliokuwa unaporomoshwa
Kama Super Nyamwela! Dogo ana kipaji cha kucheza muziki nouma!
Bendi ya Shule ya Joyland ilikuwapo kuwatumbuiza yatima siku ya leo yaani ilikuwa faraja kubwa kwa watoto hao
Mkurugenzi wa Joyland Pre& Primary, Fred Otieno akiomba kabla ya shughuli kuanza...yaani kama Pastor
Ameen! Walimu na watoto wakitikia sala ya mambi kabla ya shughuli kuanza leo Chamazi.
Ameeen! Watoto wakiitikia dua
Baadhi ya yatima wakiwa wamewabeba wanafunzi wa Joyland waliowatembelea kituoni kwao leo na kukabidhiwa msaada ya vitru mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Mil. 5
Utoto bana! wenzake wanaangalia mbele yeye anaangalia nyuma, lakini ni raha tupu!
Baadhi ya walimu wa Joyland wakiwa katika pozi kuangalia usalama wa watoto wao na yatima waliowatembelea
Yaani hawa madogo walifanya hata wenzao wasahau kucheza muziki kuwashuhudia vizuri wanavyochuana kunengua kwa raha zao
We angalia mpambano ulivyokuwa halafu toa maoni yako unadhani nani aliibuka mkali wa kudansi
Mkaanga Chips huyu balaa kama Titina Alcapone au Komba Belou Mafwala

Sehemu ya msaada uliotolewa na Shule ya Joyland kwa Yatima Trust Funds
Madam Anna alikuwa bize na mtoto aliyempakata...uchungu wa mwana jamani!
baadhi ya walimu wa Joyland waliowatembelea yatima wa Chamazi
Walimu wa Joyland wakiwa katika pozi

Friday, March 28, 2014

KASEBA NA MASHALI WAPIMA UZITO KUPIGANA JUMAMOSI MARCH 29 PTA SABASABA


Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Thomasi mashali kushoto mpambano utakaofanyika PTA Sabasaba siku ya jumamosi march 29 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mabondia Thomasi Mashali kushoto na Japhert Kaseba wakiwa na mkanda ambao wataugombania katika ukumbi wa PTA sabasaba siku ya jumamosi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Promota wa mpambano huo Ally Mwazoa akizungumza mbele ya waandishi wa habari
Mabondia Alani Kamote wa Tanga kushoto pamoja na Karage Suba wakiwa na mkanda watakaougombania kesho kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Ally Mwazoa akisisitita jambo

Super D: Kocha anayejitolea kuinua mchezo wa ngumi nchini

Super D: Kocha anayejitolea kuinua mchezo wa ngumi nchini


  Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini, Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akikabizi vifaa vya mchezo wa masumbwi Gloves pamoja na DVD za mafunzo ya mchezo kwa Kocha wa GYM ya Uhuru uwanja wa Basket, Kariakoo  Mohamed Chipota kwa ajili ya kuamasisha mchezo  wa masumbwi katika eneo ilo na kuwapa moyo wa kuendelea na mazoezi wanaoshudia wengine wa pili kushoto ni Atanasi kibwe,Omari Bai, Raymond Mbwago na Mussa Sindano Vifaa hivyo pamoja na Dvd vina thamani ya shilingi laki mbili picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimkabidhi clip bandeji na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kwa bondia Mussa Mchopanga baada ya kumdunda Anton Idoa kwa K,o ya raundi ya pili bondia huyo ndie bingwa kwa sasa wa mkoa wa Dar ers salaam na anajiandaa na mashindano ya Majiji yatakayofanyika katikati ya mwaka huu Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



KIU kubwa aliyonayo katika mchezo wa ngumi ndiyo unaomfanya bondia wa zamani wa klabu za
Simba,  Reli  na Amana, Rajabu Mhamila 'Super D' ndiyo iliyomfanya kujitolea kwa hali na mali kuwasaidia na kuendeleza vipaji vipya vya mchezo huo.
Mwishoni mwa mwaka jana kocha huyo anayetambuliwa kimataifa na Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Duniani (AIBA) alifanya ziara mikoani ili  kuhamasisha ngumi akigawa pia DVD zenye (clips) za mapambano ya mabondia mbalimbali nyota ili watu wajifunze mchezo huo.
Pia mapema mwaka huu amejitolea akigawa vifaa vya michezo kwa baadhi ya klabu za ngumi lengo likiwa kuwahamasisha vijana kujifunza na kuucheza mchezo huo bila ya matatizo ya ukosefu wa vifaa.
Aligawa vifaa hivyo katika klabu ya Uhuru Gerezani, pia amekuwa akisaidia na kuuza vifaa vya ngumi kwa bei rahisi katika michuano na mapambano mbalimbali za ngumi za ridhaa na zile za kulipwa ili kusaidia kuendelea mchezo huo.
Super D, pia amekuwa akiendelea kuwanoa mabondia chipukizi katika klabu za Amana akisaidia na wazoefu wa kazi hiyo Habib Kinyogoli na Kondo Nassor na klabu yake ya Ashanti iliyoshirikina kufanya vyema michuano ya Kombe la Taifa na Klabu Bingwa ya ngumi.

