Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 8, 2010

kampuni ya uwakala wa bima ya African Trade Insurance Agency (ATI) yafunguliwa


ATI iko mbioni kuvunja rekodi ya bima nchini Tanzania, huku ikiinua wawekezaji na wakopeshaji nchini

DAR ES SALAAM, TANZANIA, Disemba 1, 2010 – Katika jitihada za kuongeza ufahamu na kuwafikia wateja, kampuni ya uwakala wa bima ya African Trade Insurance Agency (ATI) inaendesha mfululizo wa semina ya siku mbili inayolenga mawakala, maofisa wa benki na vyombo vya habari. Tangu kufunguliwa kwa ofisi yake hapa nchini mwezi Aprili mwaka huu, ATI imefanikiwa kukuza biashara yake nchini Tanzania kutoka kiwango cha thamani ya uendeshaji cha Dola milioni 11 za Kimarekani mwaka 2009 hadi kufikia zaidi ya Dola milioni 195 mwaka 2010 – ukuaji huo ukiwakilisha zaidi ya asilimia 1,000 na kunufaisha sekta za nishati, uzalishaji na huduma. Wakala huyo wa bima za aina mbalimbali pia amewezesha uwekezaji hapa nchini toka Kanada, Italia na Mauritius ambao thamani yake ya uwekezaji inazidi Dola milioni 24.

“Lengo la semina hizi ni kulielimisha soko la hapa nchini juu ya uwekezaji wetu wa kipekee na bidhaa zetu nyingine za bima za mikopo ya biashara. Huduma hizi zinaweza kuwalinda wauzaji wa bidhaa nje ya nchi wanaolenga masoko mapya, kulinda mabenki dhidi ya mikopo isiyolipwa pamoja na wawekezaji wanaolenga masoko yasiyo na usalama,” alieleza Stewart Kinloch, Afisa Mdhamini Mkuu wa ATI.

Kwa hapa nchini, manufaa, hasa katika hali ya sasa ya kiuchumi, yanaweza kuwa makubwa. Baadhi ya matatizo ya kila siku ya kibishara ambayo bima hii inaweza kusaidia kupunguza ni pamoja na:

* Wawekezaji na biashara za ndani zinazohitaji mikopo lakini zinashindwa kuafikiana masharti nafuu na wakopeshaji wa nchini au benki za nje kutokana na kutokuwa na vidhibiti vya kuaminika.
* Benki za ndani zinzlazimika kupunguza viwango vya mikopo kwa kuhofia uhakika wa wateja wa anayeomba mkopo hasa kwa wauzaji wa bidhaa nje ya nchi.
* Waagizaji bidhaa toka nje wanalazimishwa kuzilipia kwanza kwa sababu hawawezi kuafikiana masharti ya mikopo na wakopeshaji wa nje kutokana na kuhofiwa kushindwa kulipa.
* Wauzaji bidhaa nje wanaoingia hasara kutokana na kutolipwa na matatizo mengineyo wateja wao walioko Ulaya na kwingineko wanaposhindwa kulipa.

ATI inatoa aina mbili za kipekee za bima – bima dhidi ya hali ya kisisasa inayojulikana pia kama bima ya uwekezaji na bima ya mikopo ya biashara. Kwa pamoja bidhaa hizi zimesaidia kukuza ushindani wa wafanyabiashara wa Afrika wanaouza bidhaa nje na pia kuvutia uwekezaji toka nje katika muongo uliopita.

Bima ya mikopo ya biashara ni bidhaa ambayo wauzaji bidhaa nje wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini wamekuwa wakiitumia kwa manufaa makubwa kwa miongo mingi. Wauzaji wa nje toka kwenye masoko haya wana bima toka mashirika ya nchi zao zinazowalinda dhidi hatari kama vile kutolipwa, zinazowawezesha kufanya biashara popote duniani. Hali hii inawafanya wawe na uwezo wa ushindani kuliko wenzao wa Afrika ambao mara kwa mara wanatumia fedha taslimu dhidi ya hati au nyaraka zinazoidhinisha mikopo. ATI ni wakala wa mikopo ya uuzaji nje wa Afrika, anayetoa huduma nyingi kama hizi zinazoweza kuongeza ushindani wa bara la Afrika.

Kinagaubaga, bima dhidi ya hali ya kisiasa ni bima ambayo wawekezaji aidha wa Kiafrika au nje ya Afrika wanaweza kujiwekea ili kulinda biashara zao dhidi ya itikadi za serikali au vurugu za kisiasa zinazoweza kuwasababishia hasara. Hii inawapatia kinga wawekezaji na wakopeshaji ambao wangependa kuelekeza fedha zao nchini Tanzania.


Faida ya kipekee ATI iliyonayo ni kwamba nchi za Kiafrika kama Tanzania zimewekeza fedha zao ili kuwa mwanachama wa ATI, na hivyo serikali zao hazina sababu ya kusababisha madai yoyote. Wawekezaji wanahakikishiwa usalama na uhusiano huu na wamechagua bima ya ATI badala ya makampuni mengine ya nje ya bara la Afrika makusudi kwa sababu hii ni taasisi ya Kiafrika yenye uelewa mzuri wa changamoto na fursa zilizopo kwenye mazingira ya biashara ya hapa.

Ili kuongeza uelewa katika soko la Tanzania, Mwakilishi wa ATI nchini, Bw. Albert Rweyemamu na Bw. Stewart Kinloch wataendesha mfululizo wa warsha tarehe 6 na 7 Desemba kwenye hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.

African Trade Insurance Agency (ATI) ni wakala pekee wa bima anayejihusisha na bima zaidi ya moja katika sekta za uwekezaji na biashara. ATI ilianzishwa mwaka 2001 na nchi wanachama za Kiafrika kutoa huduma zitakazosaidia kuongeza uwekezaji toka nje kupitia huduma zenye bei nafuu kwa wawekezaji wa kimataifa. Mwaka 2006 ATI ilianzisha bima ya mikopo ya biashara ili kusaidia kulinda wauzaji bidhaa nje wa Kiafrika dhidi ya wateja wao wanaoshindwa kulipa.


Tangu 2001 ATI imefanikisha uwekezaji na biashara wenye thamani ya zaidi ya Dola bilioni 2 barani Afrika.

ATI imekuwa ikitunukiwa kiwango cha juu katika nguvu ya kifedha na uwezeshaji katika mikopo na taasisi ya Standard & Poor’s mfululizo tangu mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...