Super D anasema japokuwa kazi ya ukocha wa ngumi imekuwa hailipi na pengine ndiyo sababu ya mabondia wengi wa zamani waliostaafu mchezo huo kutopenda kuifanya, lakini yeye anafurahia kwa kuona vijana waliopitia mikononi mwake wakipata mafanikio na kuwa tishio.
Baadhi ya vijana wanaotamba wakipitia mikononi mwake ni Erck Magana,Husein Pendeza, Mussa Mchopanga,Juma Bigrii, Ibrahim Class 'King Class Mawe', Idd Mnyeke, Mussa Sunga na wengineo.
"Nafarijika kuona vijana niliowaibua kupitia klabu ya Ashanti Boxing wakizidi kuwa tishio, nadhani muda si mrefu watavaa viatu vya akina Rashid Matumla, Joseph Marwa na wakali wengine," anasema.
Anasema bila kujali kama ananufaika au la, furaha yake ni kuona mchezo wa ngumi ukizidi kusimama na kuendelea kuibua vipaji vipya ambavyo anaamini watakuja kuwa faida ya baadaye kwa taifa.
Super D   baba wa watoto wawili, Zainabu Mhamila 'Ikota' (11) na Saada Swedi (16) mtoto wa kuasili, anasema kumekuwa na vikwazo vingi katika kuendeleza ngumi nchini hasa suala la wafadhili na wadhamini.
Anasema wafadhili na wadhamini wamekuwa wazito kujitokeza kuupiga tafu mchezo huo na mabondia kwa ujumla kitu ambacho hakujua kinasababishwa na nini ilihali huo ni mchezo kama michezo mingine.
"Tatizo kubwa katika ngumi ni suala la udhamini, ngumi zimesahauliwa sana na hata wafadhili kwa mabondia nalo ni tatizo, japo inaelezwa ubabaishaji unaofanywa na wasimamizi wa ngumi ni sababu," anasema.
Anasema ni wajibu wa wasimamizi wa ngumi na wadau kwa ujumla kupigana kurekebisha hali ya mambo ili kutoa ushawishi kwa wadhamini na wafadhili kujitokeza kuwapiga tafu.
Rajabu Mohammed Mhamila 'Super D' alizaliwa mwaka 1977 jijini Dar akiwa mtoto wa pili kati ya wanne wa familia yao na alianza kupenda michezo tangu akiwa mdogo.
Mwenyewe anasema aliyemuingiza kwenye ngumi ni baba yake mzazi, Mzee Mhamila 'Chuck Norris, aliyekuwa mnyanyua vitu vizito na 'gateman' wa ukumbi wa DDC Kariakoo aliyekuwa akiwalazimisha kufanya mazoezi bila kupenda akidai anataka wawe fiti.

Mazoezi hayo na kule kumuona akinyanyua vitu vizito vilimfanya taratibu ayafurahie mazoezi kabla ya kuanza kupenda ngumi kwa kuvutiwa na mabondia Muhammad Ali na George Foreman.
Anasema mwanzoni mwa miaka ya 1980 alipelekwa klabu ya Simba na mjomba wake aliyewahi kuwa bondia tishio nchini, Iraq Hudu 'Kimbunga' na ikawa mwanzo wa safari yake ndefu katika ngumi mpaka
Super D anasema mbali na yeye pia kaka yake Shaaban Mhamila "Star Boy',  na wadogo zake Rashid Mhamila 'Nature Fire' na 'Mohamed Hemed' 'Kadogo Ninja' wote walitamba kwenye ngumi enzi zao wakipigwa tafu na mazoezi ya baba yao aliyekuwa pia mwanamieleka.
Baada ya kupata mafanikio akiwa Simba akishiriki michezo kadhaa, alihama kujiunga klabu ya Reli kisha baadae Amana, ingawa hakupata mafanikio makubwa.
Anasema kati ya michezo yote aliyocheza hawezi kusahau pambano dhidi ya Roger Mtagwa anayeishia kwa sasa Marekani, ambapo anakiri aklichakazwa isivyo kawaida.
"Siwezi kumsahau Mtagwa kwani alinipa kichapo  kutokana na jamaa alijua ngumi na alileta yupinzani wa ali ya juu kwani nilipofika raundi ya tano
nilikuwa nimeumia taya," anasema.
Anamshukua kocha wake, Habib Kinyogoli pamoja na mabondia mahiri nchini kama  Maneno Osward, Japhet Kaseba, Kalama Nyilawila,Said Mbelwa,Fransic Miyeyusho pamoja na uongozi Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT)  kwa kumtia moyo katika juhudi zake za kuendeleza mchezo huo.

Thursday, March 27, 2014

KAMANDA WA CCM KAWE AISHA VONIALIS KATIKA KUMPOKEA ABDULAHAMANI KINANA LEO KAWE


Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis akiwa katika harakati ya kumpokea katibu mkuu wa CCM Kinana alipokwenda kuzindua tawi la bondeni
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis katikati akiwa na Msaidizi wa Diwani wa Kata ya Kawe Bi, Sara Kilo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa kata ya Kawe Bi, Jen Mkndya na  Mjumbe wa Halimashahuli kuu kata ya kawe Bi, Rehema Msuta
 Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis katikati akiwa na makamanda wenzie
Baadhi ya wana ccm wakimsubili Katibu mkuu wao kushoto ni Pius Mlekwa,Mwenyekiti wa vijana kata ya mbezi juu Felex Nyanga na Kada wa CCM Jems Rock Mwaikibinga
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis kulia akiwa na makamanda wenzie

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini Aisha Vonialis

Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis katikati akiwa na makamanda wenzie
Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis katikati akiwa na makamanda wenzie
Katibu mkuu wa ccm kinana akipandisha bendera ya chama anae onekana katikati ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis

Katibu mkuu wa ccm kinana akipandisha bendera ya chama anae onekana katikati ni Mjumbe wa maendereo ya wanawake katika mchezo wa masumbwi nchini, ambaye pia ni kamanda wa UVCCM Kawe,Bi, Aisha Vonialis
Katibu mkuu wa ccm Adbullahamani Kinana akizungumza na wakazi wa mbezi leo

MMJKT MABINGWA WA NGUMI MKOA WA DAR ES SALAAM

Bondia Hamisi Mputeni kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Victor Njaiti wakati wa mpambano wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam juzi Njaiti alishinda kwa pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Mohamed Chibumbuli kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Abdul Rashid  wakati wa mchezo wao katika mashindano ya klabu bingwa mkoa wa Dar es salaam Chibumbuli alishinda kwa pointi mchezo huo juzi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya MMJKT jana imeibuka mabigwa wa mashindano ya mkoa wa Dar es salaam baada ya kuvipiku vilabu nane vilivyoweza kujitokeza kushiliki mashindano hayo

na kutawazwa kuwa bingwa wa mkoa baadhi ya mabondia waliocheza fainal za mashindano hayo ni Hamisi Mrisho wa 'MMJKT' alisambalatishwa kwa pointi na bondia Oscar Richard wa 'Urafiki'   na Omari Mohamed wa urafiki akichezea kichapo kutoka kwa mwenzie John Mwambinga, na bondia anaekuja kwa kasi ya ali ya juu akitokea timu ya Ashanti ya ilala kwa sasa akichezea timu ya 'MMJKT'  alifanikiwa kumpiga John Christian wa 'Mgulani' Saleh Abdallah wa mgulani alishindwa kutamba mbele ya  Undule Langson wa Magereza

nae Jacobo Agusteno wa 'mgulani' alishindwa kufulukuta mbele ya Bosco Bakari wa 'MMJKT' katika mpambano mwingine uliowakutaniasha Festo Ngabo wa Magereza alishindwa kutamba mbele ya Victor Njaiti wa 'mmjkt' nae bondia Mohamedi Chibumbuli wa magereza alimsambalatisha vibaya bondia Said Saleh wa 'mavituzi'
 akizungumzia maandalizi ya mabondia wa mkoa wa Mwenyekiti wa chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam 'DABA' Akaroli Godfrey amesema
kwa sasa mabondia wa timu ya mkoa wa Dar es salaam wapo kambini wakijiandaa na mashindano ya majiji yatakayoanza Kampala Uganda April 2 mwaka huu 

timu hiyo ambayo ipo na makocha wazoefu wakiongozwa na David Yombayomba ,Ferdnand Nyagawa mazoezi yanayofanyika kila siku mgulani JKT, wakisaidiwa na Mazimbo Ally na Kameda Antony 

timu hiyo ina maitaji mbalimbalio ikiwemo kambi pamoja na kupeleka timu Uganda ambayo itagalimu milioni 16 kwa ajili ya kwenda kwenye mashindano
hayo ambapo mpaka sasa wamenda sehemu mbalimbali ikiwemo makampuni na kwa watu binafsi

ata hivyo akuna mafanikio yoyote hivyo kuwaomba wadau wa mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kusaidia timu hiyo ambayo inakabiliwa na mashindano ya majiji
   


UJENZI BOMBA LA GESI KUKAMILIKA JULAI



Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Katikati) akitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara. Wanaomsikiliza ni Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Salome Kingdom (Kushoto) na Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia).
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa makazi ya wafanyakazi katika kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
Mmoja wa wakaguzi kutoka Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Nancy Kitajo akistaajabu bomba za kusafirishia gesi zinazoelekea kwenye kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
Vongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
 Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
Na Saidi Mkabakuli mdau  wa matukiodaima.com Mtwara 

Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo.

Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa wakati.

“Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiki,” alisema Mhandisi Yagela.

Kwa mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa Julai kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya wafanyakazi imekamilika.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa kukamilika kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.

“Kukamilika kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam,” alisema Bibi Mwanri.

Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam unafanywa sambamba na ujenzi wa mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi Dar es Salaam. 

Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa.
Lengo la Dira ni  kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...